STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 4, 2015

Manchester United yaing'oa Cambridge Utd kwa kuinyuka 3-0

Mata finished off Di Maria's cross from six yards out to break the deadlock and put Manchester United ahead
Juan Mata akifunga bao la kuongoza la Manchester United
Wilson came off the bench to score Manchester United's third goal in the 73rd minute to finish off Cambridge United
James Wilson akifunga bao la tatu
Argentine defender Rojo doubled Manchester United's lead over Cambridge United in the 32nd minute at Old Trafford
Marcos Rojo akiiandikia Mashetani Wekundu bao la pili
Elliott and his Cambridge United team-mates react in despair after seeing his shot flick the outside of the post and go wide
Hayaaa! Tom Elliot akisikitika kwa kukosa bao la wazi
Manchester United's Argentine winger Angel di Maria tries to break down the Cambridge United defence
Angel di Maria akimtoka mchezaji wa Cambrigde United
WAKIWA kwenye kiwango bora kuliko mchezo uliopita na huku wakicheza kwa tahadhari kubwa, Manchester United wamefanikiwa kuichapa Cambridge United kwa mabao 3-0 na kutinga hatua ya Tano ya michuano ya Kombe la FA.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Manchester United waliolazimishwa suluhu bila kutarajiwa na timu hiyo ya Daraja la Pili katika mechi ya wiki iliyopita uwanja wa ugenini, walienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.
Kiungo Mshambuliaji Juan Mata alianza kuiandikia wenyeji bao katika dakika ya 25 akimalizia krosi pasi ya Angel di Maria kabla ya Marcos Rojo kuongeza la pili kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Robin van Persie katika dakika ya 32.
Wageni walikaribia kuwatungua Mashetani Wekundu baada ya 'kinda' Tom Elliott, kushindwa kufunga mara mbili akiwa peke yake na lango kutokana na makosa ya mabeki wa Manchester United.
Mtokea benchi James Wilson aliyempokea van Persie aliihakikisha Manchester United nafasi ya kusonga mbele kwa kufunga bao la tatu kwa mkwaju mkali wa mguu wa kushoto katika dakika ya 73 baada ya kunyezewa pasi murua na  Ander Herrera.
Kwa ushindi huo Manchester United sasa watavaana na timu ya Preston North End ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Sheffield United katika mechi nyingine ya marudiano ya michuano hiyo baada ya awali kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi ya timu hizo itachezwa Jumatatu ya Februari 16.
Katika pambano jingine la marudiano Sunderland ikiwa ugenini ilitakata kwa kuisasambua Fulham kwa mabao 3-1 na kutinga raundi ya Tano wakikaribiana na Bradford City katika mechi itakayochezwa Jumapili ya Februari 15. Katika mechi yao ya kwanza timu hizo zilitoka 0-0.
Timu ya Bradford City ndiyo iliyoing'oa Chelsea kwenye michuano hiyo katika raundi hiyo ya nne kwa kuilaza vinara hao wa Ligi Kuu ya England mabao 4-2 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stanford Bridge wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment