RAIS Jakaya Kikwete anasubiriwa kwa hamu na watanzania kukata kiu juu ya baadhi ya mambo yaliyojiri nchini ambayo yameliacha taifa kwenye sintifashamu.Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow zipatazo bil. 306, na mvurugano uliojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni kati ya vinavyosubiriwa kusikia Rais atasema nini.
Juzi watanzania walidokezwa kuwa kungekuwa na fursa kwa Rais kuzungumza na wananchi kabla ya kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kukanusha taarifa hizo na kudai Rais atazungumza na Watanzania kesho kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Je mawaziri waliotajwa kuhusika kwa namna moja juu ya sakata ya Escrow na uchaguzi wa serikali za mitaa waenda na maji au watapeta kulingana na duru za kisiasa na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaigana kwamba hatajiuzulu na pia yeye na Rais wametoka mbali?
Ngoja tusubiri tuone Rais atakata kiu ya watanzania kivipi hiyo kesho katika hotuba yake!
MWANAMKE mmoja raia wa
Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto
wa jirani bila ruhusa anakabiliwa
na kifungo cha karibu miaka
miwili kwa kumwambukiza mtu
HIV kwa kukusudia kwa kuwa
yeye ni mwathirika.


BAO la dakika ya 90 lililofungwa na Adam Johnson limeiwezesha Sunderland kuwatambia wapinzani wao wa jadi Newcastle United wakiwa nyumbani kwao katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.








