STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 19, 2014

Gareth Bale bado aiwaza Spurs, ahidi kurejea

Gareth Bale alihama Spurs masimu uliopita
http://www.guinnessworldrecords.com/media/6352324/Gareth-Bale-main.jpgWINGA machachari wa Real Madrid, Gareth Bale amezungumzia dokezo la kurejea Tottenham hapo baadaye.
Nyota huyo aliondoka White Hart Lane msimu uliopita kwa rekodi ya dunia ya uhamisho na ameendelea kuimarisha kiwango chake nchini Hispania.
Lakini licha ya kuonekana ametulia ndani ya kikosi akiwa sambamba na Cristiano Ronaldo ndani ya Bernabeu, Bale amesema bado anaipenda Tottenham.
"Tottenham siku zote itaendelea kuwepo ndani ya moyo wangu. Natumaini mashabiki bado wananipenda inagawa nimeondoka," alisema wakati akiongea na BT Sport.
"Nawapenda mashabiki wa Spurs. Huwezi jua ninaweza kurejea siku moja".

Katibu Mkuu Coastal Union 'kizimbani' TFF

http://1.bp.blogspot.com/-m-eOTD4-Boc/UDyJyvnKKwI/AAAAAAAAPFM/iLLhP7kUPho/s640/DSC04297.JPG
El Siagi (katikati)
KATIBU Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi atafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushinikiza mkutano wa wanachama wa klabu hiyo ufanyike bila kuandaliwa na Kamati ya Utendaji. Pia El Siagi alitumia vyombo vya habari kuishambulia TFF ambayo haikutambua uamuzi wa mkutano huo ulioelezwa kumdumaza Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Steven Mnguto. TFF ilimtuma Mkurugenzi wake Msaidizi wa Sheria na Uanachama kufanya uchunguzi wa mgogoro uliokuwa unaendelea katika klabu hiyo. Baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi huo, TFF imebaini kuwa Mwenyekiti na Mweka Hazina wa klabu hiyo walishajiuzulu, hivyo uitishwe uchaguzi haraka na kujaza nafasi hizo na nyingine zilizo wazi.
Pia wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Salim Amir na Albert Peter wameonywa kwa kushiriki katika mkutano ambao wanajua haukuandaliwa na Kamati ya Utendaji.
Vilevile uchunguzi wa TFF umebaini kuwa ushiriki wa Salim Bawazir na Akida Machai kwenye vikao vya Kamati ya Utendaji ya Coastal Union si halali kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wanachaguliwa na Mkutano Mkuu na si kuteuliwa na Mwenyekiti.
Kwa vile kutakuwa na uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo zipo wazi, uchaguzi huo utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Coastal Union kwa kushirikiana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga na Coastal Union watafanya uhakiki wa reja ya wanachama.

Hujuma mechi ya Stars, Mambas kuchunguzwa

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/07/10s.jpgSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea tuhuma za hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu mashindano ya AFCON. TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya. TFF itateua jopo la kuchunguza tuhuma hizi. Wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania (Members of TFF Family) watakaohitajika kuhojiwa na jopo hilo kwa mujibu wa Ibara ya 37 ya Kanuni za Maadili za TFF watalazimika kutoa ushirikiano. 
Atakayeshindwa kutoa ushirikiano atachukuliwa hatua za kimaadili. 
Pia wadau wa mpira wa miguu ambao sio wanafamilia wa TFF, watakaoitwa na jopo hili wanaombwa watoe ushirikiano kwa nia ya kujenga mpira wetu.

Uongozi Yanga kitanzini, TFF yaipa wiki 2

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/yangaa%20clement.JPG?itok=3lkNdTVBSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kuwasilisha rasimu ya Katiba waliyoipitisha, kwa kuzingatia kuwa Muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu wao wa Juni 1 mwaka huu umeainisha baadhi ya marekebisho waliyofanya kwa tulivyowaelekeza.
Yanga wanatakiwa kuwasilisha rasimu hiyo kabla ya Oktoba 5 mwaka huu. Ikiwa itakubaliwa na TFF, itapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo ili waweze kufanya uchaguzi wa viongozi wao.

