STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 4, 2015

ZAHIR ALLY ZORRO FT MWANA FA

VIJIMAMBO: ZAHIR ALLY ZORRO FT MWANA FA

Michuano ya Utalii Cup 2015 kutimka Feb 23 jijini Dar

http://www.mercurialsports.com/media/catalog/product/cache/1/image/9df78eab33525d08d6e5fb8d27136e95/t/r/tr1543f.jpgMICHUANO ya soka ya kuwania kombe la Utalii ‘Utalii Cup 2015’ inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 23, kwenye viwanja mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya Bos Promotions, Samuel Peter, alisema maandalizi yanakwenda vizuri na bingwa atazawadiwa Ng’ombe.
Peter alisema mbali ya zawadi hiyo, washindi wa kwanza pia watapata nafasi ya kutembelea moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini.
Alisema lengo la michuano hiyo ni kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi jijini Dar es Salaam na kutangaza utalii wa ndani kupitia mchezo wa soka.
Msemaji huyo alisema timu 12 zinatarajia kushiriki na zitapangwa katika makundi mawili ambapo nne za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya robo fainali.
Peter alisema milango ipo wazi kwa timu ya daraja lolote inayotaka kushiriki mashindano hayo yatakayokuwa yakifanyika kila mwaka.
“Maandalizi yanakwenda vizuri na tayari tumeshaanza kutoa fomu kwa timu zinazotaka kushiriki na namba ya mawasiliano ni 0714 743276”, alisema.

YANGA, COASTAL UNION NI VITA TUPU LEO MKWAKWANI

Wagosi wa Kaya, Coastal Union waliopania kuwatia maumivu vijana wa Jangwani leo Mkwakwani
Yanga waliopa kuondoa 'gundu' Mkwakwani kwa kuinyoa Coastal Union
COASTAL Union wametangaza vita ya dakika 90 dhidi ya Yanga katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, inayopchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku Yanga wenyewe akitamba kuwa wameenda Mkwakwani kuchukua pointi tatu kwa wenyeji wao.
Timu hizo zinakutana kwenye mchezo nhuo wa kiporo huku kila moja ikitoka kulazimishwa sare isiyo na mabao nyumbani katika mechi zao za mwishoni mwa wiki.
Yanga ilibanwa na Ndanda Fc kwenye uwanja wa Taifa, wakati Coastal ikiwa nyumbani ilishindwa kufurukuta kwa Mtibwa Sugar, hali inatyofanya pambano la leo kuwa kama vita ya kusaka pointi tatu kwa timu zote.
Coastal kupitia Msemaji wake, Oscar Assenga, amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kuwatoa nishai Yanga, wakati Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro akisema wameenda Tanga kuchukua pointi tatu kwa vile timu yao ni bora kuliko wapinzani wao.
Coastal inayonolewa na kocha James Nandwa kutoka Kenya itakuwa na kibarua kigumu kwa wapinzani wao licha ya kwamba kwa muda sasa Yanga haijaonja ushindi Mkwakwani dhidi ya Wagosi wa Kaya ama Mgambo JKT.
Mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilikuwa Novemba 12, 2012 iliposhinda 2-0.
Katibu Mkuu wa Coastal Kassim El Siagi alisema angetaka mashabiki wa soka kuthibitisha ipi timu ya soka la kweli la uwanjani na timu za magazetini ambao namna wanavyopambwa unaweza kusema ni Barcelona ilihali ni timu ya kawaida ionayoshindwa kuzifunga hata timu ndogo kama Ruvu Shooting na Ndanda FC.
Hata hivyo Yanga wameapa kufanya kweli leo baada ya kushuhudia safu yake ya ushambuliaji katika mechi tatu ilizocheza za Ligi Kuu ikifunga moja tu walipoilaza Polisi Moro.
Mashabiki wa Yanga pamoja na timu yao wapo mjini Tanga tangu majuzi kwa ajili ya pambano hilo ambalo litatoa taswira mpya ya msimamo wa Ligi Kuu timu mojawapo ikipata ushindi, Yanga ikiweza kurejea kileleni baada ya kutemeshwa muda mrefu na Mtibwa Sugar na baadaye Azam.
Kadhalika Coastal ikishinda inaweza kukwea hadi nafasi ya pili na kuwaengua Yanga waliopo katika nafasi hiyo kwa sasa wakiwa na pointi 19, mbili nyuma ya Azam wanaoongoza na pointi zao 21.
MSIMAMO LIGI KUU ULIVYO KWA SASA
                             P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Azam              11  06  03  02  15  08  07   21
02.  Yanga            11  05  04  02  12   07  05  19
03. Mtibwa Sugar  11  04  06  01  13  07  06   18
04. Polisi Moro      13  04  06  03   10  09  01  18
05. JKT Ruvu        13  05  03  05   13   13  00  18
06. Ruvu Shooting13  05  03   05   09   10  -1  18
07. Coastal Union 12  04  05   03  10   08  02  17
08. Simba            12  03  07   02   13   11  02  16
09. Mbeya City     12   04  03  05  08   10  -2   15
10. Kagera Sugar 13  03  06  04   10   11   -1  15
11. Mgambo JKT  11  04  02  05   06    10  -4  14
12. Ndanda Fc     13  04  02   07  12    17  -5  14
13. Stand Utd      13  02  05   06   08   16  -8  11
14. Prisons          12  01  07   04   09   11  -2   10

MWANASHERIA MKUU AKATA MZIZI WA FITINA MAHAKAMA YA KADHI

http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/2604484/highRes/932159/-/maxw/600/-/d4xms2z/-/AG_Masaju.jpg
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akizungumza na wanahabari
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/5.jpg
Viongozi wa Kiislam wakizungumza na wanahabari kupinga tamko la Jukwaa la Wakristo waliopinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni hivi karibuni
TEC
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo wakitoa msimamo wao wa kupinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni ikiwa kama sehemu ya msimamo wao wa kuikata tamaa mahakama hiyo ianzishwe nchini
WAKATI viongozi wa Kikristo wakiendelea kushupaa na kuipinga kwa nguvu Mahakama ya Kadhi inayoliliwa na Waislam nchini Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ameweka wazi kwamba hakuna jambo baya juu ya uwepo wa mahakama hiyo kama inavyolazimishwa kuaminishwa.
Kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE, limedokeza kuwa wakati muswada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ukitarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, amesema haitakuwa na athari yoyote hasi nchini.
Masaju alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE jijini Dar es Salaam akifafanua juu ya muswaa huo hasa baada ya kuwapo kwa dalili za mvutano kuhusu uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Alisema tatizo lililopo ni kwamba serikali haijachukua hatua madhubuti kuwaelimisha wananchi namna ambavyo mahakama hiyo itakuwa inaendesha kazi zake.
“Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwapo tangu zamani na ilikuwa ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Serikali hatuoni kwa nini suala hili lisifanikiwe,” alisema.
Masaju alisema Watanzania lazima watambue kuwa Mahakama ya Kadhi itahusu mambo ya Waislamu wenyewe ambayo ni mirathi, ndoa na talaka.
“Sioni kwa nini isifanikiwe kwa sababu mahakama hii haiwahusu watu ambao siyo Waislamu na pia haitakuwa ya kulazimisha,” alisema.
Alisema Mahakama hiyo kwa sababu itakuwa inashughulikia masuala binafsi kama ndoa na talaka ambayo serikali haishughuliki nayo.
Alisema serikali imekuwa ikishughulika na masuala ya jinai kama vile wizi, watu wanaokula rushwa hivyo mambo binafsi kama ya talaka haishughuliki nayo.
Aliongeza kuwa kujiunga katika Mahakama ya Kadhi itakuwa ni hiari hata miongoni mwa Waislamu na gharama za uendeshaji wake serikali haitahusika.
Masaju alisema suala hilo kama wananchi wakielimishwa haliwezi kuleta mgogoro kwa kuwa ni kitu cha kawaida na linafanyika katika baadhi ya nchi.
Alisema kimsingi suala hilo linakuzwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusisitiza kuwa Watanzania ni wamoja na watabaki kuwa wamoja.
Aliongeza kuwa watu ambao hawataki mahakama hiyo wataenda kwenye mahakama nyingine za kawaida.
“Pamoja na Mahakama ya Kadhi kuamua masuala hayo, mahakama za kawaida zitabaki kuwa na mamlaka ya kusikiliza masuala ya talaka, mirathi na ndoa,” alisema.
Alisema wakati wa Bunge Maalum la Katiba Waislamu walitaka suala hili liingizwe katika Katiba mpya, lakini serikali iliona yasiingizwe kwa sababu ni ya imani za dini na hivyo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliahidi serikali itapeleka muswada bungeni.
