STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Nani bingwa mpya wa Chalenji 2013, Kili Stars kama kawa....!


MICHUANO ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kufikia tamati leo ambapo bingwa mpya atajulikana wakati wenyeji Kenya, Harambee Stars itakapovaana na Sudan 'Falcons' katika pambano la fainali.
Watanzania waliotumbukiwa nyongo na michuano hiyo baada ya timu zao kushindwa kufurukuta watasubiri kuona kama Kili Stars itakayoumana na Zambia itaambulia nini katika mchezo wa mshindi wa tatu.
Hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa Tanzania Bara kucheza hatua hiyo na mara zote imeambulia patupu mbele ya wapinzani wao.
Kili Stars iliyokuwa imewapa matumaini makubwa mashabiki wa kurejea na taji baada ya kulitwaa mara ya mwisho mwaka 2010 michuano ikifanyika Tanzania, licha ya kuivua taji Uganda, ilikwama kwa Kenya hatua ya nusu fainali.
Hivyo mchana wa leo itavaana na Chipolopolo kabla ya kupisha pambano la Kenya na Sudan ili kuandikisha bingwa mpya baada ya The Cranes kulitema taji lake.
Mechi zote za leo zitachezwa kwenye uwanja wa Nyayo na pambano la awali litachezwa kuanzia saa 8 mchana kabla ya fainali kupigwa jioni, huku Kenya wakijiamini watalinyakua taji hilo baada ya kulikosa tangu ilipotwaa mara ya mwisho mwaka 2002 nchini Tanzania.
Kabla ya mechi hizo kutakuwa na pambano la kukata na shoka la kukumbushia vipaji halisi vya Afrika Mashariki wakati timu ya wazee ya Tanzania itakapovaana na wenzao wa Kenya.
Hata hivyo pambano hilo litachezwa uwanja wa City, Nairobi majira ya saa 7 mchana na kisha shughuli zote kuhamia Nyayo Stadium kuhitimisha michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment