STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 19, 2014

Kumekucha Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-2015

Watetezi Azam watakuwa nyumbani kuialika Polisi Moro


Yanga wenyewe watakuwa Moro kucheza na Mtibwa, watatoka salama?
Simba wataanza kibarua chao Jumapili dhidi ya Coastal Union
JKT Ruvu wenyewe watakuwa Mbeya kupepetana na Mbeya City
FILIMBI ya kuanza kwa kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-2015 kinatarajiwa kupulizwa rasmi kesho wakati viwanja sita vitakapowaka moto kwa kushuhudia timu 12 kati ya 14 zitakapoanza mbio za kuufukuzia ubingwa wa ligi hiyo.
Kuanza kwa ligi hiyo kutatoa picha halisi ya tambo na mbwembwe za timu wakati wa usajili kwani kwa kuwa soka ni mchezo wa hadharani mashabiki watajua mbivu na mbichi juu ya vikosi hivyo.
Kwa miezi minne klabu 14 za ligi hiyo zimekuwa zikitambiana kuhusu vikosi ilivyosajili na kujigamba kwa matokeo ya mechi kadhaa za kirafiki za kujiandaa na ligi hiyo, hata hivyo tija na ukweli wa ufanisi wa usajili huo utafahamika baada ya kuanza kwa ligi hiyo kesho.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mabingwa watetezi Azam ambao wiki iliyopita walishindwa kufurukuta mbele ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, itakuwa dimba la nyumbani kupepetana na maafande wa Polisi-Moro waliorejea kwenye ligi hiyo katika pambano litakalochezwa uwanja wa Chamazi.
Yanga wenyewe wakiwa na kocha mpya Marcio Maximo kutoka Brazili watakuwa uwanja wa Jamhuri Morogoro kupepetana na wenyeji wao, Mtibwa Sugar ambao hawajawahi kupoteza mchezo wowote kwenye dimba hilo mbele ya Yanga tangu mwaka 2009.
Ratiba Kamili ya kesho;
Septemba 20,2014.
Azam FC vs Polisi Moro [Azam Dar es Salaam] Mtibwa Sugar vs Yanga [Jamhuri, Morogoro] Stand United vs Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga] Mgambo JKT vs Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga] Ruvu Shooting vs  Prisons [Mabatini, Mlandizi] Mbeya City vs JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya] JUMAPILI:
Simba v Coastal Union [Taifa, Dar es Salaam]

No comments:

Post a Comment