Kivumbi England, Arsenal kesho, Man City, Chelse J'pili

http://img.eplmatches.com/2014/06/premier-league.jpg
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea tena kesho wakati Arsenal watakapokuwa ugenini kuvaana na wenyeji wao Aston Villa, huku kazi nzima ikiwa Jumapili.
Arsenal iliyotoka kukong'otwa mabao 2-0 na Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya watawafuata Villa ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa ikiwa nafasi ya pili katika msimamo nyuma ya Chelsea wanaoongoza wakiwa na pointi 12, Villa ikiwa na 10.
Arsenal inayokamata nafasi ya saba itahitaji ushindi ili kurejea kwenye mbio zao za kutaka kutwaa ubingwa licha ya kukabiliwa na majeruhi katika kikosi chao.
Mechi nyingine za kesho Jumamosi zitakuwa ni kati ya vibonde QPR waliozabuliwa mabao 4-0 wiki iliyopita na Manchester United itakapokuwa nyumbani kuialika Stoke City, huku Liverpool itaifuata West Ham ikiwa inaugua kipigo ilichopewa wiki iliyopita na Aston Villa.
Ratiba kamili ya kesho ni;
14:45 QPR v Stoke  
17:00 Aston Villa v Arsenal
17:00 Burnley v Sunderland
17:00 Newcastle v Hull
17:00 Swansea v Southampton
19:30 West Ham v Liverpool
Jumapili  
15:30 Leicester v Man United  
15:30 Tottenham v West Brom
18:00 Everton v Crystal Palace
18:00 Man City v Chelsea
Ratiba nyingine ya ligi hiyo;
Jumamosi Septemba 27  
14:45 Liverpool v Everton
17:00 Chelsea v Aston Villa
17:00 Crystal Palace v Leicester
17:00 Hull v Man City
17:00 Man United v West Ham
17:00 Southampton v QPR
17:00 Sunderland v Swansea
19:30 Arsenal v Tottenham
Jumapili Septemba 28
18:00 West Brom v Burnley
Jumatatu Septemba 29  
22:00 Stoke v Newcastle

Jose Mourinho aanza mikwara yake England

http://cdn2.crhoy.com/wp-content/uploads/2014/06/Mou1.jpg 
SAA chache kabla ya kuvaana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Jose Mourinho a.k.a Only Special' ameanza zake.
Meneja huyo wa Chelsea amedai hana tatizo katika kikosi chake na kwamba wapo kamili gado kuivaa  Manchester City Jumapili katika mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Etihad. 
Mourinho ameshuhudia kikosi chake kikishinda kila mchezo wa Ligi Kuu msimu huu lakini waligonga mwamba kwa Schalke Jumatano wakati walipolazimishwa sare. 
Hata hivyo, Mourinho anaamini Chelsea ina uwezo wa kuwafunga mahasimu wao hao katika mbio za ubingwa na kusisitiza wanajiamini kwa uwezo wao kuelekea katika mchezo huo. 
Kocha huyo kutoka Ureno, 51 amesema siku zote ni jambo zuri kucheza dhidi ya timu kubwa kwani inafanya kazi yake kuwa rahisi. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wanaiheshimu City kwasababu wanastahili lakini wao pia wanajiamini kufanya vyema katika mchezo huo.

MCT yalaani 'uhuni' wa Polisi kwa waandishi wa Habari

We unajifanya mjuaji eeh?
Hivi ndivyo baadhi ya askari wetu wanavyoshindwa kuthamini kazi za watu wengine. Hapa wakimsulubu mwandishi wa habari katika tukio la jana ambalo MCT limelilaani.

Kumekucha Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-2015

Watetezi Azam watakuwa nyumbani kuialika Polisi Moro


Yanga wenyewe watakuwa Moro kucheza na Mtibwa, watatoka salama?
Simba wataanza kibarua chao Jumapili dhidi ya Coastal Union
JKT Ruvu wenyewe watakuwa Mbeya kupepetana na Mbeya City
FILIMBI ya kuanza kwa kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-2015 kinatarajiwa kupulizwa rasmi kesho wakati viwanja sita vitakapowaka moto kwa kushuhudia timu 12 kati ya 14 zitakapoanza mbio za kuufukuzia ubingwa wa ligi hiyo.
Kuanza kwa ligi hiyo kutatoa picha halisi ya tambo na mbwembwe za timu wakati wa usajili kwani kwa kuwa soka ni mchezo wa hadharani mashabiki watajua mbivu na mbichi juu ya vikosi hivyo.
Kwa miezi minne klabu 14 za ligi hiyo zimekuwa zikitambiana kuhusu vikosi ilivyosajili na kujigamba kwa matokeo ya mechi kadhaa za kirafiki za kujiandaa na ligi hiyo, hata hivyo tija na ukweli wa ufanisi wa usajili huo utafahamika baada ya kuanza kwa ligi hiyo kesho.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mabingwa watetezi Azam ambao wiki iliyopita walishindwa kufurukuta mbele ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, itakuwa dimba la nyumbani kupepetana na maafande wa Polisi-Moro waliorejea kwenye ligi hiyo katika pambano litakalochezwa uwanja wa Chamazi.
Yanga wenyewe wakiwa na kocha mpya Marcio Maximo kutoka Brazili watakuwa uwanja wa Jamhuri Morogoro kupepetana na wenyeji wao, Mtibwa Sugar ambao hawajawahi kupoteza mchezo wowote kwenye dimba hilo mbele ya Yanga tangu mwaka 2009.
Ratiba Kamili ya kesho;
Septemba 20,2014.
Azam FC vs Polisi Moro [Azam Dar es Salaam] Mtibwa Sugar vs Yanga [Jamhuri, Morogoro] Stand United vs Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga] Mgambo JKT vs Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga] Ruvu Shooting vs  Prisons [Mabatini, Mlandizi] Mbeya City vs JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya] JUMAPILI:
Simba v Coastal Union [Taifa, Dar es Salaam]

