STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

Mashali kuwania taji dhidi ya Mganda

Thomas Mashali
Med Sebyala


BONDIA wa Ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali, amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati na Mganda Medi Sebyala, mchezo utakaofanyika Oktoba 14 mwaka huu katika Ukumbi wa friends Corner.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO Regina Gwae amesema leo kwamba mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Thomas mashali sasa anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vyema nchini.

“huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda ulaya Afrika mashariki ukaikimbia hivyo tumeona tumpe mchezo Afika mashjariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa, alisema Regina.

Amesema kwa upandewa mazungumzo na Bondia Medi Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa Mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo.

“ pamabano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na afrika mashariki kwa ujumla huwezi kuacha kuwataja mashali na sebyala,alisema regina.

Regina amesema tunataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala nae ni Bondia Mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia Fransis Cheka wa Morogoro na rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti.

Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unatarajiwa kuwa na mapambanio yaq utangulizi yenye kuvutia ambapo mabondia wake waktatangazwa baadae watakaosindikiza mpambano huo.

TOFAUTI YA KATI YA MABASI YA SIMBA  YANGA NA LA GOR MAHIA

 yasemekana hili ni basi lililo nunuliwa na mashabiki wa Gor Mahia kwa ajili ya timu yao
 
 
 Mabasi ya Simba na yanga - PICHA KWA HISANI YA http://moronew.blogspot.com

TBL YAKABIDHI MABASI YA KISASA KWA SIMBA NA YANGA


 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akicheza sambamba na mashabiki wa timu hiyo wakionesha furaha yako baada ya Kampuni ya Bia Tanzania TBL kuvikabidhi klabu za Simba na Yanga mabasi mapya katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche  kulia akimkabidhi mfano wa ufunguo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wakati wa hafla ya kukabidhi basi jipya kwa klabu hiyo. TBL ndio mdhamini Mkuu wa klabu za Simba na Yanga.
 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche kama ishara ya makabidhiano ya basi jipya lililotolewa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo
 Viongozi wa Simba na Yanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa TBL
Mkuu wa Usambazaji wa TBL, James Bokella akionesha ishara ya kuanza rasmi kwa msafara wa kuyatembeza magari ya Simbana Yanga katika mitaaya jiji la Dar es Salaam ili mashabiki wa timu hizo wayaone.
Aliyedai Asizikwe Atafufuka Baada ya Siku Mbili Asababisha Balaa

NewsImages/6601474.jpg
Tuesday, September 18, 2012 4:25 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini ambaye alidai enzi za uhai wake kuwa atakapofariki asizikwe kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili ameshindwa kufufuka baada ya kifo chake na maiti yake imekuwa kero kwa watu kutokana na harufu kali inayotoa.
Mwanaume huyo aliyekuwa mkazi wa Tsolo, Eastern Cape nchini Afrika Kusini aliwaagiza ndugu zake wakati wa uhai wake kuwa atakapofariki basi mwili wake usipelekwe monchwari kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili.

Mwanaume huyo alifariki jumanne ya wiki iliyopita na ndugu zake walifuata maagizo yake kwa kuuweka mwili wake nyumbani kwake wakimsubiria arudi toka kuzimu akiwa hai tena.

Familia yake iliendelea kuutunza mwili wake huku wanajumuiya wa kanisa lake wakija kumuombea dua.

Baada ya siku mbili kupita ambazo alidai angefufuka maiti yake ilianza kuharibika na kutoa harufu kali iliyoanza kuwa kero kwa majirani.

Msemaji wa eneo hilo aliyetambulishwa kama Sizwe Kupelo aliwaambia waandishi wa habari kuwa majirani wameanza kulalamika harufu kali inayotoka kwenye nyumba yake.

"Limekuwa tatizo la kiafya sasa, watu wanaohofia kupata maambukizi", alisema Kupelo.

Timu ya maafisa wa afya na mapolisi walitarajiwa kuitembelea familia hiyo na kuishawishi iachane na mawazo ya kusubiria kufufuka kwa ndugu yao na hatimaye wauzike mwili wake kama inavyotakikana.


