STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 12, 2013

Kili Stars bado gonjwa Chalenji 2013

 
KILIMANJARO Stars bado haijapata dawa ya kufanya vyema kwenye mechi zake za kuwania ushindi wa tatu baada ya jioni hii kupoteza mchezo kwa Zambia.
Kili Stars inashiriki mechi ya kusaka mshindi wa tatu kwa mara ya tatu mfululizo toka mwaka 2011 na mara zote imekuwa ikiambulia vipigo kama ilivyokuwa jioni hii kwa Chipolopolo walioshinda kwa mikwaju ya penati.
Timu hizo mbili zilimaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1 na kuingia hatua ya kupigiana penati na Kili Stars kunyukwa kwa mikwaju 6-5. 
Kipa Ivo Mapunda aliendelea kuonyesha ushujaa kwa kupangua penati mbili, lakini hiyo haikusaidia kwa vile wachezaji wa Tanzania walikosa penati tatu.
Katika muda wa kawaida, Zambia ilianza kupata bao kupitia kwa Ronald Kampamba katika dakika ya 51 kabla ya Kili Stars kusawazisha kupitia nyota wa pambano hilo, Mbwana Samatta dakika ya 65. Kwenye penati Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi' walipata penati zao, huku Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani wenyewe walikosa na kumaliza wakishika nafasi ya nne kwa mara ya tatu.

No comments:

Post a Comment