STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 10, 2016

Yanga yawafuata Simba Dar, watolewa na URA

YANGA imeifuata Simba baada ya kutolewa na URA kwa penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 matokeo yakiwa 1-1.

Pambano limeisha Yanga, URA kwenye penalti

PAMBANO la nusu fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi, kati ya Yanga na URA limemalizika baada ya dakika 90 kuisha matokeo yakiwa bao 1-1.
Kwa sasa timu zinajiandaa kupigiana penalti. Ngoja tuone mambo yatakuwaje kwa wababe hao wa Tanzania na Uganda.

SAMATTA NAHIODHA MPYA WA TAIFA STARS

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amemtangaza mshambuliaji Mbwana Ally Samatta kuwa Nahodha mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’. Akizungumza na leo, Mkwasa amesema kwamba uamuzi huo umetokana na kazi nzuri ya Samatta kuitangaza Tanzania na Taifa Stars kimataifa. “Anastahili kuwa Nahodha wa Taifa Stars kuanzia sasa, na ingawa tumekuwa na Nahodha ambaye anastahili kuendelea, lakini tumeona kitu pekee cha kumlipa Samatta kwa sasa ni beji ya Unahodha,”amesema Mkwasa.

Mkwasa amesema kuanzia sasa Cannavaro atakuwa Nahodha wa kikosi cha wachezaji wanaocheza nyumbani kwa ajili ya michuano ya CHAN, wakati John Bocco atakuwa Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars chini ya Samatta.
Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika katika sherehe zilizofanyika usiku wa Alhamisi ukumbi wa mikutano wa Kimataifa mjini Abuja.
Samatta alipata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad Bounedjah amepata pointi 63.
Mafanikio ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa ukanda w Afrika Mashariki na Kati kushinda tuzo kubwa ya Afrika, yanakuja baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake nane.
Aidha, Samatta sasa ndiye anaweza kuitwa Mchezaji Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania – bada ya miaka mingi ya kutokuwa na uhakika wa nani apewe sifa hiyo.
Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa msimu mmoja akitokea African Lyon iliyomtoa Mbagala Market, ambayo ilimuibua Kumbagulile FC ya kwao, Mbagala.
Chanzo-Bin Zubeiry

URA wanachomoa bao URA 1, Yanga 1

http://urafc.co.ug/wp-content/uploads/2015/02/URA-Peter-Lwasa-300.jpg
PETER Lwasa aliyeingia kipindi cha pili, anaisawazishia bao URA kutokana na wachezaji wa Yanga kucheza Offside-trick ambapo mabeki walidhani mfungaji ameotea, lakini bado ndivyo tena. Yanga 1 URA 1

Tetesi za usajili majuu zipo hivi

http://i2.walesonline.co.uk/incoming/article6494703.ece/ALTERNATES/s615/1Gareth-Bale.jpgDIRISHA la usajili kwa mwezi Januari lipo wazi na klabu kadhaa zimeanza kuchangamkia kwa kunyakua nyota mbalimbali, huku tetesi nyingine zikizidi kuenea kila uchao.
Straika wa Real Madrid, Gareth Bale anatarajiwa kukataa maombi ya kutoka Manchester United na Chelsea kufuatia nyota huyo wa kimataifa wa Wales kutaka kuendelea kubakia Santiago Bernabeu. Pia inaelezwa kuwa Klabu ya Manchester United inaripotiwa kujipanga kumchukua meneja wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kama mbadala wa Louis van Gaal, huku meneja wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc naye akitajwa kufikiriwa katika nafasi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa Sunday Mirror. 
Kwingineko klabu ya Tottenham Hotspurs inajipanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy kwa mkopo majira haya ya kiangazi, huku Manchester United inataka kitita cha paundi milioni 24 kwa ajili ya Marouane Fellaini lakini hawatakubali kiungo huyo kuondoka kwa mkopo. Pia klabu hiyo ya Manchester United inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Mainz Yoshinori Muto kwa kitita cha paundi milioni 12 hii ni kwa mujibu wa Sunday Mirror.
The Suna lenyewe limeeleza kuwa Klabu ya Manchester City imeingia katika kinyang’anyiro cha paundi milioni 80 na Real Madrid na Paris Saint-Germain kama Eden Hazard ataamua kuondoka Chelsea kipindi hiki cha majira ya kiangazi, huku Chelsea nayo ikidaiwa kuwa inamuwinda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ili aweze kuwa mbadala wa Guus Hiddink pindi atakapomaliza muda wake mwishoni mwa msimu huu.

Tambwe aifungia Yanga bao

AMISSI Tambwe ameifungia Yanga bao la mapema na kuifanya iende mapumziko ikiwa mbele dhidi ya URA ya Uganda. Kipindi cha pili kimeanza matokeo yakiwa bado ni 1-0, Yanga wakiwa mbele.
Matokeo yakibaki hivi Yanga itakutana na Mtibwa katikam fainali za Kombe la Mapinduzi kama ilivyokuwa mwaka 2007.

Spurs chupuchupu, Chelsea yapeta Kombe la FA

Harry Kane akishangilia penalti yake iliyoiokoa Spurs kulala nyumbani
WAKATI Chelsea ikivuka hadi raundi ya nne baada ya kuifunga timu ya Scunthorpe kwa mabao 2-0 katika mechi ya mfululizo wa michuano ya Kombe la FA, Tottenham hotspur ikiwa nyumbani ilinusurika kulala baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Penalti ya Harry Kane katika dakika za lala salama iliiokoa Spurs kulala kwa Leichester City, huku Swansea City iking'olewa na Oxford United kwa mabao 3-2.
Chelsea wenyewe wakiwa nyumbani kwao Stamford Bridge ilipata ushindi wa mabao 2-0 na kuungana na vigogo wengine wa Ligi Kuu kufuzu raundi nyingine ya michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Arsenal iliifumua Sunderland jana Jumamosi kwa mabao 3-1.



Simba yatemeshwa taji, Mtibwa hiyoo fainali za Mapinduzi

Ibrahim Rajab 'Jeba', akichuana na Mohammed Tshabalala wa Simba jioni ya leo na Simba kulala bao 1-0
NDIVYO hivyo tena. Simba imetemeshwa taji lake la Kombe la Mapinduzi baada ya kulala bao 1-0 kwa Mtibwa Sugar.
Bao pekee la sekunde chache kabla ya mapumziko lililofungwa na Ibraihm Rajab 'Jeba' lilitosha kuirudisha Simba jijini dar es Salaam na kuiacha Mtibwa ikitangulia fainali yao ya tano.
temesha Simba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kuifungasha virago kurudi jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo la kwanza la nusu fainali lililochezwa jioni kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani humu, Simba itabidi ijilaumu kwa kutemeshwa taji.
Na kama kuna mtu ambaye atajuta kwa kung'oka kwa Simba ni kipa Peter Manyika aliyeizawadia Mtibwa bao baada ya kushindwa kudaka mpira uliiopigwa na Shiza Kichuya na kumfanya Jeba kumpoka na kufunga bao hilo.

Mtibwa sasa inasubiri kujua itacheza na nani kati ya Yanga na URA ambazo zinaendelea kuumana muda huu.
Hizo ni fainali za tano kwa Mtibwa tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2007 ikikutana na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka huo na kufungwa.
Pia hii itakuwa fainali ya pili mfululizo ya Mtibwa baada ya mwaka jana kucheza fainali dhidi ya Simba na kufungwa kwa mikwaju ya penalti.
Pamoja na Simba kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa na hasa katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko, lakini umakini mdogo wa washambuliaji wa Msimbazi wakiongozwa na Danny Lyanga, Mussa Mgosi na Ibrahim Ajib.