Nifahamishe.com    

Kocha Yanga akiri kuzidiwa ujanja na Mtibwa alaumu wachezaji wake

Kocha Tom Saintfiet akiwa haamini kama jahazi la timu yake limezana uwanja wa Jamhuri, walipokandikwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar

KOCHA wa klabu ya Yanga, Tom Saintfiet, amekiri timu yake ilizidiwa maarifa na Mtibwa Sugar na kulazwa mabao 3-0, akidai hakuna cha kusingizia kwa kipigo hicho.
Akihojiwa na kituo kimoja cha redio, Mbelgiji huyo alisema tofauti na utetezi wake katika mechi iliyopita waliotoka sare ya 0-0 na Prisons Mbeya, kipigo cha Mtibwa kilikuwa halali kwa sababu kila kitu kwao kilikuwa vema.
Saintfiet, alisema hawezi kusema uwanja wa Jamhuri ulikuwa mbaya, ama chakula au hoteli waliyolala kama ilivyokuwa mjini Mbeya, zaidi ya kuwashutumu wachezaji wake kwamba hawakuwa makini uwanjani kutumia nafasi walizopata.
"Mtibwa walipata nafasi nne na kuzitumia vema tatu kwa kufunga mabao matatu, wakati sisi tulipata karibu nafasi nane na hata moja hatukutumia," alisema.
Aliongeza amegundua kinachowaathiri wachezaji wake ni kulewa sifa za magazetini na hivyo kuishia kushindana kubadilisha mitindo ya nywele na viatu badala ya kushindana uwanjani kuisaidia timu.
"Wamelewa sifa, walisifiwa kwenye michuano ya Kagame na wamejisahau wao kila siku wamekuwa wakishindana kubadilisha mitindo ya nywele na viatu, watambue wakati mwingine wanapaswa kufanya nini uwanjani," alisema.
Alidai lau kama yeye (Saintfiet) na msaidizi wake, Fred Felix Minziro wangeingia uwanjani wangeweza kufunga mabao kwa nafasi walizokuwa wamezitengeza.
Yanga ilikumbana na kipigo hicho cha 3-0 toka kwa Mtibwa katika mechi ambayo Hamis Kiiza alikosa penati dakika lala salama, na kuicha ikisaliwa na pointi moja tu.
Timu hiyo kesho inatarajiwa kushuka dimbani kuumana na JKT Ruvu katika mechi nyingine ngumu, ingawa Saintfeit amedai amezungumza na wachezaji na kuahidi kurekebisha makosa kwa kuipa timu ushindi hili mambo yasiendelee kuwa mabaya.

  WILSHERE, FRIMPONG WAPONA WAJIFUA NA WENZAO

Jack Wilshere
Emmanuel Frimpong
LONDON, England
Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere amerudi kikosini na kujifua na wenzake katika muda wote wa mazoezi leo baada ya kuwa nje kwa miezi 14 kutokana na jeraha la muda mrefu la 'enka'.

Kiungo huyo mwenye miaka 20 alikuwamo katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na kuitwa pia katika kikosi cha timu ya taifa ya England kabla ya kuondolewa baadaye.

"Tumefurahi sana, Jack amerudi kamili mazoezini. Amekuwa nje kwa miezi 14 na hicho ni kipindi kirefu kwa mtu wa umri wake. Ni habari njema," kocha Arsene Wenger ameiambia tovuti ya klabu yake (www.arsenal.com).

Kiungo mwenzake Emmanuel Frimpong pia amerudi mazoezini baada ya kuumia goti Februari wakati akichezea Wolverhampton Wanderers kwa mkopo.

Wote, Wilshere na Frimpong watakabiliwa na kazi ngumu ya kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya  Wenger kumleta kiungo wa timu ya taifa ya Hispania, Santi Cazorla na Arsenal kuanza vizuri msimu huu wa Ligi Kuu ya England, wakishika nafasi ya tatu baada ya mechi nne.

AIRTEL YAKABIDHI T-SHIRT 400 NA MILIONI TANO KWA AJILI YA MASHINDANO YA RIADHA YA ROCK CITY


Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati ya T-shirt mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-shirt mia nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo.


Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati ya T-shirt mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-shirt mia nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo.
Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi T-shirt mia nne zitakazotumika katika mbio hizo.

AIRTEL yaahidi kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini

KAMPUNI ya mawasiliano nchini ya Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kukabidhi shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne kama udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zenye kauli mbiu ‘tukuze utalii wa ndani kupitia michezo’, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwemo riadha ili kukuza maendeleo ya vijana.
“Udhamini wetu wa shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne katika mbio za Rock City mwaka huu unalenga katika kusukuma maendeleo ya vijana kupitia michezo kwa kuwa tunaamini kuwa michezo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira duniani.
“Tunaahidi kuendelea kusaidia michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini kupitia michezo mbalimbali tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii duniani. Mfano nzuri ni mbio za mwaka huu za Rock City Marathon zitakazowakutanisha wanariadha mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza Bi. Matinde.
Akipokea hundi na T-shirt hizo, Mratibu wa mbio hizo kutoka katika kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa mashirikia na makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo.
“Tunaishukuru Airtel kwa msaada wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia tujiandae vizuri na Rock City Marathon ya mwaka huu itakayofanyika Oktoba tarehe 28 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema Grace.
Grace alisema kuwa mbali na Airtel wadhamini wengine ni pamoja na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita Gold Mine, African Barrick Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL), Mamlaka ya Taifa ya Mbuga za Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Nyanza Bottles, New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.
Aidha, Bi Sanga aliwaasa wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za Bodi ya Utalii jengo la IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com.
CPI ilitangaza kuwa atakayeibuka kinara katika mbio za kilometa 21 mwaka huu kwa wanaume na wanawake atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili wakati mshindi wa pili ataweka mfukoni shilingi laki tisa na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki saba.

FLAVIANA MATATA OPENS UP ABOUT HER LIFE & FASHION ON BBC AFRICA'S PROGRAMMES DIRA YA DUNIA & FOCUS ON AFRICAThe supermodel and former Miss Universe Tanzania (2007), Flaviana Matata, was in the UK for the London Fashion Week.
She spoke to the BBC a few hours before returning to New York where she is based when not working in Europe, Africa or other parts of the world. Here she is being interviewed for BBC Africa’s news and current affairs TV programme in Kiswahili, Dira ya Dunia.
 She was also interviewed for BBC's Focus on Africa radio programme. Listen to the interview at 1500 GMT. It will also appear on our podcast.
 Flaviana posing with BBC Africa's very fashionable presenter Kassim Kayira
 Flaviana with Jestina George of www.jestina-george.com (a blogger based in London) at the BBC studios in London
For the interview Flaviana rocked  a leather jacket from Zara, Dress from Mango, Gucci sunglasses & gorgeous shoes from McQueen.
---
Tanzania's supermodel Flaviana Matata has had a very busy schedule and to be precise she's been busy on the runway between New York  & London. 

At the moment Flaviana is in the UK where she has just taken part in London Fashion Week.
Earlier today Flaviana visited the BBC  Africa studios in London where she was interviewed for BBC Africa’s news and current affairs TV programme in Kiswahili, Dira ya Dunia  &  for Focus on Africa.

The former winner of Tanzania's first Miss Universe pageant, in 2007, started by telling how she got into the fashion industry and later dished out on the latest tips on what is fashionable these days.Below is the link where you can listen to the Focus on Africa interview. It is also being currently promoted on the BBC’s Entertainment & Arts pages. 
 For more African news from the BBC download the Africa Today podcast.

