STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

MADEREVA PIKIPIKI WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA MASAA MATATU POLISI WAWATAWANYA KWA MABOMU

Waandamanaji ambao ni madereva wa pikipiki mkoani Arusha,wakiwa wamefunga barabara ya Moshi Arusha katika eneo la Ngulelo huku wakionyesha moja ya mabango waliokuwa nao.
 Madereva wa bodaboda wakiziba barabara kuu ya Arusha Moshi na kufanya magari zaidi ya 100 kushindwa kupita kwa saa 3
 Askari wa FFU wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya madereva hao waliokuwa wamefunga njia
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana  mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa kagi hilo  kutaka kupita eneo walilosuia.
 
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya 300,jijini hapa wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha kwa zaidi ya saa 3 ,katika eneo Ngulelo jijini hapa , wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.
 
Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya  saa 4  asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .
Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki,Jonathan Emanuel ,Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru,maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36)mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi  septembe 15 mwaka huu akiwa barabarani  eneo la baraa akimsafirisha abilia aliyekuwa amemkodi.
 
 
Madereva hao wakiwa na mabango  yenye ujumbe mbalimbali  wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji(jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari  na mkazi wa Baraa jijini hapa ,walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja  walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake  lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.
 
Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza  mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.
 
Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao  walivunja vioo vya magari kwa kupiga  mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.
 
Hata hivyo polisi baada ya kufika eneo la tukio, waandamanaji hao walianza kupiga yowe huku wakirushia mawe  gari la polisi ambao walilazinika kuondoka kwa kasi kwa lengo la kujinusulu, ambapo baadae walirejea wakiwa na nguvu mpya  na kuanza kuwafyatua mabomu zaidi ya 10 na kufanikiwa kuwasambaratisha na kufungua njia .
 
Akisimulia chanzo cha mauaji hayo,Jonathan Emanuel alieleza kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na dereva mwenzake walikodishwa na abilia  wawili kwa lengo la kuwapeleka nyumbani kwao,lakini wakiwa njiani waliliona gari aina ya Escudo kwa mbele yao na kujaribu kulipita.
 
Alisema kuwa marehemu alijaribu kulipita gari hilo lakini  dereva wa gari hilo ambaye ni mtuhumiwa alimzuia kwa kuziba na kusimama ambapo alimuuliza alikuwa anakimbilia wapi.
‘’huyo dereva wa escudo alimzuia marehemu kupita kwa kuziba njia na kumhoji kuwa kwanini anakimbia na alikuwa nakimbilia wapi’’alisema
 
Alisema kuwa kulitokea majibishano  baina ya marehemu na mtuhumiwa ndipo mtuhumiwa huyo alipochomoa bastola na kumfyatulia risasi kifuani na kufariki dunia papo hapo huku abilia wake akiduwaa asijue la kufanya.
 
Madereva hao wanadai kuwa jeshi la polisi mkoani Arusha wameshindwa kuwatendea haki kwa kumbana mtuhumiwa ambaye anaonekana mtaani huku akitamba kuwa yeye ni zaidi yao na kwamba hawezi kufungwa kama wanavyofikiria.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap en o la Oldadae.
 

Chanzo:libeneke la kaskazini.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment