STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Kenya ndiye bingwa mpya wa Chalenji 2013

http://www.standardmedia.co.ke/images/sunday/Harambee-09082013.jpg
Harambee Stars

WENYEJI wa michuano ya Kombe la Chalenji, Kenya Harambee Stars imefanikiwa kutawazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuinyuka Sudan kwa mabao 2-0 katika pambano lililochezwa jioni hii jijini Nairobi.
Harambee iliyowaondoa patupu Tanzania katika mechi ya nusu fainali, ilipata mabao yake yaliyoizima Sudan kupitia kwa Alain Mwanga na kunyakua taji lake la sita la michuano hiyo na mara ya kwanza kwa taifa hilo kutwaa taji hilo katika ardhi yake tangu ilipofanya hivyo mwaka  1983.
Mara ya mwisho kwa Kenya kunyakua taji hilo ilikuwa mwaka 2002 walipoitungua Tanzania Bara waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa mabao 3-2. Katika fainali za mwaka jana, Kenya inayosherehekea miaka 50 ya Uhuru wa taifa hilo ilifika fainali dhidi ya Uganda na kufungwa, lakini safari hii wamekomaa na kunyakua taji hilo.
Michuano hiyo ilishuhudia Salah Ibrahim kunyakua tuzo la Mfungaji Bora akifunga mabao matano.
Hongera Kenya, Hongera Harambee Stars kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru na Taji la Chalenji katika ardhi yenu baada ya miaka 30 iliyopita.

No comments:

Post a Comment