STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 21, 2014

Liverpool, Arsenal hakuna mbabe

Borini akilimwa kadi kizembe
Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la pili
PAMBANO la kukata na shoka baina ya Liverpool na Arsenal limemalizika hivi punde kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2, huku wenyeji wakimaliza pungufu baada ya Fabio Borini kuonyesha kadi ya pili ya njano iliyoambatana na nyekundu na kutolewa nje ya uwanja wakati timu yake ikiwa nyuma ya ba02-1.
Borini aliyeingia toka benchi alipewa kadi hiyo, dakika ya 90 lakini vijana na Branden Rodgers walicharuka na kurejesha bao dakika za majeruhi kupitia Martin Skrtel.
Kabla ya hapo wageni walipata bao la pili dakika ya 64 kupitia kwa Olivier Giroud na kuonekana kama Arsenal wataibuka na ushindi kabla ya beki Skrtel akiwa amefungwa kichwani kutokana na kuumia kuryka juu kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Adam Lallana na kuipa afueni Liverpool iliyoiengua Everton na kukaa nafasi ya 10 kutoka ile ya 11 waliokuwa wakishikilia.
Arsenal kwa sare hiyo imeishusha Tottenham hotspur na kukalia nafasi ya sita licha ya zote kulingana pointi 27 kila moja baada ya timu zote kucheza mechi 17, ila zinatenganishwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment