STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

RUFAA YA LEMA YAHAIRISHWA HADI OCTOBER 2

 Msafara wa aliekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjii ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama
 Gari ya lema ikiwa inasukumwa na mashabiki mara baada yakutoka mahakamani
 Gari ya polisi ikiwa inapisha maandamano yapite



 kila mmoja alikuwa anashangilia kivyake
 wamama wakiwa wanapita njiani wakishangilia aliyekuywa mmbunge wakati akipita kutoka mahakamani
 wananchi wengine waliendeea na shughuli zao wakati msafara ukipita

 Hawa ni makamanda waliokuwa wamevalia Tisheti za M4C huku mungine akiwa ameshona kanzu kabisa

 Lema akiongea a wananchi nje ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani
 wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza lema

RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake, Natalia Kimaro na Salum Massatiumesikilizwa ila kesi imearishwa.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi leo imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali kupata matatizo ya kufiwa  na  baba yao mzazi
Jaji mkuu alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.
Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alongea na wananchi walikuwa wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki.
“mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi”alisema lema
Alibainisha kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo itajulikana   kufa au kupana ,mkutano ambao utafanywa kwa nyumba kwa nyumba  pamoja na kitongoji kwa kitongoji

Hata hivyo, habari za uhakika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa tayari mawakili wa pande zote mbili wameandika barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, mwaka huu, kufuatia mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji, kufiwa na baba yao mzazi.


Shauri hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa Jiji la Arusha na Watanzania wengi linatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja kisha kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.


Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.


Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.


Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.


Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.


Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Chanzo:Libeneke la Kaskazin

No comments:

Post a Comment