STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Sanchez aibeba Arsenal, Napoli hoi Ulaya

Alexis Sanchez
Cazorla akishangilia nao la sanchez. Yeye alikosa penati usiku huu
Alexis Sanchez
Sanchez akishangilia bao lake
Jack Wilshere
Welshere akisikitika baada ya kukosa bao
Nenda nje bwana we si uonyeki mara moja'

Alexis Sanchez
Sanchez akifunga bao la Arsenal
Mathieu Debuchy
Mathieu Debuchy akisikitika baada ya kulimwa kadi ya pili ya njano iliyoambana na nyekudnu na kutolewa uwanjani usiku huu.
Alexis Sanchez pays off his transfer fee in one swoop.
Oyooooooooooooo!
STRIKA mpya wa Arsenal kutoka Chile, Alexis Sanchez  usiku huu ameibuka shujaa baada ya kuivusha timu yake hiyo kwenye hatua ya makundi kwa mwaka wa 17 mfululizo baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Besiktas ya Uturuki.
Katika mchezo huo Arsenal ilijikuta wakicheza pungufu baada ya Methieu Debuchy kulimwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano, moja kila kipindi katika pambano hilo lililochezwa uwanja wa Emirates, mjini London.
Sanchez aliyesajiliw ana Arsenal hivi karibuni akitokea Barcelona alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 45 za kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri ya Jack Wilshere na kuifanya Ze Gunnerz kufuzu kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0.
Katika mechi ya kwanza baina ya timu hiyo wiki iliyopita zilishindwa kutambiana kwa kutofungana mjini Instabul.
Katika mechi nyingine za Ligi hiyo ya mabingwa Ulaya,  Malmo ya Sweden iliitambia Salzburg ya Uswisi kwa kuichapa mabao 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-2 kwani katika mechi ya kwanza Malmo walifungwa mabao 2-1 ugenini.
Bayer Leverkusen wakiwa nyumbani nchini Ujerumani walipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya  Copenhagen na kufuzu kwa mabao 7-2 kwani mechi ya awali walishinda ugenini mabao 3-2, huku Athletico Bilbao ikiizima napoli kwa mabao 3-1 baada ya wiki iliyopita kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.

Diamond azidi kutusua kimataifa, Mdogomdogo wambeba

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasib Abdul 'Diamond' amezidi kuangukiwa na neema ibaada ya kuteuliwa kuwania tuzo za muziki za kimataifa za IRAWMA kupitia wimbo wake mpya wa Mdogo Mdogo.
Nyimbo nyingine zilizopo katika kinyang'anyiro hicho katika category ya 'Best African Song/Entertainer' ni pamoja na Aye wa Davido toka Nigeria, Bundeke wa Awilo Longomba toka Congo, Tam Tam wa Willy Paul Msafi toka Kenya, Sitya Loss wa Eddy Kenzo toka Uganda na Mama Africa wa Brakets toka Nigeria
Hii ni mara ya nne kwa Diamond kupenya kwenye tuzo za kimataifa baada ya mwaka huu kuteuliwa kuwania tuzo za MTV za Afrika Kusini, BET za Marekani na AFRIMMA ambapo ndipo pekee alipoibuka kidedea.
Kuteuliwa kuwania tuzo hizo za sasa zinazidi kumpa nafasi msanii huyo kuzidi kutamba anga la kimataifa.

Sijadungwa Mimba na Mchungaji Gwajima-Flora Mbasha




NYOTA wa muziki wa Injili nchini, ambaye pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima,


Flora Mbasha akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV, amefunguka na kusema kuwa hata mimba aliyonayo siyo ya mchungaji Gwajima kama inavyopakaziwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Flora amesema hayo leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa Sita kamili.
Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo
Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi.

"Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji
Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? " Alisema Flora, wakati akijibu ya maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumeo kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti.

Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao.
Muimbaji huyo amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.
"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo wa
baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. 

"Hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili"
 

HAJAACHANA NA MBASHA KWA AJILI YA GWAJIMA
Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote hajaachana na Mbasha sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu zaidi.

Ila amekuwa na matatizo katika ndoa yake kati yake na mumewe na ni matatizo yao ya ndani ambayo asingependa kuyaweka wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia heshima mumewe, maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe asingependa kuwa wazi sababu wanamtoto mkubwa sasa.
"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"
Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambae ni Emmanuel Mbasha maana ameishi nae katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe na kwenda kwenye michepuko hivyo huo ujauzito ni wa Mume wake Emmanuel Mbasha na siyo Gwajima.

Balotelli aandaliwa kuiua Spurs Jumapili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiaVQQWvCjgmGQoV60H_iQem7DH3sMHClKoS-HrMHiFyPnB5CMmYLIOJJXsYdpV2cLgqx3InxajvilHnHSm7LuExKxBqGyR5yVYYrNIRz2jg_5LTLapESn3zHuiCXdGWTTlVQ7dpsCwwva0/s1600/1409137512960_wps_12_Mario_Balotelli_joins_the.jpg
Balotelli akiwa na wachezaji wenzake wakifanya mazoezi
KOCHA Brendan Rodgers wa Liverpool ameweka bayana kwamba anatarajia kumtumia Mario Balotelli, mshambuliaji wake mpya waliyemsajili akitokea AC Milan kwa mechi yao ya Jumapili dhidi ya Tottenham Hotspur.
Nyota huyo wa Italia alijiunga na vijogoo hao wa Merseyside na kuishuhudia Liverpool ikikanyagwa mabao 3-1 na Manchester City walipoifuata Etihad, uwanja aliokuwa akiiutumia strika huyo miezi sita iliyopita.
Rodgers, aliuambia mtandao kwamba anamuandaa nyota huyo mwenye vituko ambaye tayari ameanza kuyazoea mazingira ya Anfield kwa kufanya mazoezi na wenzake ili kuwakabili vinara hao wa ligi, Spurs kwenye uwanja wa ugenini wa White Hartlane.
"Nadhani wikiendi hii atakuwa tayari kuanza kuitumia timu," kocha Rodgers alisema.
Vijogoo hao walioanza ligi kwa kishindo kwa kuifunga Southampton kwa mabao 2-1 na kushtukizwa na mabingwa watetezi kwa kulazwa mabao 3-1 huku Balotelli akishuhudia jukwaani.

Crystal Palace yamrejesha Neil Warnock klabuni


http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2010/01/04/article-1240631-07C239A3000005DC-843_306x423.jpg
Kocha Warnock aliyerejea tena Crystal Palace
KLABU ya Crystal Palace imemrejesha kikosini aliyekuwa meneja wake, Neil Warnock.
Kocha huyo alitimka katika klabu hiyo 2010 kwenda kuiongoza QPR na kuipandisha Ligi Kuu kabla ya kutimuliwa mwaka 2012 amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo ambayo ilikuwa ikifundishwa na Keith Millen.
"Neil amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuongoza timu katika pambano la Jumamosi dhidi ya Newcastle United," Mtandao wa klabu hiyo (www.cpfc.co.uk) uliandika leo Jumatano.

Huu ndio ujio mpya wa Benjamini wa Mambo Jambo

MWANAMUZIKI Benjamin wa Mambo Jambo ameamua kuvunja ukimya akijiandaa kurudi kwa kishindo na ngoma mpya inayofahamika kama Kata K. Mwanamuziki huyo amebainisha kuwa alikuwa masomoni kiasi cha kushindwa kuwashushia mashabiki wake burudani zilizozoeleka, ila kwa sasa amewataka mashabiki hao kaeni mkao wa kula kwani amerejea kimoja katika 'game'.

Manchester United yahaha kusaka saini ya Arturo Vidal

http://www.bettingadda.com/wp-content/uploads/2014/07/Arturo-Vidal-Juventus.jpgKIPIGO cha aibu cha mabao 4-0 toka kwa timu ya daraja la kwanza ya MK Dons waliowang'oa kwenye Kombe la Ligi kimemzindua Kocha wa Manchester United, Luis Van Gaal ambaye amehamishia nguvu zake kumnasa kiungo wa Juventus, Arturo Vidal.
Van Gaal na Afisa mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward wanahaha kusaka saini ya Vidal baada ya kumaliza kusajili Angel Di Maria jana. 
United imekuwa ikipinga kumhitaji Vidal kwa kipindi kirefu lakini sasa wanadaiwa kuanza mazungumzo kama wanayofanya dhidi ya Ajax Amsterdam kwa ajili ya kumsajili Daley Blind. 
Majeruhi pekee ndiyo yalioonekana kumzuia Van Gaal kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile ambaye ana thamani ya paundi milioni 30 lakini kutokana na matokeo mabovu ya hivi karibuni klabu imeona hakuna jinsi bali kutumia fedha ili wajiimarishe. 
Upasuaji wa goti msimu uliopita ulimzuia Vidal kuitumikia Juventus toka mwishoni mwa Machi mwaka huu ingawa baadae alipona na kupata muda wa kuwepo katika kikosi cha Chile katika michuano ya Kombe la Dunia. 
Ujio wa Vidal, 27 United kutasaidia kuimarisha safu ya kiungo ambayo imeonekana kuyumba na kupelekea kipigo cha mabao 4-0 jana dhidi ya timu ya daraja la chini ya MK Dons katika mchezo wa Kombe la Ligi. 
Kama United wakifanikiwa kumsajili Vidal watakuwa wamefikisha kiasi cha paundi milioni 150 walizotumia msimu huu kwa ajili ya usajili baada ya kuvunja rekodi nchini Uingereza kwa uhamisho wa Di Maria.

Morocco yaikwepa Stars, sasa kukipiga na Burundi

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2013/07/173420877-1811087.jpg
Morocco iliyoichomolea Stars
MOROCCO imechomoa kucheza na Tanzania katika kalenda ya FIFA na sasa Taifa Stars itacheza na Burundi Septemba 5, mwaka huu mjini Bujumbura.
Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa amesema Morocco imejitoa kwa sababu imesema haitaweza kuwapata wachezaji wake wa kimataifa.
Mwesigwa amesema sasa Taifa Stars itacheza na Burundi mjini Bujumbura siku hiyo hiyo. Burundi iliitoa nishai Stars siku ya Uhuru kwa kuilaza mabao 3-0.

Kocha Mholanzi, Mart Nooij, tayari ameita kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo huo.

Hao ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio (ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Ebola waitisha Congo, yagoma kwenda Nigeria

http://english.umuseke.rw/wp-content/uploads/2013/08/Congo_soccer_team-300.jpgNCHI ya Congo imetangaza kugoma kwenda Nigeria kucheza pambano lao la kuwania kufuzu Fainali za Afrika za 2015 kwa ilichodai inahofia tisho la ugonjwa wa Ebola.
Hata hivyo Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limedai kuwa halijapata taarifa yoyote rasmi kutoka Shirikisho la Soka la Afrika-CAF juu ya madai ya Congo Brazzaville kuelekea katika mchezo huo uliopangwa kuchezwa huko Calabar. 
Congo ambao watakuwa wageni wa Nigeria katika mchezo huo utakaochezwa Septemba 6 mwaka huu wametuma malalamiko CAF kueleza wasiwasi wao juu usalama katika mchezo huo. 
Congo wamesisitiza hawatakwenda katika mji wa Calabar au mwingine wowote nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo huo kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ugonjwa huo usiokuwa na tibaumeripotiwa kuua zaidi za watu 1427 katika miji ya nchi za Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria, huku wengine  zaidi ya 2,615 wakiambukizwa toka ugonjwa huo ulipolipuka Machi mwaka huu. 
Kocha wa timu ya taifa ya Congo, Claude Leroy amesema itakuwa ngumu na hatari kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo na kudai kuwa hata majirani zao Cameroon tayari wamefunga mipaka yao ili kuepusha maambukizi zaidi. 
Hata hivyo NFF wamesisitiza kuwa mchezo utafanyika kama ulivyopangwa katika Uwanja wa UJ Esuene uliopo mji wa Calabar.

Chegge atambia video ya Wauwe

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Said Chegge 'Chegge Chigunda' ametamba video yao mpya ya wimbo 'Wauwe' ni funika bovu na anaamini itasumbua katika vituo vya runinga ndani na nje ya nchi.
Chegge aliyeshirikiana na Mheshimiwa Temba kutoa wimbo na video hiyo aliiambia MICHARAZO kuwa, ukali wa video hiyo unathibitisha Watanzania wanavyoweza kutengeneza kazi kinyume na wanaokimbilia nje ya nchi.
"Hatujisifu, lakini video ya 'Wauwe'  imetulia na ni bonge la kazi ambayo inathibitisha kuwa wapo Watanzania wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha video tofauti na tazamo wa baadhi ya wasanii kukimbilia nje," alisema.
Chegge alisema kazi kubwa iliyofanywa na Adam Juma wa Next Level itazidi kuliweka kundi lao la TMK Wanaume Family matawi ya juu.
Wimbo huo Chegge na Mhe Temba wameshirikiana na mkali wa Moto Band aliyeibuliwa na kituo cha Mkubwa na Wanae, Maromboso na video yake imewajumuisha nyota mbalimbali akiwamo Jokate na Julio wa Big Brother

