STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Shaa aweka kiporo Sifa Ujinga akisaka madansa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifTHyk2hW154PLhd-dO1ue1WNz2zW9kYykXLpBOfVnvl-fh6nXZJnuBAEdNktOq7o4NuUd03vtCRr8FauFMTCc7LAqrHGWcVnPG3LyYEb0IhQ070nKLFUBTlr2J0J4OiFyDTfdTKDGnKLE/s1600/SHAA.jpg
Shaa katika pozi

MCHAKATO wa kusaka madansa watakapamba jukwaa la msanii Sarah Kais 'Shaa' umeanza ukiendeshwa na mabosi wa msanii huyo, kituo cha Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa kituo hicho na meneja wa Shaa, Said Fella alisema tayari wameanza kupokea wasanii wanaotaka kuwa miongoni mwa madansa hao wanne kabla ya kuanza kuwafanyia usaili kisha wale watakaokithi viwango kushindanishwa kusaka madansa wanne wa kuunda kundi la Shaa.
Fella alisema mchakato wa kuwashindanisha madansa huo utafanyika kwa utaratibu maalum katika kundi zitakazotangazwa ndani ya wilaya ya Temeke kabla ya fainali ya mwisho kufanyika katika ukumbi mmoja maarufu hapa jijini Dar.
'Tumeshaanza kupokea madansa wanaotaka kuwania kuwa miongoni mwa madansa wanne wa Shaa, tutawachuja kisha wale watakapita watashindanishwa ili kusaka wanne wa mwisho watakaoambatana na Shaa katika maonyesho yake," alisema.
Aidha Fella alisema wimbo mpya na wa pili wa Shaa uitwao 'Sifa Ujinga' umeshakamilishwa na sasa unaandaliwa video yake ndipo vtyote viachiwe hadharani.
Pia alisema wameona isingekuwa vyema kuutoa wimbo huo mpya wakati wimbo wa 'Sugua Gaga' ulioachiwa hivi karibuni ukiendelea kutesa katika vituo vya redio na runinga.

Rais Kikwete awalilia waliokufa ajali ya Burdan

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/06/Jakaya-Kikwete-na.jpg
Rais Jakaya Kikwete
          THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Lt(Mst) Chiku Galawa kufuatia vifo vya watu 12 na wengine 71 kujeruhiwa baada ya basi Na. T610 ATR la Kampuni ya Burudani lililokuwa likitokea Korogwe kwenda Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Taula mapema asubuhi ya tarehe 12 Desemba, 2013.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 12 vilivyotokea tarehe 12 Desemba, 2013 huku wengine 71 wakijeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya Burudani walilokuwa wakisafiria kutoka Korogwe kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Taula”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.

Rais Kikwete amesema vifo vya watu hao ni pigo kubwa siyo tu kwa familia za watu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo, bali pia Taifa letu kwa ujumla ambalo limepoteza nguvu kazi muhimu iliyokuwa bado inahitajika kwa ujenzi wa Taifa.

“Kutokana na msiba huo mkubwa uliotokea katika eneo la Mkoa wako, ninakutumia Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu wewe Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Lt. (Mst) Chiku Galawa kwa kupoteza watu wengi kwa mara moja katika ajali hiyo.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, Amina”.

Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo, lakini amewahakikishia kwamba yuko pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.  Amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia wakiomboleza vifo vya ndugu zao.

Aidha Rais Kikwete amesema anawaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida, ili waungane tena na ndugu na jamaa zao na kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa kabla ya kutokea kwa ajali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Desemba, 2013

Hii ndiyo taarifa rasmi ya ajali ya basi la Burudan



WATU 12 wamekufa papo hapo huku wengine 71 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali basi la abiria la Kampuni ya Burdan kupinduka katika kona ya Kwaluguru kata ya Kabuku wilayani Handeni Mkoani Tanga leo asubuhi.

Basi hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Korogwe Dar es Salaam lilipata ajali majira ya ya asubuhi kutokana na mwendo kasi uliopelekea dereva kushindwa kumudu gari hilo na kuacha njia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,Costantine Massawe amethibitishwa kutokea kwa ajali hiyo,na kusema majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Wilaya Magunga kwa ajili ya matibabu.

