Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo |
CRISTIANO Ronaldo atauzwa kwa kiasi cha pauni Milioni 300 endapo klabu ya Real Madrid itaamua hata kesho kumuchia
mchezaji huyo kuondoka.
Hayo yalisemwa na wakala wa
mchezaji huyo nyota wa Ureno alipozungumza leo na BBC Sport.
Wakala huyo Jorge Mendes alisema nahodha huyo wa timu ya taifa ya
Ureno ni “mchezaji bora
wa muda wote”.
"Ni mchezaji bora wa muda wote duniani. Kamwe huwezi
kumfananisha na mchezaji mwingine yeyote, “alisema Mendes alipozungumza na muhariri wa michezo Dan Roan.
Ronaldo, mwenye umri wa miaka 29, mwezi uliopita alichaguliwa kwa
mara ya tatu kuwa mchezaji bora wa dunia, akimbwaga Lionel Messi wa Barcelona katika
tuzo hiyo.
Alipoulizwa mchezaji huyo ana thamani kiasi gani, Mendes alisema:
"Cristano Ronaldo? Bilioni moja. Anakaribia Bilioni moja, hivyo ni bilioni
moja. Kwa kweli haiwezekani kumpata mwingine anayefanana nay eye.
"Endapo kwa sabbau zozote zile klabu itaamua kumuuza hata
kesho kwa Milioni 300, mtu atalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa. "
Hata hivyo, Mendes alisisitiza kuwa raia huyo mwenzake wa Ureno
ambaye alinunuliwa na Real Madrid kwa rekodi ya dunia ya ada ya dola za
Marekani Milioni 80 mwaka 2009, ataendelea kubaki Bernabeu, licha ya “mapenzi yake" kwa klabu yake ya zaman ya Manchester United.
Alipoulizwa kama atamalizia soka lake Real Madrid, Mendes alisema "na
uhakika". "Hataondoka Real Madrid," aliongeza.
Mendes, aliyeripotiwa kuwa alipata zaidi na pauni bilioni 1 kwa
ajili ya uhamisho tu, akielezewa kuwa ni mmoja wa watu wenye nguvu sana katika
mchezo huo.
"Watu wana mtazamo tofauti kuhusu mawakala. Kuwa wakala kuna
maana tofauti. Mimi ni mtu wa kawaida kabisa. Ninafanya kazi kwa bidii kila
siku. Nina malengo na kusema ukweli ninatenda haki na hilo ndio muhimu zaidi.
Alielezea kuwa soka ni mchezo muhimu sana duniani na alitetea
mishahara ya wachezaji, akisema wanastahili kiasi kikubwa kama inawezekana".
Mendes alifananisha kufanyakazi na wachezaji kwa mikataba ni sawa
na familia.
"Ni kama vile unavyozungumza na mtoto wako, au familia yako
wakati wote unajaribu kutafuta njia bora ya kuwasaidia."
Mendes, DJ wazamani na mmiliki wa klabu ya usiku, pia ni wakala wa
Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari, Radamel Falcao, Angel Di Maria, James
Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa.
No comments:
Post a Comment