Wembley kutumika Nusu Fainali Ulaya 2020

https://www.daytona.co.uk/news_images/WEM_007936.jpgSHIRIKISHO la Soka Ulaya, UEFA limethibitisha kuwa Uwanja wa Wembley uliopo jijini London Uingereza ndiyo utakaotumika kwa mchezo wa nusu fainali na fainali ya michuano ya Ulaya 2020. 
Viwanja vya Hampden Park na Dublin Aviva vilivyopo jijini Glasgow, Scotland vinatarajiwa kutumika kwa ajili ya mechi za hatua ya 16 bora na mechi tatu za hatua ya makundi. 
Chama cha Soka nchini Uingereza,FA kilishinda nafasi hiyo baada ya Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB kujitoa muda mchache kabla ya kura za UEFA na kuamua kuhamishia nguvu zao katika kutafuta nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2024. 
Michuano ya mwaka 2020 UEFA imefanya kuwa maalamu hivyo itaandaliwa katika viwanja 13 kutoka miji tofauti barani Ulaya. 
Mechi za robo fainali na tatu za hatua ya makundi zitaandaliwa jijini Munich, (Ujerumani), Baku (Azerbaijan), Roma (Italia) na St Petersburg (Urusi). 
Miji mingine itakayoandaa mechi 3 za makundi na moja ya mkondo wa pili ni Copenhagen (Denmark), Bucharest (Romania), Amsterdam (Uholanzi), Bilbao (Uhispania), Budapest (Hungary) na Brussels (Ubeljiji).

Maskini Arsenal yamkosa Debuchy wiki 6

http://ep.imgci.com/PICTURES/CMS/72200/72245.3.jpgIMETHIBITIKA kuwa, beki wa kulia wa Arsenal, Mathieu Debuchy atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita hali inayozidi kuiweka pabaya klabu hiyo.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Debuchy atakaa nje ya uwanja kwa kipindi hicho kutokana na kuumia kwake kifundo cha mguu. 
Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye alitolewa nje kwa machela katika mchezo dhidi ya Manchester City Jumamosi iliyopita anaweza kukosekana kwa miezi mitatu kama itahitajika kufanyiwa upasuaji. 
Wenger alithibitisha hilo na kudai kuwa matokeo zaidi watayajua katika siku chache zijazo baada ya kufanyiwa vipimo zaidi kuonyesha jinsi eneo hilo lilivyoathirika. 
Calum Chambers,19 anatarajiwa kuchukua nafasi ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 katika mchezo wa kesho dhidi ya Aston Villa. 
Debuchy aliyejiunga na Arsenal akitokea Newcastle United Julai mwaka huu amecheza katika mechi zote saba za timu hiyo msimu huu ukiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City. 
Beki mwingine kinda Hector Bellerin,19 ndio aliyeingia kucheza nafasi ya upande wa kulia katika mchezo wa Jumanne waliofungwa na Borussia Dortmund kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hatari! Mke wa mtu afa kwa hawara Dar

MWANAMKE Jane Bhoke (27) amefariki dunia nyumbani kwa hawara yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kifo hicho kilitokea juzi saa 12 jioni eneo la Zingiziwa Chanika wilayani Ilala.
Kamanda Nzuki alisema mtoa taarifa, Mohamed Kambi (44) mkazi eneo hilo alieleza kwamba alikutana na marehemu Septemba 12 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji huko Chanika.
Kambi alisema baada ya kukubaliana walianza kuishi kama mke na mume na huku akibainisha kwamba walifanya mapenzi mara mbili.
“Septemba 15 saa 11 jioni mtoa taarifa na marehemu walikwenda magengeni kununua mahitaji ghafla marehemu alianguka akawa analalamika mguu wa kulia unamuuma… katika harakati za kupunguza maumivu alimeza dawa aina ya diclopa,” alisema kamanda.
Alisema hali ya mgonjwa haikubadilika na ilipofika Septemba 16 saa 10 jioni alifariki dunia huku akibainisha kwamba haifahamiki marehemu ni mkazi wa wapi.