
Hata hivyo Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limedai kuwa halijapata taarifa yoyote rasmi kutoka Shirikisho la Soka la Afrika-CAF juu ya madai ya Congo Brazzaville kuelekea katika mchezo huo uliopangwa kuchezwa huko Calabar.
Congo ambao watakuwa wageni wa Nigeria katika mchezo huo utakaochezwa Septemba 6 mwaka huu wametuma malalamiko CAF kueleza wasiwasi wao juu usalama katika mchezo huo.
Congo wamesisitiza hawatakwenda katika mji wa Calabar au mwingine wowote nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo huo kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ugonjwa huo usiokuwa na tibaumeripotiwa kuua zaidi za watu 1427 katika miji ya nchi za Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria, huku wengine zaidi ya 2,615 wakiambukizwa toka ugonjwa huo ulipolipuka Machi mwaka huu.
Kocha wa timu ya taifa ya Congo, Claude Leroy amesema itakuwa ngumu na hatari kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo na kudai kuwa hata majirani zao Cameroon tayari wamefunga mipaka yao ili kuepusha maambukizi zaidi.
Hata hivyo NFF wamesisitiza kuwa mchezo utafanyika kama ulivyopangwa katika Uwanja wa UJ Esuene uliopo mji wa Calabar.
No comments:
Post a Comment