Akijibu swali la kwamba huenda kuwasilishwa bungeni kwa muswada huo sasa kunalenga kuvuruga Watanzania kuacha kufikiri masuala muhimu yaliyopo mbele kama uchaguzi mkuu, Masaju alisema siyo kweli.
Alifafanua kuwa masuala yote kama ya kura ya maoni kuamua Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu yote yana umuhimu na yataenda sambamba.
“Wakristo ni majirani wa Waislamu, Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja, katika baadhi ya familia wengine kuna Waislamu na Wakristo, mwanasheria mmoja aliniuliza ni amri ipi iliyokuu kuliko yote akasema, mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende jirani yako kama nafsi yako, Waislamu ni jirani zetu,” alisema.
Masaju alisema kutugwa kwa sheria hii ni kuwezesha Mahakama ya Kadhi kufanya kazi kwa kufuata utaratibu bila kuingilia mambo mengine ya serikali.
“Hii siyo mara ya kwanza kutunga sheria. Mtusaidie kama taifa, sioni sababu Watanzania kupigana na kupinga suala la Mahakama ya Kadhi na kusababisha kuvunjika kwa amani,” alisema.
Aliongeza kuwa Zanzibar wana Mahakama ya Kadhi, hivyo itakuwa jambo la kushangaza kwa nini Tanzania Bara kusiwe na mahakama hiyo hali ambayo italeta manung’uniko kwa Waislamu waliopo bara.
Alisema kwa waliosoma Chuo Kikuu cha Sheria Dar es Salaama suala la mahakama ya Kadhi hufundishwa kwa mwaka mzima ili kulielewa vizuri.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatumika hata Zanzibar, hivyo siyo jambo zuri bara kusiwe na Mahakama ya Kadhi kwani itawafanya Waislamu waliopo bara wasononeke.
“Tumeona Waislamu wanaona na Wakristo, hiki ni kitu cha kawaida kabisa hakuna sababu ya kulipinga, sisi wote tunategemeana, sisi ni ndugu, binadamu tunaoishi pamoja.
Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwa likizungumzwa sana bungeni tangu Augustino. Mrema alipopeleka hoja binafsi akidai Mahakama hiyo mwaka 1998.
Tangu wakati huo mwaka 1998 - 2000 iliundwa kamati ndogo ya Bunge kulishughulikia suala hilo chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa mbunge wa Muhambwe  na baadaye liliibuliwa tena mwaka 2002 na Thomas Ngawaiya aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini na likashughulikiwa na Kamati ya Katiba, Utawala na sheria chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Athumani Janguo akiwa mbunge wa Kisarawe.
Baadaye suala hilo lilirudishwa serikalini chini ya Tume ya Kurekebisha Sheria kati ya 2006 -2008. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti Profesa Ibrahimu Juma.
Viongozi wa Kikristo wamekuwa wakipinga kuwepo kwa Mahakama hiyo, huku Waislam wakiililia kwa kudai ni haki yao katika kushughulikia kesi zinazowahusu waumini wake ambao misingi yao ipo kwa muongozo wa Qur'an na Mafundisho ya Mtume Muhammad SAW.
Msimamo wa AG Masaju unaendana na ukweli kuwa yapo mataifa yenye waislam wachache lakini yana Mahakama hiyo ya Kadhi na kuwa wanachama wa OIC jambo jingine linalopingwa nchini na viongozi wa Kikristo na mambo yao yanaendelea bila ya hofu wala tatizo kama inavyoelezwa kama njia ya kukwamisha jambo hilo nchini.

