STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 4, 2015

Ivory Coast iliyokamilika kuvaana na DR Congo leo Afcon

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/8/8a/Cheick_Ismael_Tiote_9030.JPG
Cheikh Tiote
http://4.bp.blogspot.com/-aPtQr6424F8/Ub7f4ODHjdI/AAAAAAAADKo/cHjPrwVwbEE/s1600/IMG_9994.JPG
Kikosi cha Ivory Coast kitakachokabuiliana na DR Congo leo kwenye nusu fainali ya kwanza ya AFCON 2015
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imemkaribisha kwa mikono miwili katika mazoezi ya timu hiyo mchezaji wake Cheick Tiote kabla timu hiyo leo haijashuka dimbani kucheza  mchezo wao wa nusu fainali wa Mataifa ya Afrika.
Ivory Cioast baada ya kuitoa  Tunisia katika hatua ya robo fainali, inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo makubwa kwa nchi barani Afrika.
Cheick Tiote huenda leo Jumatano akawemo katika kikosi cha Ivory Coast cha nusu fainali dhidi ya Jamhuri ya Watu wa Kongo.
Kiungo huyo mahiri wa Newcastle United hajapangwa katika kikosi cha kocha wake Herve Renard  tangu alipoichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho wakati ilipocheza na Mali katika mchezo wa  Januari 24 kutokaana na maumivu ya kifundo cha mguu.
Hatahivyo, kocha wa timu hiyo Renard ana matumaini makubwa kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, atarejea uwanjani na wanafuzu kwa fainali zao za sita ndani ya miaka sita katika mashindano hayo.
"Tiote alianza mazoezi mepesi na yumo katika orodha ya kikosi cha leo Jumatano kitakachoshuka dimbani.
"Kwa kweli ni vigumu kwake kuanza mchezo huo, lakini yumo katika kikosi hicho.
Ivory Coast wanaangalia kutwaa taji lao la kwanza la AFCON tangu mwaka 1992 huko Equatorial Guinea, huku kocha Renard akiwa na matumaini kibao ya kujaribu bahati ya kulitwaa taji hilo tena baada ya kufanikiwa kufanya hivyo alipokuwa akiifundisha Zanzibar mwaka 2012.
Kesho Alhamisi kutakuwa na nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Ghana na wenyeji Equatorial Guinea ambao watakuwa wakicheza mbele ya wapenzi wao.

No comments:

Post a Comment