Tanzania Kwanza yaishutumu UKAWA kwa kiburi

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2014/04/Mwenyekiti-wa-Kamati-ya-Tanzania-Kwanza-ya-Nje-ya-Bunge-la-Katiba-Agustino-Matefu-alionesha-waraka-wa-Tundulisu-ambao-aliikataa-Zanzibar-kushoto-ni-Iddi-Majuto-Katibu-wa-Kamati-hiyo.jpg
Augostino Matefu (kulia)
http://udakuleo.com/wp-content/uploads/2014/04/3b83d__ukawa.jpg
Viongozi wakuu wa UKAWA wanaoshutumiwa na Tanzania Kwanza
NA SULEIMAN MSUYAWAKATI Wabunge wajumbe wa Bunge la Katiba Wanaounga Mkono Rasimu iliyotolewa na iliyokuwa Tume ya Rasimu ya Katiba wakijulikana kwa jina maarufu la (UKAWA) wakiendelea na msimamo wao wa kutorejea Bungeni Kamati ya Tanzania Kwanza imewashutumu kuwa kiburi chao kinasababishwa na wafadhili kutoka Ujerumani na Uholanzi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Augustino Matefu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema takribani wiki moja iliyopita alipozungumza na wanahabari alitoa siku saba za UKAWA kurejea Bungeni na kinyume cha hivyo ataweka wazi juu ya nini kinawapa kiburi wabunge hao.
Matefu alisema  vyama vya CDU na Consecutive  kupitia benki moja kubwa ya nchini Ujerumani na taasisi inayojulikana kwa jina la (KAS) wamekuwa wakiwapatia viongozi wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) fedha haramu zaidi ya bilioni 4.6 kwa lengo la kugomea bunge la katiba linaloendelea mkoani Dodoma.
“UKAWA wanapokea fedha kutoka Ujerumani ndio maana wanakataa kuingia bungeni na kama kuna mtu anabisha aende mahakamani na sisi tunaonyesha ushahidi kwani fedha hizo zimeingia katika akaunti ya Freeman Mbowe na Dk. Wilbrod  Slaa na ipo taasisi hapa nchini ndio inapokea”, alisema
Alisema vyama hivyo vya siasa vinavyosaidia UKAWA kupitia viongozi wakuu wa CHADEMA vina lengo la kuvunja amani ya nchi jambo ambalo Tanzania Kwanza hawawezi kulivumilia.
Mwenyekiti huyo alisema UKAWA kupitia akaunti ya Mbowe na Slaa mnamo tarehe 4 hadi 15 mwezi Machi waliingiziwa shilingi bilioni 1.7, mwezi Machi huo tarehe 26 mwaka huu UKAWA walipokea shilingi milioni 380 kupitia akaunti ya Mbowe.
Matefu alisema hivi majuzi Mbowe amepokea shilingi milioni 580 kwa lengo la kufadhili maandamano ambayo kwa mujibu wa Matefu yataweka nchi hatarini ambapo aliomba Watanzania kutounga mkono.
Aidha alisema hivi karibuni vyama hivyo vya Ujerumani vimeahidi kuingizia vyama vya umoja wa UKAWA shilingi bilioni 4.6 hiyo ikiwa ni baada CHADEMA kuonyesha msimamo wa kutoridhia maridhioano na chama tawala CCM kwa kile anachodai Matefu kuwa CCM itaongoza milele.
Mwisho.

Wajasiriamali 200 wapewa mafunzo Kanda ya Ziwa

http://danalbrecht.com/wp-content/uploads/2010/04/rocks.jpgNA SULEIMAN MSUYA
ZAIDI ya Wajasiriamali 200 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wameshiriki mafunzo ya jinsi ya kuandaa bidhaa kabla ya kuingia sokoni yaliyoandaliwa na kampuni ya Usalama Chakula na Ubora (Food Safety and Quality Consultancy Co. Limited) jijini Mwanza.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Petronella Mlowe wakati akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu akiwa mkoani Mwanza.
Mlowe alisema katika mafunzo hayo yaliyofanyika jana na leo jijini Mwanza yamepata mafanikio makubwa kwa kuwepo kwa mwitikio kwa wajasiriamali wakiume zaidi ya wanawake.
Alisema pamoja na mwitikio mkubwa kutoka kwa wajasiriamali amebaini kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa wahusika wa mafunzo hayo hasa kwenye maandalizi ya bidhaa jambo ambalo amesema kuwa ni muhimu serikali ikatumia vyombo vyake kuwajengea uwezo wajasiriamali.
“Mafunzo yamekuwa ya mafanikio makubwa sana hasa kwa wanaume wengi wamejitokeza jambo ambalo limenipa matumaini ya kuendelea na kampeni hii ambayo ina lengo la kukuza uchumi wa wa wajasiriamali wa Kitanzania”, alisema.
Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yalishirikisha wajasiriamali kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Bukoba na Geita ambapo waliomba kampuni hiyo kuendelea na mpango huo ili kuhakikisha kuwa wanapata mafanikio.
Alisema wajasiriliamali wengi ni wale ambao wanajihusisha na uuzaji wa asali, maembe, chili, pilipili na bidhaa nyingine mbalimbali ambazo zimekuwa zikiuzwa katika soko la ndani ila la nje hazipatikani.
Pia alitoa wito kwa asasi, taasisi na mashirika mengine ambayo yanajihusisha na kuelimisha kutoa elimu ya jinsi ya kuandaa bidhaa hasa katika kuweka lebo ili kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa unapatikana ili kuleta ushindani wa ndani na nje ya nchi.
Mlowe alisema kampuni yao itaendelea kushirikiana na wajasiriamali ambapo zoezi hilo linaendelea katika mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 hadi 29 mwezi huu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanapata uelewa mzuri juu ya uandaji wa bidhaa.

Eto'o hatimaye aangukia miaka miwili Everton

Samuel Eto'o akisaini mkataba wa kuichezea Everton

Samuel Oto'o
MSHAMBULIAJI nyota wa nchi ya Cameroon aliyekuwa akiichezea Chelsea kabla ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja hivi karibuni, Samue Eto'o amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili wa kukipiga Everton.
Awali Eto'o alikuwa akitajwa kunyemelewa na Liverpool lakini ujio wa Muitalia Mario Balotelli ulimfanya nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Inter Milan kutua kwa Ze Toffies.

Zitto Kabwe ajitosa 'bifu' la Diamond, Ali Kiba

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/Zitto-Queen-Darlin-Mwasiti-na-wengine.jpg
Zitto Kabwe kati kati na wasanii wa Leka Dutigite
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGj0GmR29OLVja_Ne6iqPPepXro0cl0KYsdtlk0FnXs6HVn77yq9d3I-IkfJuMIB_yYqsh__7Nqd03BCZ773OICts1TrjLHk2mjAm4GaZROS6hm6eaePjgcm5SF_3H52QfaMCsRsld1LCD/s1600/Ali+K+na+Diamond.jpg
Ali Kiba na Diamond ambao wanadaiwa hawaivi, japo Kiba amekanusha taarifa hizo akidai hana 'bifu' na Diamond
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejitosa kusuluhisha ugomvi wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziku wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba na Nasibu Abdul 'Diamond'.
Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV baada ya kuulizwa kuwa ni jitihada gani amezifanya kusuluhisha ugomvi wa wasanii hao akiwa kama mlezi wa wasanii wanaotoka mkoani Kigoma.
Alisema anafahamu kuwapo kwa ugomvi wa kutoelewana kati ya wasanii Ali Kiba na Diamond na kwamba alishawahi kufanya jitihada za kuwaita kila mmoja kwa nyakati tofauti.
Alifafanua kuwa katika kuhakikisha anawasuluhisha wasanii hao, anaifanya kazi hiyo kwa umakini kwa sababu hataki kuonekana anaingilia maisha ya watu na kwamba ana imani atafanikiwa kuwapatanisha.
Kuhusu madai kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Mwasiti Almas, alisema ni kweli kumekuwapo na uvumi huo lakini kimsingi hana uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii huyo.
"Nasikitishwa na madai hayo yanayotolewa na baadhi ya watu, Mwasiti ni kama dada yangu ambaye nimekuwa nikimsaidia katika kazi zake, kuhusishwa naye kimapenzi ni jambo linalonisononesha,"alisema.
Zitto alisema wanaomhusisha katika suala la mapenzi na msanii huyo ni kwa sababu Mwasiti ameimba wimbo ambao amemtaja yeye (Zitto) lakini kiukweli hana uhusiani naye wa kimapenzi.
Alipoulizwa ni lini ataoa, alisema bado 'yupo yupo' na kwamba kuna mwanamke aliyemtaja kwa jina la Jack ambaye amezaa naye mtoto ambaye kwa sasa miaka nane na anasoma darasa la pili nchini Uganda.
Zitto alizungumzia pia kampuni ya Leka Dutigite inayounganisha wasanii wa Kigoma All Stars, na kusea kuwa ni kampuni ambayo kila msanii anayetoka mkoani Kigoma ana hisa na ikipata faida wanagawana.
Zitto alisema Leka Dutigite pia inamiliki kampuni nyingine ambayo imekuwa ikipata kazi mfano katika Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na yeye kama mlezi amekuwa akitoa fedha zake kusaidia.

Hatimaye Di Maria rasmi Man Utd




HATIMAYE Muargentina, Angel Di Maria ametua na kusaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Manchester United.
Mkataba huo ndiyo rekodi mpya ya usajili baada ya Man United kukubali kutoa pauni milioni 59.7 ambazo ni pauni milioni 60 ili kumpata.
Atakuwa akilamba mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki, anachukua nafasi ya pili kwa mshahara mkubwa baada ya nahodha wake, Wayne Rooney.
Mchezaji huyo hata hivyo aliingia Old Trafford na mguu mbaya baada ya klabu yake hiyo kulambwa mabao 4-0 na timu ya Daraja la Kwanza katika mechi ya Kombe la Ligi na anategemea kuwemo katika kikosi cha Mashetani hao Wekundu katika mechi ya Ligi Kuu siku ya Jumamosi dhidiya Banley.

