SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa
zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea tuhuma za
hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu mashindano
ya AFCON.
TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya. TFF itateua jopo la kuchunguza tuhuma hizi.
Wanafamilia
wa mpira wa miguu Tanzania (Members of TFF Family) watakaohitajika
kuhojiwa na jopo hilo kwa mujibu wa Ibara ya 37 ya Kanuni za Maadili za
TFF watalazimika kutoa ushirikiano.
Atakayeshindwa kutoa ushirikiano
atachukuliwa hatua za kimaadili.
Pia
wadau wa mpira wa miguu ambao sio wanafamilia wa TFF, watakaoitwa na
jopo hili wanaombwa watoe ushirikiano kwa nia ya kujenga mpira wetu.
No comments:
Post a Comment