 Photo credit: Manuel Toledo, BBC Africa

DIAMOND KUPATA WENYE VIPAJI KESHONa Elizabeth John
MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania kupitia muziki wengi wenye vipaji mitaani na kwenye sekta nyingine, wasiojua wafanyeje kufikia ndoto zao, hivyo kuhitaji kushikwa mkono na wengine.
Akizungumza na Habari Mseto, Diamond alisema tatizo kubwa ni jamii kuchukulia masuala ya mitindo na muziki kama uhuni na kuuza sura yaani kupata umaarufu tu kwenye televisheni na vyombo vingine vya habari, akisema kuna haja ya kuifanya jamii kuachana na fikra hizo.
“Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine.

Najua wapo wanaoweza ‘kufit’ kwenye matangazo ya biashara, pia watapata fursa hiyo,” alisema Diamond.
Kuhusu majaji katika mchujo huo utakaofanyika Nyumbani Lounge kuanzia saa 5 asubuhi, aliwataja kuwa ni Raqey Mohammed wa I-View Studios watakaofanya kazi za matangazo, Ally Rehmtulah ambaye ni Mbunifu na Sammy Cool, mcheza dansi na mwalimu.
Kwa mujibu wa Diamond, jaji mwingine ni Missie Popular ambaye ni mwandishi na mwanamitindo anayejua wapi kwa kuwafikisha watu wengine kama alivyofanikiwa yeye kupitia muziki.

ZAWADI SAFARI POOL TAIFA 2012 ZATANGAZWAMeneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari
Na Elizabeth John
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, leo imetangaza zawadi za washindi wa mashindano ya Safari Pool Taifa yanayotarajiwa kufanyika Septemba 26 hadi 29, mwaka huu jijini Mwanza kwa kushirikisha mabingwa wa klabu kutoka mikoa 16 ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema zawadi kwa bingwa wa fainali za Safari Pool Taifa 2012 ni pesa taslimu shilingi milioni tano, Kombe na Medali za dhahabu kwa washindi wa upande wa timu.
Shelukindo alisema kuwa, zawadi za washindi wa pili itakuwa ni shilingi 2,500,000, huku washindi wa tatu wakiondoka na kitita cha shilingi 1,250,000, ambapo washindi wa nne watajinyakulia shilingi 750,000.
Alisema kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja, mshindi kwa wanaume atajinyakulia kiasi cha shilingi 500,000, huku bingwa wa wanawake akinyakua shilingi 350,000 na mshindi wa pili wanaume atapata shilingi 250,000.
Mshindi wa pili kwa wanawake, ataondoka na shilingi 200,000 na mshindi wa tatu kwa wanaume atapata shilingi 200,000, huku mshindi wa nafasi hiyo kwa wanawake akiondoka na kitita cha shilingi 150,000.
Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga, alizitaja klabu zilizofuzu kushiriki fainali za Taifa jijini Mwanza kuwa ni Balele ya Tanga, Mbosho ya Kilimanjaro,  2 Eyes ya Arusha, Janja Wild ya Manyara, Sabasaba ya Lindi na Texas ya Tabora.
Nyingine ni New Stand ya Shinyanga, Anatory ya Morogoro, Atlantic ya Dodoma, Nginja ya Iringa, Blue House ya Mbeya, Sun City ya Temeke, Kayumba ya Ilala, Meeda kutoka Kinondoni, huku wenyeji wa mashindano hayo Mwanza wakitarajiwa kuwakilishwa na klabu ya Paseansi.

RUFAA YA LEMA YAHAIRISHWA HADI OCTOBER 2

 Msafara wa aliekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjii ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama
 Gari ya lema ikiwa inasukumwa na mashabiki mara baada yakutoka mahakamani
 Gari ya polisi ikiwa inapisha maandamano yapite kila mmoja alikuwa anashangilia kivyake
 wamama wakiwa wanapita njiani wakishangilia aliyekuywa mmbunge wakati akipita kutoka mahakamani
 wananchi wengine waliendeea na shughuli zao wakati msafara ukipita

 Hawa ni makamanda waliokuwa wamevalia Tisheti za M4C huku mungine akiwa ameshona kanzu kabisa

 Lema akiongea a wananchi nje ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani
 wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza lema

RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake, Natalia Kimaro na Salum Massatiumesikilizwa ila kesi imearishwa.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi leo imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali kupata matatizo ya kufiwa  na  baba yao mzazi
Jaji mkuu alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.
Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alongea na wananchi walikuwa wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki.
“mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi”alisema lema
Alibainisha kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo itajulikana   kufa au kupana ,mkutano ambao utafanywa kwa nyumba kwa nyumba  pamoja na kitongoji kwa kitongoji

Hata hivyo, habari za uhakika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa tayari mawakili wa pande zote mbili wameandika barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, mwaka huu, kufuatia mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji, kufiwa na baba yao mzazi.


Shauri hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa Jiji la Arusha na Watanzania wengi linatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja kisha kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.


Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.


Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.


Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.


Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.


Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Chanzo:Libeneke la Kaskazin

MADEREVA PIKIPIKI WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA MASAA MATATU POLISI WAWATAWANYA KWA MABOMU

Waandamanaji ambao ni madereva wa pikipiki mkoani Arusha,wakiwa wamefunga barabara ya Moshi Arusha katika eneo la Ngulelo huku wakionyesha moja ya mabango waliokuwa nao.
 Madereva wa bodaboda wakiziba barabara kuu ya Arusha Moshi na kufanya magari zaidi ya 100 kushindwa kupita kwa saa 3
 Askari wa FFU wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya madereva hao waliokuwa wamefunga njia
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana  mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa kagi hilo  kutaka kupita eneo walilosuia.
 
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya 300,jijini hapa wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha kwa zaidi ya saa 3 ,katika eneo Ngulelo jijini hapa , wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.
 
Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya  saa 4  asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .
Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki,Jonathan Emanuel ,Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru,maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36)mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi  septembe 15 mwaka huu akiwa barabarani  eneo la baraa akimsafirisha abilia aliyekuwa amemkodi.
 
 
Madereva hao wakiwa na mabango  yenye ujumbe mbalimbali  wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji(jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari  na mkazi wa Baraa jijini hapa ,walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja  walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake  lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.
 
Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza  mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.
 
Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao  walivunja vioo vya magari kwa kupiga  mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.
 
Hata hivyo polisi baada ya kufika eneo la tukio, waandamanaji hao walianza kupiga yowe huku wakirushia mawe  gari la polisi ambao walilazinika kuondoka kwa kasi kwa lengo la kujinusulu, ambapo baadae walirejea wakiwa na nguvu mpya  na kuanza kuwafyatua mabomu zaidi ya 10 na kufanikiwa kuwasambaratisha na kufungua njia .
 
Akisimulia chanzo cha mauaji hayo,Jonathan Emanuel alieleza kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na dereva mwenzake walikodishwa na abilia  wawili kwa lengo la kuwapeleka nyumbani kwao,lakini wakiwa njiani waliliona gari aina ya Escudo kwa mbele yao na kujaribu kulipita.
 
Alisema kuwa marehemu alijaribu kulipita gari hilo lakini  dereva wa gari hilo ambaye ni mtuhumiwa alimzuia kwa kuziba na kusimama ambapo alimuuliza alikuwa anakimbilia wapi.
‘’huyo dereva wa escudo alimzuia marehemu kupita kwa kuziba njia na kumhoji kuwa kwanini anakimbia na alikuwa nakimbilia wapi’’alisema
 
Alisema kuwa kulitokea majibishano  baina ya marehemu na mtuhumiwa ndipo mtuhumiwa huyo alipochomoa bastola na kumfyatulia risasi kifuani na kufariki dunia papo hapo huku abilia wake akiduwaa asijue la kufanya.
 
Madereva hao wanadai kuwa jeshi la polisi mkoani Arusha wameshindwa kuwatendea haki kwa kumbana mtuhumiwa ambaye anaonekana mtaani huku akitamba kuwa yeye ni zaidi yao na kwamba hawezi kufungwa kama wanavyofikiria.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap en o la Oldadae.
 

Chanzo:libeneke la kaskazini.blogspot.com