Manchester United yaing'oa Cambridge Utd kwa kuinyuka 3-0

Mata finished off Di Maria's cross from six yards out to break the deadlock and put Manchester United ahead
Juan Mata akifunga bao la kuongoza la Manchester United
Wilson came off the bench to score Manchester United's third goal in the 73rd minute to finish off Cambridge United
James Wilson akifunga bao la tatu
Argentine defender Rojo doubled Manchester United's lead over Cambridge United in the 32nd minute at Old Trafford
Marcos Rojo akiiandikia Mashetani Wekundu bao la pili
Elliott and his Cambridge United team-mates react in despair after seeing his shot flick the outside of the post and go wide
Hayaaa! Tom Elliot akisikitika kwa kukosa bao la wazi
Manchester United's Argentine winger Angel di Maria tries to break down the Cambridge United defence
Angel di Maria akimtoka mchezaji wa Cambrigde United
WAKIWA kwenye kiwango bora kuliko mchezo uliopita na huku wakicheza kwa tahadhari kubwa, Manchester United wamefanikiwa kuichapa Cambridge United kwa mabao 3-0 na kutinga hatua ya Tano ya michuano ya Kombe la FA.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Manchester United waliolazimishwa suluhu bila kutarajiwa na timu hiyo ya Daraja la Pili katika mechi ya wiki iliyopita uwanja wa ugenini, walienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.
Kiungo Mshambuliaji Juan Mata alianza kuiandikia wenyeji bao katika dakika ya 25 akimalizia krosi pasi ya Angel di Maria kabla ya Marcos Rojo kuongeza la pili kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Robin van Persie katika dakika ya 32.
Wageni walikaribia kuwatungua Mashetani Wekundu baada ya 'kinda' Tom Elliott, kushindwa kufunga mara mbili akiwa peke yake na lango kutokana na makosa ya mabeki wa Manchester United.
Mtokea benchi James Wilson aliyempokea van Persie aliihakikisha Manchester United nafasi ya kusonga mbele kwa kufunga bao la tatu kwa mkwaju mkali wa mguu wa kushoto katika dakika ya 73 baada ya kunyezewa pasi murua na  Ander Herrera.
Kwa ushindi huo Manchester United sasa watavaana na timu ya Preston North End ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Sheffield United katika mechi nyingine ya marudiano ya michuano hiyo baada ya awali kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi ya timu hizo itachezwa Jumatatu ya Februari 16.
Katika pambano jingine la marudiano Sunderland ikiwa ugenini ilitakata kwa kuisasambua Fulham kwa mabao 3-1 na kutinga raundi ya Tano wakikaribiana na Bradford City katika mechi itakayochezwa Jumapili ya Februari 15. Katika mechi yao ya kwanza timu hizo zilitoka 0-0.
Timu ya Bradford City ndiyo iliyoing'oa Chelsea kwenye michuano hiyo katika raundi hiyo ya nne kwa kuilaza vinara hao wa Ligi Kuu ya England mabao 4-2 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stanford Bridge wiki iliyopita.

CAF yamfungia mwamuzi aliyewabeba wenyeji Afcon 2015

http://ww1.hdnux.com/photos/34/36/27/7464396/5/628x471.jpg
Refa Seechurn Rajindraparsad

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/RFZ6duPBZw4ebZ6b797g2A--/YXBwaWQ9eW5ld3M7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/fr_FR/Sports/Eurosport/1405900-30114704-640-360.jpg
Polisi wakimlinda mwamuzi Rajindraparsad asipewe kichapo na wachezaji wa Tunisia baada ya kutoa penati tata kwa wenyeji dakika za lala salama
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemsimamisha mwamuzi Seechurn Rajindraparsad aliyevurunda pambano la Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) kutakiwa kuomba msahama kwa vurugu zilizofanywa na wachezaji wa nchi hiyo.
Mwamuzi huyo kutoka Mauritius alitoa penati ya utata dakika za lala salama za pambano hilo na kuwapa wenyeji bao la kusawazisha lililofanya mchezo huo kuongezewa muda wa dakika 30 na Guinea ya Ikweta kushinda kwa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali.
Wachezaji wa Tunisia walionyeshwa kukerwa na maamuzi hayo kiasi cha askari Polisi kulazimika kumuokoa na kumlinda ili asidhuriwe.
Katika taarifa yake iliyotolewa juzi, CAF imetangaza kuondoa mwamuzi huyo kwa kuchezesha ovyo mechi hiyo na kusimamisha kwa muda wa miezi sita sambamba na kumuondoa kwenye orodha ya Caf ya waamuzi wa Daraja A kutokana na kikao cha Kamati ya waamuzi.
Mwamuzi huyo licha ya 'kubanyanga' mchezo huo ambao ulionekana wazi wenyeji wameondoshwa mashindanoni, huku TFT ikitakiwa kuomba radhi kwa vitendo vilivyofanywa na wachezaji wa timu yao ya taifa  siku ya mchezo huo.
TFT tayari imeshaadhibiwa kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wa timu yao ya taifa na maafisa wake, ingawa CAF kupitia kamati ya Waamuzi inakiri kwamba mwamuzi wa pambano hilo alivurunda kwa kuchezesha chini ya kiwango jambo ambalo CAF haipo tayari kuona madudu kama hayo katika michuano yake.

Bayern Munich wang'ang'aniwa nyumbani Bundesliga

http://i1.eurosport.com/2015/02/03/1408140-30159502-1600-900.jpg
Thomas Mullier akipambana dhidi ya wachezaji wa Schalke 04
http://b.smimg.net/15/06/640x480/bayern-munich-arjen-robben.jpg
Mfungaji wa bao la Bayern Munich, Arjen Robbin akishangilia
MABINGWA watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich wameshindwa kutamba nyumbani baada ya kung'ang'aniwa na Schalke 04 na kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mfululizo wa ligi hiyo nchini Ujerumani.
Bayern wakiwa kwenye uwanja wao wa Allianz Arena, walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya wageni wao ambao walionekana kudhamiria kuendeleza aibu kwa mabingwa hao ambao walikuwa wametoka kupokea kipigo chao cha kwanza katika ligi hiyo wakiwa ugenini dhidi ya Wolfsburg waliowachapa mabao 4-1.
Baada ya kumaliza dakika 45 za awali wakiwa nguvu sawa, wenyeji walianza kuandikisha bao la kuongoza dakika ya 67 kupitia kwa Arjen Robben akimalizia kazi nzuri ya Xabi Alonso.
Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika tano tu kwani Schalke walisawazisha kupitia kwa Benedikt Howedes na kuwafanya wenyeji waliocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wake tegemeo Jeremy Boateng kulimwa kadi nyekundu dakika ya 17 tu ya mchezao kuhaha kusaka bao la ushindi bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Bayern wameendelea kukalia kiti cha uongozi wa Bundesliga wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 19 huku wapinzani wao wakipanda hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 31.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa juzi, Borussia Monchengladbach walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Freiburg uliowapeleka hadi nafasi ya tatu wakifikisha pointi33, huku Hannover 96 na Mainz 05 wakishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 kama ilivyokuwa katika mchezo wa timu za Eintracht Frankfurt na 'wababe' wa Bayern Munich Wolfsburg

Ivory Coast iliyokamilika kuvaana na DR Congo leo Afcon

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/8/8a/Cheick_Ismael_Tiote_9030.JPG
Cheikh Tiote
http://4.bp.blogspot.com/-aPtQr6424F8/Ub7f4ODHjdI/AAAAAAAADKo/cHjPrwVwbEE/s1600/IMG_9994.JPG
Kikosi cha Ivory Coast kitakachokabuiliana na DR Congo leo kwenye nusu fainali ya kwanza ya AFCON 2015
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imemkaribisha kwa mikono miwili katika mazoezi ya timu hiyo mchezaji wake Cheick Tiote kabla timu hiyo leo haijashuka dimbani kucheza  mchezo wao wa nusu fainali wa Mataifa ya Afrika.
Ivory Cioast baada ya kuitoa  Tunisia katika hatua ya robo fainali, inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo makubwa kwa nchi barani Afrika.
Cheick Tiote huenda leo Jumatano akawemo katika kikosi cha Ivory Coast cha nusu fainali dhidi ya Jamhuri ya Watu wa Kongo.
Kiungo huyo mahiri wa Newcastle United hajapangwa katika kikosi cha kocha wake Herve Renard  tangu alipoichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho wakati ilipocheza na Mali katika mchezo wa  Januari 24 kutokaana na maumivu ya kifundo cha mguu.
Hatahivyo, kocha wa timu hiyo Renard ana matumaini makubwa kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, atarejea uwanjani na wanafuzu kwa fainali zao za sita ndani ya miaka sita katika mashindano hayo.
"Tiote alianza mazoezi mepesi na yumo katika orodha ya kikosi cha leo Jumatano kitakachoshuka dimbani.
"Kwa kweli ni vigumu kwake kuanza mchezo huo, lakini yumo katika kikosi hicho.
Ivory Coast wanaangalia kutwaa taji lao la kwanza la AFCON tangu mwaka 1992 huko Equatorial Guinea, huku kocha Renard akiwa na matumaini kibao ya kujaribu bahati ya kulitwaa taji hilo tena baada ya kufanikiwa kufanya hivyo alipokuwa akiifundisha Zanzibar mwaka 2012.
Kesho Alhamisi kutakuwa na nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Ghana na wenyeji Equatorial Guinea ambao watakuwa wakicheza mbele ya wapenzi wao.