STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Arsenal yafa ikifuzu 16 Bora, Neymar apiga hat trick ya kwanza Barca ikiua

Pilikapilika za Arsenal dhidi ya wenyeji wao Napoli

Neymar akitupia bao kambani

Demba Ba akifunga bao lake lililoipa Chelsea ushindi
VINARA wa Ligi Kuu ya Engalnd Arsenal imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora lakini wakiangukia pua kwa kunyukwa mabao 2-0 na Napoli ambayo hata hivyo itacheza sasa Europa League licha ya ushindi huo wakiwa nyumbani.
Arsenal iliyokuwa kinara wa kundi lake kabla ya mechi ya usiku wa jana ilikumbana na kipigo hicho kilichowafanya washike nafasi ya pili na kuungana na Borussia Dotmund kucheza hatua ya mtoano kwa uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Napoli yamefungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 73 Callejon dakika ya 90, na kuifanya timu hiyo nayo kufikisha pointi 12 lakini ikiwa na uwiano mdogo wa mabao na kukamata mafasi ya tatu na kuangukia ligi ya Ulaya ndogo na timu nyingine ikiwamo Juventus waliolala bao 1-0 mbele ya Galatasaray mapema jana.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo kuhitimisha hatua ya makundi, Barcelona licha ya kuwakosa Andres Iniesta, Leo Messi na Cesc Fabregas iliichapa Celtic kwa mabao 6-1.
Hat trick ya kwanza ya nyota wao mpya toka Brazil, Neymar na mengine ya  Gerrard Pique, Pedro na Tello yalitosha kuifanya vinara hao wa La Liga kukalia uongozi wa kundi hilo ikiwa ilishatangulia 16 Bora mapema.
Nao Chelsea ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya  Steaua Bucharest shukrani ikienda kwa Demba Ba aliyefunga dakika ya 11 ya mchezo huo uliochezwa darajani.
Marseille ya Ufaransa ilimaliza mechi zake za makundi bila ushindi wowote baada ya jana kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Wanafainali wa mwaka uliopita Borussia Dortmund waliokuwa ugenini, huku Atletico Madrid weakishinda mabao 2-0 dhidi ya Porto.
Timu ya Schalke 04 ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Basel, huku Austria Vien iliisasambua Zenith kwa mabao 4-1 na AC Milan ikiwakomboa Waitalia kwa kufuzu hatua ya 16 Bora baada ya sare isiyo na mabao dhidi ya Ajax.
Orodha kamili ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bota katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo;
Manchester  Utd, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Galatasaray, PSG, Olympikaous,
Bayern Munich, Manchester City, Chelsea, Schalke 04, Borussia Dotmund, Arsenal, Atletico Madrid, Zenith, Barcelona na Ac Milan.

No comments:

Post a Comment