Giroud awapa presha Arsenal

HUENDA Olivier Giroud akakaa nje ya dimba kwa miezi mitatu ijayo baada ya vipimo kuonyesha kuwa amevunjika mfupa katika unyayo wakati wa mechi dhidi ya Everton Jumapili kwenye Uwanja wa Goodison Park, kwa mujibu taarifa kutoka Ufaransa.
Jarida la Ufaransa la L'Equipe limeripoti matokeo hayo ya majeraha ya Giroud yamezua hofu kwa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na kwamba sasa atalazimika kurudi sokoni kwa kasi kununua mshambuliaji.
Wenger alikuwa amesisitiza kwamba hana mpango wa kusajili mshambuliaji katika dirisha hili la usajili wa majira ya joto, akiamini kuwa usajili mpya wa Alexis Sanchez, huku hivi karibuni Theo Walcott akitarajiwa kurejea pamoja na uwapo wa Yaya Sanogo kungemwezesha kuwa na safu bora ya ushambuliaji.
Hata hivyo, kitendo cha Giroud kutokea benchi katika Uwanja wa Goodison Park Jumamosi na kusawazisha kulimpa matumaini kocha huyo, hatua iliyomfanya kumtabiria kuwa atamaliza Ligi Kuu England akiwa na mabao 25.
Kama taarifa hizo zitathibitishwa, mipango yake hiyo itafanyiwa mabadiliko, wakati huu ambao chumba cha majeruhi cha  Arsenal kikianza kusheheni wagonjwa ndani ya wiki mbili hizi za mwanzo wa msimu mpya.
Kuwa majeruhi kwa Giroud, kutamlazimisha Wenger kusaka huduma ya mshambuliaji wa Queens Park Rangers, Loic Remy, licha ya mapema majira haya ya joto kutupilia mbali uwezekano wa kumsajili Mfaransa huyo.

Arsenal katika mtihani mzito leo Ulaya

WAKATI kiungo wake mahiri, Jack Wilshere akiamini kuwa sare ya 2-2 waliyopata na Everton mwishoni mwa wiki itawasaidia kuwapoa morali wa kufanya vyema katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal ina mtihani mgumu leo.
Klabu hiyo ya meneja Arsene Wenger inaikaribisha Besiktas ya Uturuki katika mechi ya marudiano ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ze Gunnerz wakihitaji ushindi ili kuingia kwenye makundi.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza timu hizo zilipokutana mjini Instabul, zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila magoli, huku Arsenal ikimpoteza nyota wake kwa kupewa kadi mbili za njano na kufuatia nyekundu.
Walshere anaamini Arsenal wapo poa baada ya kufanikiwa kutoka nyuma kwa kufungwa mabao 2-0 na kufanikiwa kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita. 
Akihojiwa Wilshere amesema alama waliyopata dhidi ya everton ilikuwa ni muhimu kwani inawapa nguvu kwa ajili ya mchezo wao wa leo ambapo sare ya aina yoyote inaweza kuwaondoa mashindano ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mingi kwa vijana hao wa Emirates.

Kocha amuonya Balotelli, amwambie akiharibu inakula kwake

http://assets2.sportsnet.ca/wp-content/uploads/2013/05/balotelli_mario640.jpgMARIO Balotelli yuko katika "nafasi yake ya mwisho" baada ya kujiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 16, alisema kocha Brendan Rodgers.
Mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 24 aliishuhudia kutokea jukwaani Liverpool ililala 3-1 ugenini dhidi ya klabu yake ta zamani ya Manchester City juzi baada ya kujiunga akitokea AC Milan kwa mkataba wa miaka mitatu.
Balotelli alikuwa maarufu kwa matukio ya utata wakati akichezea Man City lakini Rodgers anakubali kuwa kumsajili nyota ni "kama kucheza kamari" lakini anasema anaweza kujirekebisha.
"Tunaweza kumfanya awe bora kama mchezaji na ajutambue kama mtu mzima," alisema.
"Ni kijana mzuri. Alikuwa mwerevu sana. Anatambua mahala alipo ni wapi, katika wakati wake huu, na anatambua kwamba pengine hii ni fursa yake ya mwisho.
"Muda utaongea. Hakika ni kama kamari. Sitasema kwamba hafiti, ila anatambua anapaswa kufiti katika utamaduni wetu."

Mbunge Viti Maalum ataka viti maalum vifutwe Katiba Mpya

Ritta Kabati alipokuwa kitoa mtazamo wake kuhusu viti maalumu vya ubunge


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) amesema moja ya mambo anayounga mkono katika mchakato wa Katiba Mpya ni kufutwa kwa viti maalumu vya ubunge.
Akizungumza hivi karibuni nje ya jengo la CCM Mkoa wa Iringa, Kabati alisema Viti Maalumu vina faida zake katika mchakato wa maendeleo lakini vinawadhalilisha sana wanawake.
“Siku hizi wabunge wanawake wa viti maalumu tunaitwa wabunge wa vitanda maalumu, huu ni udhalilishaji kwa sababu wengi wanahisi upatikanaji wake una mahusiano yasiofaa,” alisema.
Alisema utaratibu unaotumiwa na nchi kama Uganda na Rwanda kupata wawakilishi wanawake katika mabunge yao ndio unaopaswa kutumiwa na Tanzania na kama ikishindikana basi wanawake nao wapewe nafasi sawa na wanaume ya kugombea moja kwa moja kwenye majimbo ya Uchaguzi.
“Tumetembelea Uganda na Rwanda, kule hawaiti viti maalumu vya wanawake, wanaita viti vya wilaya vinavyoshindanisha wanawake wa vyama mbalimbali katika wilaya hizo,” alisema.
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, Kabati alisema endapo viti maalumu vitafutwa ataamua wapi atupe karata yake kati ya jimbo la Iringa Mjini au Kilolo.

“Kilolo ni kwetu na Iringa Mjini ni kwetu, kwahiyo kama Katiba Mpya itaondoa viti maalumu basi nitaamua wapi niende kati ya majimbo hayo,” alisema.

Mkubwa na Wanae kutambulisha chipukizi wapya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6Kc_Ur8Lec9lYrBOF-IQAUaRSFQDK8Cdxz_8hhYUt4XGOWTORG7E7OH7FEYP_r6op9UjS_24xidUE0xrJVx_XNzUQTPr_8iyprsuw_DKzExTICOG6MOUOobngot5tCcegYMZg5V4AfR0/s1600/ya+moto+band.jpg
Said Fella akiwa nna wasanii wa Moto Band ambayo ni chimbuko lililoibuliwa na kito cha Mkubwa na Wanae
KITUO cha kukuzia na kuendeleza vipaji vya wasanii cha Mkubwa na Wanae kinatarajiwa kuwatambulisha rasmi wasanii chipukizi pamoja na nyimbo zao mpya siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam.
Onyesho hilo litafanyika kwenye ukumbi wa Maisha Club na wasanii hao watasindikizwa na 'kaka' zao wa TMK Wanaume Family na Moto Band.
Akizungumza na MICHARAZO mmoja wa wakurugenzi wa kituo hicho, Said Fella 'Mkubwa Fella' alisema wasanii watakaotambulishwa katika onyesho hilo la Agosti 31 ni Dogo Muu, Getu, Dulla Yeyo, Mugogo na chipukizi wengine ambao wamekamilisha nyimbo zao mpya hivi karibuni chini ya kituo hicho.
"Tunatarajia kuwatambulisha rasmi wasanii wetu wapya ambao wamekamilisha nyimbo mpya. Onyesho hilo litafanyika Agosti 31 Masaki," alisema Fella.

Manchester Utd majanga matupu, yanyukwa 4-0

Finish: Arsenal loanee Benik Afoba (left) losts home under pressure from Keane for 3-0 with 20 minutes remaining in the game
Efoba akiwatungua Mashetani Wekundu bao la tatu
Unbelievable: United players stand shocked after MK Dons scored to make it 2-0, but worse was to come for Louis van Gaal's menJINAMIZI baya limeendelea kuiandama Manchester United baada ya usiku wa kuamkia leo kubamizwa mabao 4-0 na timu ya MK Dons.
Pambano hilo lililokuwa la michuano ya Kombe la Ligi (Capital One) limemuacha katika sintofahamu Kocha
Louis van Gaal ambaye ni kipigo cha pili kwa vijana wake tangu msimu mpya wa soka England uanze.
Mashetani Wekundu hao walikumbana na kipigo hicho kutokana na magoli ya Will Grigg dakika ya 25 na 63 na Benik Afobe anayecheza kwa mkopo MK Dons akitokea Arsenal aliyefunga pia mawili dakika ya 70 na 83.
Kipigo hicho kilimuacha kocha msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs kutokwa na machozi, huku LVG akishindwa kuamini kama timu ya 'mchangani' imewanyoa.

Serikali kufuta ada za shule hadi 'O Level'

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrXO0r3kx_dcsso6MygK29qiL6SqNgulI6NYBe6WNU4JSxVorninEgC8Jb5DESiJR9honvccMTJLLnYzpag6L0krQJgEKmhXaqk7S8R4a-XBtNL4hqkrcXjLcy4Qjk8K0vJ3sUEvwzdlHJ/s400/GO9G4311.JPG
Rais Kikwete akisamiliana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari.
SERIKALI inajipanga kufuta ada za sekondari, ili elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne, itolewe bure. 
Rais Jakaya Kikwete, alisema hayo juzi katika mkutano wake na wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, na wakazi wa vijiji vya jirani na chuo hicho, katika ziara yake inayoendelea katika Mkoa wa Morogoro iliyoanza Agosti 20.
“Sasa hivi tunaangalia jinsi ya kufuta karo katika shule zetu zote za sekondari za Serikali, ili kuhakikisha kila mtoto anayeanza darasa la kwanza, awe na nafasi ya kumaliza sekondari kwa maana ya kidato cha nne, bila kulazimika kuacha shule kwa sababu ya ada.
“Tunaangalia kuondoa ada hii, ambayo wazazi wanalipa Sh 20,000 kwa shule za kutwa na Sh 70,000 kwa shule za bweni, ili watoto wetu waingie darasa la kwanza, na kwenda moja kwa moja hadi kidato cha nne bila wasiwasi wa kukwamishwa na ada,” alisema Rais Kikwete.
Kwa hatua hiyo, Rais Kikwete alisema mbali na kulenga kuinua elimu, pia itawapunguzia mzigo wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika shule hizo za sekondari za Serikali.
Alisema zipo sababu za msingi zinazokwamisha wanafunzi wengi wa shule za sekondari, kuendelea na masomo yao kutokana na wazazi wao kushindwa kulipia karo ya shule, kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za umasikini.
Rais Kikwete alisema pamoja na kejeli nyingi zilizoelekezwa kwa shule za sekondari za kata, kiasi cha kuitwa Yeboyebo katika miaka ya mwanzoni ya shule hizo, bado zimekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mafanikio ya Sekta ya Elimu katika miaka karibu tisa ya uongozi wake.
Akielezea historia ya kuanzishwa kwa shule za sekondari za kata, Rais Kikwete alisema wakati alipokuwa akiingia madarakani, hali ya watoto kuingia sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa mbaya.Kwa mujibu wa Rais Kikwete, hali hiyo ilisababisha asilimia kati ya sita na kumi tu ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba, kusonga mbele kwa sababu shule za sekondari zilikuwa chache.
“Kwa miaka mingi, hatukujenga shule mpya za sekondari na kama mnavyojua, Wakoloni wa Kiingereza ndio kabisa hawakujenga shule. Kazi hiyo waliwaachia Wamisionari. Kwa hiyo wakati tunaingia madarakani, hali ilikuwa mbaya ndiyo maana tukaja na Sera ya Shule za Kata,” alisema Rais Kikwete.
Alisema takwimu rasmi zinaonesha kwamba, kulikuwa na  shule za sekondari 1,745 mwaka 2005, zikiwemo shule 1,202 za Serikali na sasa ziko shule za sekondari 4,576, zikiwemo shule 3,528 za Serikali.
Mafanikio hayo ya kupanuka kwa sekta ya elimu, kwa mujibu wa Rais Kikwete, yalileta changamoto hasa ya ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi. Alisema Serikali imepambana na changamoto hiyo na zingine zilizojitokeza, ambapo sasa wapo walimu karibu wa kutosha wa masomo hayo kwa shule za sekondari zote nchini.
Mbali na kusudio la kufuta ada, Rais pia alisema Serikali  inaandaa utaratibu maalumu utakaowezesha kujenga mabweni katika  shule za msingi na sekondari zilizopo maeneo ya jamii ya wafugaji.
Alisema lengo ni kuwawezesha watoto wa jamii hiyo, waendelee kusoma hata pale wazazi na walezi wao wanapohama kutoka eneo moja kwenda jingine  kufuata malisho ya mifugo yao.
“Tuna tatizo kubwa katika eneo hili...watoto wengi wa wafugaji wanakatishwa masomo kutokana na wazazi ama walezi kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine kufuata malisho...wanaohama wanaondoka na watoto wao wote na kuwakosesha fursa ya kusoma,” alisema Rais.
Kuhusu elimu ya juu, Rais Kikwete alisema  kwa sasa kuna vyuo vikuu 51, vikiwemo 15 vya umma na pia kuna ongezeko la fedha za mikopo ya elimu kutoka Sh bilioni 16 mwaka 2005 na kufikia Sh bilioni 345 kwa sasa.
Mbali na ongezeko la fedha za mikopo ya elimu ya juu, Rais Kikwete alisema wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu waliongezeka kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000 kwa sasa.
Awali Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa, alipongeza Serikali kwa kukuza mitaala ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kushauri kuwa ili wanafunzi washindane katika soko la ajira, upo umihimu wa mitaala  kuendelea kuboreshwa.
Alimwomba Rais Kikwete kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ya chuo hicho kutokana na uchakavu wa majengo yake.
Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, Boniface Maiga, alitaja changamoto kubwa zinazowakabili  kuwa ni pamoja na uhaba wa sehemu za malazi uliosababishwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaodahiliwa  na uchakavu wa miundombinu.
Alisema licha ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB),  kutoa mikopo hiyo kwa wakati, bado kuna malalamiko mengi kuhusu watoto wa matajiri na wenye uwezo, ambao wameendelea kupewa mikopo.
Aliiomba serikali kufanyia utafiti suala hilo na ikibaini hali hiyo, fedha hizo zitolewe kwa watoto wengi masikini.