STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 3, 2015

Kocha Redknapp abwaga manyanga QPR

http://static.guim.co.uk/sys-images/Football/Pix/pictures/2012/11/24/1353767357535/Harry-Redknapp-new-QPR-ma-008.jpg
Kocha Harry Redknapp aliyebwaga manyanga QPR
KOCHA wa timu ya Ligi Kuu ya England ya  Queen Park Rangers, Harry Redknapp ametangaza kujiuzulu kuwa kocha wa timu hiyo.
Redknapp huyo  mwenye umri wa miaka 67 amedumu na klabu hiyo kwa takribani miaka miwili ameamua kuachana na klabu hiyo kwa hiari yake baada ya kushindwa kuopa mafanikio.
Taarifa kutoka kwa Tony Fernandes inasomeka hivi; "Tunashukuru kwa kila alichofanya Redknapp hapa klabuni wakati wote wa utawala wake kama kocha."
Taarifa hiyo ya kujiuzulu kwa kocha huyo haijaeleza wazi chanzo cha kujiuzulu kwa kocha huyo ambaye pia aliwahi kuifundisha Tottenham Hotspurs na kuipa mafanikio akisi cha kupigiwa debe kuchukua mikoba ya kuifundisha timu ya taifa ya England.
Hata hivyo inaelezwa tatizo la kiafya alilonalo kocha huyo ndilo lililomfanya achukue uamuzi huo wa kutekma kibarua hicho.
Redknapp amekunuliwa akisema kuwa maumivu ya magoti yanayomsumbua kwa muda mrefu kiasi cha kuweza kusimama kwa muda mrefu ndicho sababu ya kuacha kibarua hicho na kumpigia simu bosi wake Tony Fernandes ili atafute mtu wa kuisimamia timu hiyo iliyopo nafasi ya pili mkiani mwa msimamo wa Ligi.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Viporo FA: Manchester Utd kutoka vipi leo?! Liverpool kesho

http://mufclatest.com/wp-content/uploads/2015/02/Cambridge-United-FA-Cup-Replay-750x360.png
http://i3.mirror.co.uk/incoming/article5032437.ece/alternates/s615/Cambridge-United-v-Manchester-United-FA-Cup-Fourth-Round.jpg
Man United walivyohenyaka mechi ya kwanza kwa Cambridge United, leo watatokaje
BAADA ya kushukizwa ugenini kwa kulazimishwa suluhu isiyo na magoli dhidi ya timu ya daraja la pili ya Cambridge United, leo watakuwa uwanja wa nyumbani wa Old Trafford kurudiana na timu hiyo katika mechi ya Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
Katika michuano ya kombe hilo, leo kutakuwa na mechi nyingine mbili zitakazowakutanisha timu za Fulham  na Sunderland ambazo zilishindwa kutambiana katika mechi yao ya kwanza kwa kutoka sare ya 0-0, huku timu zilizofungana bao 1-1 katika mechi iliyopita Sheffield United na  Preston North End nao wataonyeshana kazi.
Bolton Wanderers waliowasimamisha Livepool nyumbani kwao Anfield watakuwa wenyeji wa Liverpool katika mechi nyingine itakaypogwa kesho kukamilisha mechi za viporo vya michuano hiyo kabla ya kuanza mechi za raundi ya tano.
Manchester Utd ambayo imetoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 nyumbani katika Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya vibonde wa ligi hiyo Leicester City italazimika kugangamala ili wasije wakaenda na maji kama ilivyowakuta timu za Manchester City na Chelsea waliotolewa nishai na timu za madaraja ya chini katika michuano hiyo.
Kocha Luis Van Gaal anatarajiwa kuchezesha kikosi kamili katika pambano hilo ili kuweza kuvuka hatua hiyo na kujiweka katika nafssi nzuri ya kunyakua angalau kombe moja kati ya mawili ambayo wana nafasi ya kuyatwaa wakigangamala lingine likiwa la Ligi Kuu japo ana nafasi finyu.
Mabingwa hao wa zamani na wenye historia kubwa katika FA kwa kunyakua mara nyingi, imeshaondoshwa kwenye Kombe la Ligi (Capital One) na pia haishiriki michuano yoyote ya kikmataifa baada ya msimu uliopita kuwa na wakati mgumu chini ya kocha David Moyes.

