STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 10, 2016

Spurs chupuchupu, Chelsea yapeta Kombe la FA

Harry Kane akishangilia penalti yake iliyoiokoa Spurs kulala nyumbani
WAKATI Chelsea ikivuka hadi raundi ya nne baada ya kuifunga timu ya Scunthorpe kwa mabao 2-0 katika mechi ya mfululizo wa michuano ya Kombe la FA, Tottenham hotspur ikiwa nyumbani ilinusurika kulala baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Penalti ya Harry Kane katika dakika za lala salama iliiokoa Spurs kulala kwa Leichester City, huku Swansea City iking'olewa na Oxford United kwa mabao 3-2.
Chelsea wenyewe wakiwa nyumbani kwao Stamford Bridge ilipata ushindi wa mabao 2-0 na kuungana na vigogo wengine wa Ligi Kuu kufuzu raundi nyingine ya michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Arsenal iliifumua Sunderland jana Jumamosi kwa mabao 3-1.No comments:

Post a Comment