Kamanda Massawe alitaja namba za gari hilo kuwa ni T.610 ATR aina ya Nisani lilikuwa likitokea Korogwe likielekea Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Luta Mpenda ambaye alipoteza maisha papo hapo.

Mwendo kasi unatajwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali ambayo majeruhi imeitaka serikali kusimami kikamilifu na kuchukua hatua kwa madereva wanao kikuka sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akaiomba serikali kuboresha huduma za afya kwenye hosptali hiyo ili kuondokana na changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa damu.

Majeruhi wengine 19 wamepelekwa katika kospitali ya KCMC Moshi na Moi Dar es Salaam kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

BARAZA lafungia shindano la Miss Utalii Tanzania, kisa...!

BARAZA  la Sanaa la Taifa (BASATA) limeyafungia mashindano ya urembo ya Utalii 'Miss Tourism Tanzania' kutokana na kukiuka taratibu na maagizo ya baraza hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari Mkuu wa baraza hilo, Agness Kimwaga inaelezwa kuwa Miss Utalii imefungiwa kwa sababu kuu mbili;
taarifa hiyo ya BASATA inasomeka kama ifuatavyo;

Baraza la sanaa Taifa limefungia mashindano hayo kutokana na sababu kuu mbili,kwamza mashindano Miss Tourism Tanzania 2013 kushindwa kufanya tathmini ya mashindano ya miss Tourism 2012/2013 kwa muda uliokubalika baada ya maonyesho hayo kufanyika,na sababu nyingine kwamba Miss Tourism Tanzania kukiuka masharti,kanuni,miongozo na taratibu za uendesheaji wa mashindano ya urembo kama zilivyowekwa na serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa kwa hiyo hizo ndo sababu zilizofanya sisi kulifungia shindano hili kwa muda usiojulikana"
"Tukiwa na ushahidi uliokamilika kutoka kwa warembo wenyewe waliohusika hatuwezi kufungia kitu pasipo ushahidi,kumbuka mashindano haya yanapokuwa yanaendelea serikali hatukai kwenye zile kambi kwa muda wote wanaokaa kwa kuwa mara nyingi tunapokwenda kutembelea warembo wakiwa kwenye zile kambi tunawaambia popote panapokua na tatizo kunakiukwa taratibu tunawapa taratibu tunazotaka zifuatwe zinapokiukwa wao watupe taarifa,tusipopata taarifa sisi hatuwezi kumfungia mtu pasipo kuwa na taarifa tumekua na taarifa za uhakika toka kwa warembo wenyewe ndo maana tumechukua hatua".
"Tunasema kwamba tunapoendesha shughuli yoyote ya sanaa usifanye vitu ambavyo vinaweza kumdharirisha mtazamaji au mhusika anaefanya kitu kile kwa hiyo kuna vitu ukifanya vinaweza kumdharirisha mtu kwa njia moja au nyingine umekiuka kanuni na taratibu kumnyanyasa mfano kijinsia,kwanza kabla ya kukufungia tunakupa pre ya muda na tunakwambia umekosea nini na tunakupa muda kurekebisha yale makosa yaliyofanyika,kama unakumbuka zamani Miss Tanzania watu walikua wanapanda na yale mavazi ya ufukweni yakiwa tupu bila kufunga jukwaani lakini taratibu tumewaambia hairuhusiwi kupanda hivyo,kwa sababu ni lazma wakaguliwe wakiwa vile hakuna watazamaji wanaokuwepo kwa muda huo,lakini kabla hatujakufungia tunakupa barua kwamba umekosea A,B,C,D na ufanye marekebisho kwenye hatua hiyo vinginevyo tunakufungia,sasa kama umetuma barua na hakuna kilichorekebishwa pia inakua ni kinyume na utaratibu kwamba tunafika lakini si kila siku sisi huwa tunafika tunawapa wale warembo semina lakini si siku zote wanazokaa kambini sisi tunafika,siwezi kuwa na taarifa bila kuniambia mtu aliekuepo hapo.