HII NDIYO NGOMA MPYA YA AY- ZIGO


Chelsea nouma, yafanya kufuru usajili dirisha dogo

http://cdn.caughtoffside.com/wp-content/uploads/2015/02/Chelsea-Juan-Cuadrado.jpg
Kifaa kipya kilichotua Chelsea
DIRISHA dogo la usajili nchini Uingereza limefungwa usiku wa jana huku klabu ya Chelsea ikiwa ndiyo timu inayoongoza kwa kutumia fungu kubwa la fedha katika usajili huo kwa kumchukua winga wa kimataifa wa Colombia Juan Cuadrado kwa kitita cha paundi milioni 23.3.
Kwa ujumla klabu za Ligi Kuu zimetumia kiasi cha paundi milioni 130 katika usajili huu hivyo kufikia kiwango kama walichotumia mwaka jana.
Klabu ya Crystal Palace ndio iliyokuwa na harakati nyingi katika siku ya mwisho ya usajili kwa kuwachukua wachezaji wanne akiwemo Wilfried Zaha.
Klabu ya Hull City ndio iliyofunga dirisha hilo kwa kutangaza usajili wa kumchukua mshambuliaji wa Lokomotiv Moscow Dame N’Doye katika muda wa mwisho.
Jumla ya wachezaji 13 wamesajiliwa katika siku ya mwisho ya usajili huku 35 zaidi wakisajiliwa katika kipindi chote toka dirisha lilipofunguliwa Januari mosi mwaka huu.

Vita vya Nusu Fainali Afcon kuanza kesho, DRC, Ivory Coast balaa!

http://2.bp.blogspot.com/-SB-d541z6sc/VL4AkhGjdBI/AAAAAAAAxDQ/t-i41NY82rw/s1600/ivory-coast%2Bnational%2Bteam%2B2015.jpg
Kikosi cha Tembo wa Afrika, Ivory Coast watakaoanza kuvaana na DR Congo kesho mjini Bata
Kikosi cha DR Congo
http://sportsworldghana.com/wp-content/uploads/2014/12/ghana-black-stars-2.jpg
Kikosi cha Black Stars kitakachovaana na wenyeji Guinea ya Ikweta
http://en.starafrica.com/football/files/2013/03/615_340_SA_EQUATORIAL-GUINEA.jpg
Wenyeji Guinea ya Ikweta kuendeleza maajabu yao AFCON 2015
MBIVU na mbichi za timu zipi zitakazotinga Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) itafahamika kesho wakati mechi za Nusu Fainali zitakapochezwa.
Pazia la hatua hiyo litaanza kesho kwa mchezo wa kukata na mundu kati ya Ivory Coast iliyowaduwaza Algeria dhidi ya wapiganaji wa DR Congo.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Bata, mjini Bata.
DR Congo ambayo haikuwa ikipewa nafasi ya kufika kokote kwenye michuano hiyo ilipenya hatua hiyo baada ya kuwatoa nishai watani zao wa jadi Congo Brazzaville kwa kuwanyuka mabao 4-2.
Vijana hao wa Kabila walitoka nyuma ya mabao 2-0 na kuwaduwaza wakongo wenzao ambao hata hivyo licha ya kuondoka wameweka rekodi baada ya miaka mingi.
Wakongo hao watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Tembo wa Ivory Coast ambao waliwanyuka Algeria mabao 3-1 na kutinga hatua hiyo bila kutarajiwa.
Nusu fainali ya pili itakuwa keshokutwa kwenye uwanja wa Malabo, kwa pambano kali kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya Black Stars ya Ghana ambayo waliwachapa Guinea mabao 3-0 katika mechi ya robo fainali.
Wenyeji ambao hakuna aliyetarajia kama ingefika hatua hiyo kutokana na maandalizi yake, iliwatoa nishai kitatanishi Tunisia baada ya 'kupewa' penati dakika za lala salama kabla ya kupata bao la ushindi dakika ya nyongeza zilizowafanya waweke rekodi.
Hata hivyo hakuna anayetarajia Guinea ya Ikweta ifanye maajabu mengine mbele ya Ghana ambao kikosi chake kimekuwa kikizid kuimarika tangu walipoanza michuano hiyo ya kipigo toka Senegal.
Mashabiki wa soka wana hamu kubwa ya kujua ni timu zipi zitakazofuzu kwa Fainali itakayopigwa Jumapili ili kupata bingwa mpya wa Afrika.
Taji la michuano hiyo ya mwaka huu halina mwenyewe baada ya waliokuwa watetezi, Nigeria kushindwa kupata nafasi ya kwenda Guinea ya Ikweta baada ya kung'oka kwenye mechi za makundi za mchujo.
Timu mbili kati ya tano zilizokuwa zikipigiwa chapuo na kutajwa huenda zingewarithi Nigeria ndizo zilizobakia kwenye michuano hiyo ambazo ni Ghana na Ivory Coast, huku Cameroon, Afrika Kusini na Algeria zikiwa zimesharejea makwao mapema.

