STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 3, 2015

Vita vya Nusu Fainali Afcon kuanza kesho, DRC, Ivory Coast balaa!

http://2.bp.blogspot.com/-SB-d541z6sc/VL4AkhGjdBI/AAAAAAAAxDQ/t-i41NY82rw/s1600/ivory-coast%2Bnational%2Bteam%2B2015.jpg
Kikosi cha Tembo wa Afrika, Ivory Coast watakaoanza kuvaana na DR Congo kesho mjini Bata
Kikosi cha DR Congo
http://sportsworldghana.com/wp-content/uploads/2014/12/ghana-black-stars-2.jpg
Kikosi cha Black Stars kitakachovaana na wenyeji Guinea ya Ikweta
http://en.starafrica.com/football/files/2013/03/615_340_SA_EQUATORIAL-GUINEA.jpg
Wenyeji Guinea ya Ikweta kuendeleza maajabu yao AFCON 2015
MBIVU na mbichi za timu zipi zitakazotinga Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) itafahamika kesho wakati mechi za Nusu Fainali zitakapochezwa.
Pazia la hatua hiyo litaanza kesho kwa mchezo wa kukata na mundu kati ya Ivory Coast iliyowaduwaza Algeria dhidi ya wapiganaji wa DR Congo.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Bata, mjini Bata.
DR Congo ambayo haikuwa ikipewa nafasi ya kufika kokote kwenye michuano hiyo ilipenya hatua hiyo baada ya kuwatoa nishai watani zao wa jadi Congo Brazzaville kwa kuwanyuka mabao 4-2.
Vijana hao wa Kabila walitoka nyuma ya mabao 2-0 na kuwaduwaza wakongo wenzao ambao hata hivyo licha ya kuondoka wameweka rekodi baada ya miaka mingi.
Wakongo hao watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Tembo wa Ivory Coast ambao waliwanyuka Algeria mabao 3-1 na kutinga hatua hiyo bila kutarajiwa.
Nusu fainali ya pili itakuwa keshokutwa kwenye uwanja wa Malabo, kwa pambano kali kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya Black Stars ya Ghana ambayo waliwachapa Guinea mabao 3-0 katika mechi ya robo fainali.
Wenyeji ambao hakuna aliyetarajia kama ingefika hatua hiyo kutokana na maandalizi yake, iliwatoa nishai kitatanishi Tunisia baada ya 'kupewa' penati dakika za lala salama kabla ya kupata bao la ushindi dakika ya nyongeza zilizowafanya waweke rekodi.
Hata hivyo hakuna anayetarajia Guinea ya Ikweta ifanye maajabu mengine mbele ya Ghana ambao kikosi chake kimekuwa kikizid kuimarika tangu walipoanza michuano hiyo ya kipigo toka Senegal.
Mashabiki wa soka wana hamu kubwa ya kujua ni timu zipi zitakazofuzu kwa Fainali itakayopigwa Jumapili ili kupata bingwa mpya wa Afrika.
Taji la michuano hiyo ya mwaka huu halina mwenyewe baada ya waliokuwa watetezi, Nigeria kushindwa kupata nafasi ya kwenda Guinea ya Ikweta baada ya kung'oka kwenye mechi za makundi za mchujo.
Timu mbili kati ya tano zilizokuwa zikipigiwa chapuo na kutajwa huenda zingewarithi Nigeria ndizo zilizobakia kwenye michuano hiyo ambazo ni Ghana na Ivory Coast, huku Cameroon, Afrika Kusini na Algeria zikiwa zimesharejea makwao mapema.

No comments:

Post a Comment