STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 4, 2015

Bayern Munich wang'ang'aniwa nyumbani Bundesliga

http://i1.eurosport.com/2015/02/03/1408140-30159502-1600-900.jpg
Thomas Mullier akipambana dhidi ya wachezaji wa Schalke 04
http://b.smimg.net/15/06/640x480/bayern-munich-arjen-robben.jpg
Mfungaji wa bao la Bayern Munich, Arjen Robbin akishangilia
MABINGWA watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich wameshindwa kutamba nyumbani baada ya kung'ang'aniwa na Schalke 04 na kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mfululizo wa ligi hiyo nchini Ujerumani.
Bayern wakiwa kwenye uwanja wao wa Allianz Arena, walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya wageni wao ambao walionekana kudhamiria kuendeleza aibu kwa mabingwa hao ambao walikuwa wametoka kupokea kipigo chao cha kwanza katika ligi hiyo wakiwa ugenini dhidi ya Wolfsburg waliowachapa mabao 4-1.
Baada ya kumaliza dakika 45 za awali wakiwa nguvu sawa, wenyeji walianza kuandikisha bao la kuongoza dakika ya 67 kupitia kwa Arjen Robben akimalizia kazi nzuri ya Xabi Alonso.
Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika tano tu kwani Schalke walisawazisha kupitia kwa Benedikt Howedes na kuwafanya wenyeji waliocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wake tegemeo Jeremy Boateng kulimwa kadi nyekundu dakika ya 17 tu ya mchezao kuhaha kusaka bao la ushindi bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Bayern wameendelea kukalia kiti cha uongozi wa Bundesliga wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 19 huku wapinzani wao wakipanda hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 31.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa juzi, Borussia Monchengladbach walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Freiburg uliowapeleka hadi nafasi ya tatu wakifikisha pointi33, huku Hannover 96 na Mainz 05 wakishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 kama ilivyokuwa katika mchezo wa timu za Eintracht Frankfurt na 'wababe' wa Bayern Munich Wolfsburg

No comments:

Post a Comment