Wagosi wa Kaya, Coastal Union waliopania kuwatia maumivu vijana wa Jangwani leo Mkwakwani |
Yanga waliopa kuondoa 'gundu' Mkwakwani kwa kuinyoa Coastal Union |
Timu hizo zinakutana kwenye mchezo nhuo wa kiporo huku kila moja ikitoka kulazimishwa sare isiyo na mabao nyumbani katika mechi zao za mwishoni mwa wiki.
Yanga ilibanwa na Ndanda Fc kwenye uwanja wa Taifa, wakati Coastal ikiwa nyumbani ilishindwa kufurukuta kwa Mtibwa Sugar, hali inatyofanya pambano la leo kuwa kama vita ya kusaka pointi tatu kwa timu zote.
Coastal kupitia Msemaji wake, Oscar Assenga, amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kuwatoa nishai Yanga, wakati Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro akisema wameenda Tanga kuchukua pointi tatu kwa vile timu yao ni bora kuliko wapinzani wao.
Coastal inayonolewa na kocha James Nandwa kutoka Kenya itakuwa na kibarua kigumu kwa wapinzani wao licha ya kwamba kwa muda sasa Yanga haijaonja ushindi Mkwakwani dhidi ya Wagosi wa Kaya ama Mgambo JKT.
Mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilikuwa Novemba 12, 2012 iliposhinda 2-0.
Katibu Mkuu wa Coastal Kassim El Siagi alisema angetaka mashabiki wa soka kuthibitisha ipi timu ya soka la kweli la uwanjani na timu za magazetini ambao namna wanavyopambwa unaweza kusema ni Barcelona ilihali ni timu ya kawaida ionayoshindwa kuzifunga hata timu ndogo kama Ruvu Shooting na Ndanda FC.
Hata hivyo Yanga wameapa kufanya kweli leo baada ya kushuhudia safu yake ya ushambuliaji katika mechi tatu ilizocheza za Ligi Kuu ikifunga moja tu walipoilaza Polisi Moro.
Mashabiki wa Yanga pamoja na timu yao wapo mjini Tanga tangu majuzi kwa ajili ya pambano hilo ambalo litatoa taswira mpya ya msimamo wa Ligi Kuu timu mojawapo ikipata ushindi, Yanga ikiweza kurejea kileleni baada ya kutemeshwa muda mrefu na Mtibwa Sugar na baadaye Azam.
Kadhalika Coastal ikishinda inaweza kukwea hadi nafasi ya pili na kuwaengua Yanga waliopo katika nafasi hiyo kwa sasa wakiwa na pointi 19, mbili nyuma ya Azam wanaoongoza na pointi zao 21.
MSIMAMO LIGI KUU ULIVYO KWA SASA
P W D L F A GD Pts
01. Azam 11 06 03 02 15 08 07 21
02. Yanga 11 05 04 02 12 07 05 19
03. Mtibwa Sugar 11 04 06 01 13 07 06 18
04. Polisi Moro 13 04 06 03 10 09 01 18
05. JKT Ruvu 13 05 03 05 13 13 00 18
06. Ruvu Shooting13 05 03 05 09 10 -1 18
07. Coastal Union 12 04 05 03 10 08 02 17
08. Simba 12 03 07 02 13 11 02 16
09. Mbeya City 12 04 03 05 08 10 -2 15
10. Kagera Sugar 13 03 06 04 10 11 -1 15
11. Mgambo JKT 11 04 02 05 06 10 -4 14
12. Ndanda Fc 13 04 02 07 12 17 -5 14
13. Stand Utd 13 02 05 06 08 16 -8 11
14. Prisons 12 01 07 04 09 11 -2 10
No comments:
Post a Comment