Hatem Ben Arfa kustaafu soka mapema?!

http://talksport.com/sites/default/files/tscouk_old_image/benarfa_2.jpg
Hatem Ben Arfa anayedaiwa huenda akastaafu?
WAKILI wa Hatem Ben Arfa amedokeza kiungo huyo anaweza kustaafu soka baada ya Ligi ya Soka ya Ufaransa-LFP kumfungia kucheza mechi za mashindano na klabu ya Nice.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Nice akitokea Newcastle United mapema mwezi huu baada ya mkopo wake katika klabu ya Hull City kusitishwa.
Kwa mujibu wa taratibu za Shirikisho la Soa Dunia-FIFA, wacheza wanaweza kuruhusiwa kucheza mechi za mashindano katika vilabu viwili pekee kwa msimu.
Wakili Jean-Jacques Bertrand amesema ni wazi kuwa uwepo wa Ben Arfa katika timu hiyo utamalizika leo na kuhofu kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa anafikiria kustaafu.
Ben Arfa aliifungiwa Newcastle katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Readings kwa timu za vijana chini ya umri wa miaka 25 Agosti mwaka jana kabla ya kwenda Hull kwa mkopo ambako nako alicheza mechi tisa.

West Ham Utd hatarini kuenguliwa FA Cup

http://www.africatopsports.com/wp-content/uploads/2014/10/diafra-sakho.jpg
Diafra Sakho
KLABU ya West Ham United inakabiliwa na adhabu ya kuenguliwa katika michuano ya Kombe la FA kama Shirikisho la Soka Duniani-FIFA litawakuta na kosa kwa kumtumia mshambuliaji Diafra Sakho.
Sakho mwenye umri wa miaka 25 alijitoa katika kikosi cha Senegal kilichoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kutokana na maumivu ya mgongo lakini aliifungia West Ham bao siku 18 baadae katika ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Bristol City.
Sheria za FIFA hazimruhusu mchezaji kuichezea klabu yake kama anatakiwa kuwa na majukumu ya kimataifa. FIFA tayari imeshaanza kuchunguza suala hilo huku West Ham wenyewe wakikanusha kufanya lolote baya kwa kumtumia mchezaji huyo.
Kama West Ham watakutwa na kosa, FIFA inaweza kuliamuru Shirikisho la Soka la Uingereza-FA kubadilisha matokeo waliyopata dhidi ya Bristol City.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
KLABU ya West Ham United inaweza kukabiliwa na adhabu ya kuenguliwa katika michuano ya Kombe la FA kama Shirikisho la Soka Duniani-FIFA litawakuta na kosa kwa kumtumia mshambuliaji Diafra Sakho. Sakho mwenye umri wa miaka 25 alijitoa katika kikosi cha Senegal kilichoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kutokana na maumivu ya mgongo lakini aliifungia West Ham bao siku 18 baadae katika ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Bristol City. Sheria za FIFA hazimruhusu mchezaji kuichezea klabu yake kama anatakiwa kuwa na majukumu ya kimataifa. FIFA tayari imeshaanza kuchunguza suala hilo huku West Ham wenyewe wakikanusha kufanya lolote baya kwa kumtumia mchezaji huyo. Kama West Ham watakutwa na kosa, FIFA inaweza kuliamuru Shirikisho la Soka la Uingereza-FA kubadilis

Hii ndiyo bei halisi atakayouzwa Cristiano Ronaldo

http://www.independent.co.uk/incoming/article9760507.ece/binary/original/cristiano-ronaldo-5.jpg
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo
CRISTIANO Ronaldo atauzwa kwa kiasi cha pauni Milioni 300 endapo klabu ya Real Madrid itaamua hata kesho kumuchia mchezaji huyo kuondoka.
Hayo yalisemwa na wakala wa mchezaji huyo nyota wa Ureno alipozungumza leo na BBC Sport.
Wakala huyo Jorge Mendes alisema nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno ni mchezaji bora wa muda wote.
"Ni mchezaji bora wa muda wote duniani. Kamwe huwezi kumfananisha na mchezaji mwingine yeyote, alisema Mendes alipozungumza na muhariri wa michezo Dan Roan.
Ronaldo, mwenye umri wa miaka 29, mwezi uliopita alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mchezaji bora wa dunia, akimbwaga Lionel Messi wa Barcelona katika tuzo hiyo.
Alipoulizwa mchezaji huyo ana thamani kiasi gani, Mendes alisema: 
"Cristano Ronaldo? Bilioni moja. Anakaribia Bilioni moja, hivyo ni bilioni moja. Kwa kweli haiwezekani kumpata mwingine anayefanana nay eye.
"Endapo kwa sabbau zozote zile klabu itaamua kumuuza hata kesho kwa Milioni 300, mtu atalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa. "
Hata hivyo, Mendes alisisitiza kuwa raia huyo mwenzake wa Ureno ambaye alinunuliwa na Real Madrid kwa rekodi ya dunia ya ada ya dola za Marekani Milioni 80 mwaka 2009, ataendelea kubaki Bernabeu, licha ya mapenzi yake" kwa klabu yake ya zaman ya Manchester United.
Alipoulizwa kama atamalizia soka lake Real Madrid, Mendes alisema "na uhakika". "Hataondoka Real Madrid," aliongeza.
Mendes, aliyeripotiwa kuwa alipata zaidi na pauni bilioni 1 kwa ajili ya uhamisho tu, akielezewa kuwa ni mmoja wa watu wenye nguvu sana katika mchezo huo.
"Watu wana mtazamo tofauti kuhusu mawakala. Kuwa wakala kuna maana tofauti. Mimi ni mtu wa kawaida kabisa. Ninafanya kazi kwa bidii kila siku. Nina malengo na kusema ukweli ninatenda haki na hilo ndio muhimu zaidi.
Alielezea kuwa soka ni mchezo muhimu sana duniani na alitetea mishahara ya wachezaji, akisema wanastahili kiasi kikubwa kama inawezekana".
Mendes alifananisha kufanyakazi na wachezaji kwa mikataba ni sawa na familia.
"Ni kama vile unavyozungumza na mtoto wako, au familia yako wakati wote unajaribu kutafuta njia bora ya kuwasaidia."
Mendes, DJ wazamani na mmiliki wa klabu ya usiku, pia ni wakala wa Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari, Radamel Falcao, Angel Di Maria, James Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa.

TFF kusaka mdhamini Ligi Daraja la Kwanza

http://api.ning.com/files/XCoElX7q3j2IeT5tiuUefPUOAr*u*C4UA*eK*naDvxjwjW3u89dAVaxJeE-HBCAXGvMt6yoAQJAritE0jIquj2X1*yXj0FNz/tff.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko mbioni kupata mdhamini wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Tunatarajia mdhamini huyo atakuwa tayari kwa ajili ya msimu wa 2015/2016.
Ligi Daraja la Kwanza inashirikisha timu 24 zinazocheza katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Timu zinazocheza FDL msimu huu ni African Lyon (Dar es Salaam), African Sports (Tanga), Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Faso (Morogoro), Friends Rangers (Dar es Salaam), Geita Gold (Geita), Green Warriors (Dar es Salaam), JKT Kanembwa (Kigoma), JKT Mlale (Ruvuma) na JKT Oljoro (Arusha).
Nyingine ni Kimondo (Mbeya), Kinondoni Municipal Council (Dar es Salaam), Kurugenzi (Iringa), Lipuli (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers (Tabora), Toto Africans (Mwanza), na Villa Squad (Dar es Salaam).

Yanga yafanya kufuru yatenga fedha Ebola Cup

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/SAM_1702.jpg
Mwwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji ametenga kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya michuano ya Ebola  Cup itakayoshirikisha timu 108 za Afrika.
Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwa na Yanga pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Jonas Tibohora  alisema hatua za kuanza michuano hizo zipo kwenye hatua nzuri.
Alisema michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya  kuchangisha fedha  zitakazowasaidia waafrika walioathirika na ugonjwa wa Ebola.
Alisema michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Soka Afrika (CAF), na kwamba kwa sasa kamati ya michuano hiyo yenye wajumbe mchanganyiko kutoka nchi wanachama wa CAF itakaa na kupanga tarehe ya michuano hiyo.
Alisema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu kati ya nne na saba.
Alisema michuano hiyo itashirikisha timu zote kutoka Afrika ambazo ni mwanachama wa CAF ambapo kila nchi itatoa timu mbili na michuano itachezwa nyumbani na ugenini.
Alisema  kila timu zitachangia kiasi cha dola 100,000 kama ada ya ushiriki ambazo zitaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa kusaidia waathirika hao.
"Mpango huu yatari umepitishwa na kinachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya michuano ambapo kamati ya mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti wake Machache Shipanda kutoka Zambia itakutana na kutoa ratiba,"alisema Tibohora.
Alisema pia mpango huo umeungwa mkona na umoja wa Afrika (AU) ambao watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa manufaa makubwa.


HUU NDIYO USAJILI WA DIRISHA DOGO ENGLAND

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/01/28/252596E800000578-2930164-Gabriel_Paulista_poses_with_an_Arsenal_shirt_as_the_club_unveil_-a-46_1422466068639.jpg
Paulista aliyenyakuliwa na Arsenal

