STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 27, 2014

Mbunge Viti Maalum ataka viti maalum vifutwe Katiba Mpya

Ritta Kabati alipokuwa kitoa mtazamo wake kuhusu viti maalumu vya ubunge


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) amesema moja ya mambo anayounga mkono katika mchakato wa Katiba Mpya ni kufutwa kwa viti maalumu vya ubunge.
Akizungumza hivi karibuni nje ya jengo la CCM Mkoa wa Iringa, Kabati alisema Viti Maalumu vina faida zake katika mchakato wa maendeleo lakini vinawadhalilisha sana wanawake.
“Siku hizi wabunge wanawake wa viti maalumu tunaitwa wabunge wa vitanda maalumu, huu ni udhalilishaji kwa sababu wengi wanahisi upatikanaji wake una mahusiano yasiofaa,” alisema.
Alisema utaratibu unaotumiwa na nchi kama Uganda na Rwanda kupata wawakilishi wanawake katika mabunge yao ndio unaopaswa kutumiwa na Tanzania na kama ikishindikana basi wanawake nao wapewe nafasi sawa na wanaume ya kugombea moja kwa moja kwenye majimbo ya Uchaguzi.
“Tumetembelea Uganda na Rwanda, kule hawaiti viti maalumu vya wanawake, wanaita viti vya wilaya vinavyoshindanisha wanawake wa vyama mbalimbali katika wilaya hizo,” alisema.
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, Kabati alisema endapo viti maalumu vitafutwa ataamua wapi atupe karata yake kati ya jimbo la Iringa Mjini au Kilolo.

“Kilolo ni kwetu na Iringa Mjini ni kwetu, kwahiyo kama Katiba Mpya itaondoa viti maalumu basi nitaamua wapi niende kati ya majimbo hayo,” alisema.

No comments:

Post a Comment