Kenya ndiye bingwa mpya wa Chalenji 2013

http://www.standardmedia.co.ke/images/sunday/Harambee-09082013.jpg
Harambee Stars

WENYEJI wa michuano ya Kombe la Chalenji, Kenya Harambee Stars imefanikiwa kutawazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuinyuka Sudan kwa mabao 2-0 katika pambano lililochezwa jioni hii jijini Nairobi.
Harambee iliyowaondoa patupu Tanzania katika mechi ya nusu fainali, ilipata mabao yake yaliyoizima Sudan kupitia kwa Alain Mwanga na kunyakua taji lake la sita la michuano hiyo na mara ya kwanza kwa taifa hilo kutwaa taji hilo katika ardhi yake tangu ilipofanya hivyo mwaka  1983.
Mara ya mwisho kwa Kenya kunyakua taji hilo ilikuwa mwaka 2002 walipoitungua Tanzania Bara waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa mabao 3-2. Katika fainali za mwaka jana, Kenya inayosherehekea miaka 50 ya Uhuru wa taifa hilo ilifika fainali dhidi ya Uganda na kufungwa, lakini safari hii wamekomaa na kunyakua taji hilo.
Michuano hiyo ilishuhudia Salah Ibrahim kunyakua tuzo la Mfungaji Bora akifunga mabao matano.
Hongera Kenya, Hongera Harambee Stars kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru na Taji la Chalenji katika ardhi yenu baada ya miaka 30 iliyopita.

Kili Stars bado gonjwa Chalenji 2013

 
KILIMANJARO Stars bado haijapata dawa ya kufanya vyema kwenye mechi zake za kuwania ushindi wa tatu baada ya jioni hii kupoteza mchezo kwa Zambia.
Kili Stars inashiriki mechi ya kusaka mshindi wa tatu kwa mara ya tatu mfululizo toka mwaka 2011 na mara zote imekuwa ikiambulia vipigo kama ilivyokuwa jioni hii kwa Chipolopolo walioshinda kwa mikwaju ya penati.
Timu hizo mbili zilimaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1 na kuingia hatua ya kupigiana penati na Kili Stars kunyukwa kwa mikwaju 6-5. 
Kipa Ivo Mapunda aliendelea kuonyesha ushujaa kwa kupangua penati mbili, lakini hiyo haikusaidia kwa vile wachezaji wa Tanzania walikosa penati tatu.
Katika muda wa kawaida, Zambia ilianza kupata bao kupitia kwa Ronald Kampamba katika dakika ya 51 kabla ya Kili Stars kusawazisha kupitia nyota wa pambano hilo, Mbwana Samatta dakika ya 65. Kwenye penati Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi' walipata penati zao, huku Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani wenyewe walikosa na kumaliza wakishika nafasi ya nne kwa mara ya tatu.

Nani bingwa mpya wa Chalenji 2013, Kili Stars kama kawa....!


MICHUANO ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kufikia tamati leo ambapo bingwa mpya atajulikana wakati wenyeji Kenya, Harambee Stars itakapovaana na Sudan 'Falcons' katika pambano la fainali.
Watanzania waliotumbukiwa nyongo na michuano hiyo baada ya timu zao kushindwa kufurukuta watasubiri kuona kama Kili Stars itakayoumana na Zambia itaambulia nini katika mchezo wa mshindi wa tatu.
Hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa Tanzania Bara kucheza hatua hiyo na mara zote imeambulia patupu mbele ya wapinzani wao.
Kili Stars iliyokuwa imewapa matumaini makubwa mashabiki wa kurejea na taji baada ya kulitwaa mara ya mwisho mwaka 2010 michuano ikifanyika Tanzania, licha ya kuivua taji Uganda, ilikwama kwa Kenya hatua ya nusu fainali.
Hivyo mchana wa leo itavaana na Chipolopolo kabla ya kupisha pambano la Kenya na Sudan ili kuandikisha bingwa mpya baada ya The Cranes kulitema taji lake.
Mechi zote za leo zitachezwa kwenye uwanja wa Nyayo na pambano la awali litachezwa kuanzia saa 8 mchana kabla ya fainali kupigwa jioni, huku Kenya wakijiamini watalinyakua taji hilo baada ya kulikosa tangu ilipotwaa mara ya mwisho mwaka 2002 nchini Tanzania.
Kabla ya mechi hizo kutakuwa na pambano la kukata na shoka la kukumbushia vipaji halisi vya Afrika Mashariki wakati timu ya wazee ya Tanzania itakapovaana na wenzao wa Kenya.
Hata hivyo pambano hilo litachezwa uwanja wa City, Nairobi majira ya saa 7 mchana na kisha shughuli zote kuhamia Nyayo Stadium kuhitimisha michuano hiyo.

Arsenal yafa ikifuzu 16 Bora, Neymar apiga hat trick ya kwanza Barca ikiua

Pilikapilika za Arsenal dhidi ya wenyeji wao Napoli

Neymar akitupia bao kambani

Demba Ba akifunga bao lake lililoipa Chelsea ushindi
VINARA wa Ligi Kuu ya Engalnd Arsenal imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora lakini wakiangukia pua kwa kunyukwa mabao 2-0 na Napoli ambayo hata hivyo itacheza sasa Europa League licha ya ushindi huo wakiwa nyumbani.
Arsenal iliyokuwa kinara wa kundi lake kabla ya mechi ya usiku wa jana ilikumbana na kipigo hicho kilichowafanya washike nafasi ya pili na kuungana na Borussia Dotmund kucheza hatua ya mtoano kwa uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Napoli yamefungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 73 Callejon dakika ya 90, na kuifanya timu hiyo nayo kufikisha pointi 12 lakini ikiwa na uwiano mdogo wa mabao na kukamata mafasi ya tatu na kuangukia ligi ya Ulaya ndogo na timu nyingine ikiwamo Juventus waliolala bao 1-0 mbele ya Galatasaray mapema jana.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo kuhitimisha hatua ya makundi, Barcelona licha ya kuwakosa Andres Iniesta, Leo Messi na Cesc Fabregas iliichapa Celtic kwa mabao 6-1.
Hat trick ya kwanza ya nyota wao mpya toka Brazil, Neymar na mengine ya  Gerrard Pique, Pedro na Tello yalitosha kuifanya vinara hao wa La Liga kukalia uongozi wa kundi hilo ikiwa ilishatangulia 16 Bora mapema.
Nao Chelsea ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya  Steaua Bucharest shukrani ikienda kwa Demba Ba aliyefunga dakika ya 11 ya mchezo huo uliochezwa darajani.
Marseille ya Ufaransa ilimaliza mechi zake za makundi bila ushindi wowote baada ya jana kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Wanafainali wa mwaka uliopita Borussia Dortmund waliokuwa ugenini, huku Atletico Madrid weakishinda mabao 2-0 dhidi ya Porto.
Timu ya Schalke 04 ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Basel, huku Austria Vien iliisasambua Zenith kwa mabao 4-1 na AC Milan ikiwakomboa Waitalia kwa kufuzu hatua ya 16 Bora baada ya sare isiyo na mabao dhidi ya Ajax.
Orodha kamili ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bota katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo;
Manchester  Utd, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Galatasaray, PSG, Olympikaous,
Bayern Munich, Manchester City, Chelsea, Schalke 04, Borussia Dotmund, Arsenal, Atletico Madrid, Zenith, Barcelona na Ac Milan.

Breaking Newzz: Watu 12 wafariki ajali ya basi Korogwe-Tanga

Picha haihusiani na habari hii ila ni baadhi ya ajali zinazopoteza uhai wa watanzania wenzetu barabarani.
AJALI zimeendelea kunyofoa roho xa wenzetu baada ya watu 12 kuripotiwa kufariki katika ajali ya basi lililotokea Korogwe Tanga, huku wengine wakiachwa hoi na majeraha ya ajali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa hivi punde na Radio One, abiri hao walikumbwa na mkasa huo baada ya basi walililowa wakisafiria la Burudan kutoka Korogwe kwenda Dar kuacha njia yna kupinduka katika kijiji cha Taula, wilayani Handeni.
Taarifa zaidi zitawajia kujua kinachoendelea katika ajali hiyo ambayo ni mfufulizo wa matukio yanayopoteza uhai wa watanzania wenzetu na wengine kuachwa wakina ulemavu wa kudumu.