http://resources2.news.com.au/images/2015/01/27/1227198/061530-6ca4ddec-a5bb-11e4-a11e-9d15a37a8504.jpg
Huyu kasajiliwa Chelsea
http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/media/motion/ESPNi/2015/0107/int_150107_FC_VALDES_united_DISC/int_150107_FC_VALDES_united_DISC.jpg&w=738&site=espnfc
Kipa Victor Valdes aliyetua Manchester United
Wolfsburg and Chelsea have agreed terms over £24million switch for Andre Schurrle
Andre Schurrle aliyeondoka Chelsea kutua Wolfsburg
JANA ilikuwa siku ya mwisho wa dirisha dogo la usajili barani Ulaya hususani katika nchi ya England na baadhi ya timu zimechangamsha za kutosha kuimarisha vikosi vyao, japo safari hii haikusisimua kama katika dirisha kubwa au dogo la msimu uliopoita.
Klabu kubwa kama Arsenal iliwanyakua kiungo mkabaji kinda wa miaka 17,  Krystian Bielik na beki wa kati, Gabriel Paulista, wakati Manchester United ilimsajili kipa Victor Valdes, huku Sunderland ikimnyakua Jermain Defoe.
Liverpool haijafanya usajili wowote wa dirisha dogo, huku West Brom yamnyakua Callum McManaman kutoka WiganYaya Sanogo ajiunga na Crystal Palace
Chini ni usajili kamili wa klabu 20 za Ligi Kuu ya England kujua walioingia na kutoka;
ARSENAL
WALIOSAJILIWA

Gabriel Paulista (Villarreal, £11.2m)
Krystian Bielik (Legia Warsaw, £2.5m) 
WALIOONDOKA
Benik Afobe (Wolves, ada haikutajwa)
Lukas Podolski (Inter Milan, mkopo)
Yaya Sanogo (Crystal Palace, mkopo)
Joel Campbell (Villarreal, mkopo) 

ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA

Carles Gil (Valencia, £3.25m)
Scott Sinclair (Manchester City, mkopo)
WALIOONDOKA
Darren Bent (Derby, mkopo)
Gary Gardner (Nottingham Forest, mkopo)
Chris Herd (Wigan, mkopo)
Callum Robinson (Preston, mkopo)

BURNLEY
WAlIOSAJILIWA

Michael Keane (Manchester United, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Hakuna

CHELSEA
WALIOSAJILIWA

Juan Cuadrado (Fiorentina, £27m)
WALIOONDOKA
Andre Schurrle (Wolfsburg, £24m)
Ryan Bertrand (Southampton, £10m)
Mark Schwarzer (Leicester, huru)
Thomas Kalas (Middlesbrough, mkopo)
John Swift (Swindon, mkopo)
Lewis Baker (Sheffield Wednesday, mkopo)
Marko Marin (Anderlecht, mkopo)
Mohamed Salah (Fiorentina, mkopo)

CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA

Wilfried Zaha (Manchester United £6m)
Jordon Mutch (QPR, £5.75m)
Lee Chung-yong (Bolton, ada haikutajwa)
Keshi Anderson (Barton Rovers, £35,000)
Shola Ameobi (Gaziantep, huru)
Pape Souare (Lille, ada haikutajwa)
Yaya Sanogo (Arsenal, mkopo)
WALIOONDOKA
Stuart O'Keefe (Cardiff, ada haikutajwa)
Alex Wynter (Colchester, ada haikutajwa)
Zeki Fryers (Rotherham, mkopo)
Lewis Price (Crawley, mkopo)
Jake Gray (Cheltenham, mkopo) 
Barry Bannan (Bolton, mkopo)
Jimmy Kebe (huru)

EVERTON
WALIOSAJILIWA

Aaron Lennon (Tottenham, mkopo)
WALIOONDOKA
Samuel Eto'o (Sampdoria, huru)
Chris Long (Brentford, mkopo) 
Conor McAleny (Cardiff, mkopo)

HULL CITY
WALIOSAJILIWA

Dame N'Doye (Lokomotov Moscow, £3m)
WALIOONDOKA
Tom Ince (Derby County, mkopo)

LEICESTER CITY
WALIOSAJILIWA

Andrej Kramaric (Rijeka, £9.5m)
Mark Schwarzer (Chelsea, huru)
Robert Huth (Stoke City, mkopo)
WALIOONDOKA
Tom Hopper (Scunthorpe, mkopo)

LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA

Hakuna
WALIOONDOKA
Oussama Assaidi (Al Ahli, £4.7m)
Suso (AC Milan, £1m) 

MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
 
Wilfried Bony (Swansea, £28m)
WALIOONDOKA
Matija Nastasic (Schalke, mkopo)
Scott Sinclair (Aston Villa, mkopo) 

MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA

Victor Valdes ( huru)
Sadiq El Fitouri (Salford City, huru)
Andy Kellett (Bolton, mkopo)
WALIOONDOKA
Wilfried Zaha (Manchester United, £6m)
Michael Keane (Burnley, £3m)
Darren Fletcher (West Brom, huru)
Will Keane (Sheffield Wednesday, mkopo)
Ben Amos (Bolton, mkopo)
Jesse Lingard (Derby County, mkopo)

NEWCASTLE UNITED
WALIOSAJILIWA

Hakuna
WALIOONDOKA
Mapou Yanga-Mbiwa (Roma, £5.2m)
Hatem Ben Arfa (huru)
Gael Bigirimana (Rangers, mkopo)
Haris Vuckic (Rangers, mkopo)
Shane Ferguson (Rangers, mkopo)
Davide Santon (Inter Milan, mkopo)

QUEENS PARK RANGERS
WALIOSAJILIWA
 
Mauro Zarate (West Ham, mkopo)
Ryan Manning (Galway United, huru)
WALIOONDOKA
Jordon Mutch (Crystal Palace, £5.75m)
Bruno Andrade (Stevenage, mkopo)

SOUTHAMPTON
WALIOSAJILIWA

Ryan Bertrand (Chelsea, £10m)
Eljero Elia (Werder Bremen, mkopo)
Filip Djuricic (Benfica, mkopo)
WALIOONDOKA
Jack Cork (Swansea, £3m)
Jos Hooiveld (Millwall, mkopo)
Artur Boruc (Bournemouth, mkopo)

STOKE CITY
WALIOSAJILIWA

Philipp Wollscheid (Bayer Leverkusen, mkopo)
WALIOONDOKA
Ryan Shotton (Derby, ada haikutajwa)
Maurice Edu (Philadelphia Union, ada haikutajwa)
Robert Huth (Leicester City, mkopo)

SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA

Jermain Defoe (Toronto, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Jozy Altidore (Toronto, ada haikutajwa)
Mikael Mandron (Shrewsbury, mkopo)
Charis Mavrias (Panathinaikos, mkopo)
Cabral (huru)

SWANSEA CITY
WALIOSAJILIWA
 
Kyle Naughton (Tottenham, £5m)
Jack Cork (Southampton, £3m)
Matt Grimes (Exeter City, £1.75m)
Nelson Oliveira (Benfica, mkopo) 
WALIOONDOKA
Wilfried Bony (Manchester City, £28m)
Rory Donnelly (Tranmere, mkopo)
Jazz Richards (Fulham, mkopo)

TOTTENHAM HOTSPUR 
WALIOSAJILIWA

Dele Alli (MK Dons, £5m)
WALIOONDOKA
Kyle Naughton (Swansea, £5m)
Aaron Lennon (Everton, mkopo)
Milos Veljkovic (Charlton, mkopo)
Benoit Assou-Ekotto (huru)
Dele Alli (MK Dons, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA 

Callum McManaman (Wigan, £4.75m)
Darren Fletcher (Manchester United, huru)
WALIOONDOKA
Luke Daniels (Scunthorpe, ada haikutajwa)

WEST HAM UNITED
WALIOSAJILIWA

Doneil Henry (Apollon Limassol, ada haikutajwa)
WALIOONDOKA
Mauro Zarate (QPR, mkopo)
Ricardo Vaz Te (huru)


Wateja wa Airtel kuzoa magari kila siku kupitia Yatosha

Sehemu ya magari yatakayoshindaniwa  na wateja wa Airtel
KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema;
"Promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. Nia yetu kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi"Aliongeza Nyakundi.

Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwezi. Hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku.

Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  Tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”, aliongeza  Mallya.

Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au  kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima.

Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake.