STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 29, 2014

Arsenal, Manchester City zashindwa kutambiana

Olivier Giroud and Mathieu FlaminiKLABU ya soka ya Arsenal imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Manchester City katika pambano la Ligi Kuu ya England.
Wageni wa walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 18 kupitia kwa David Silva na kudumu wakati wa mapumziko.
Hata hivyo wenyeji walifanikiwa kuchomoa bao hilo dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili kupitia kwa Mathieu Flamini akimalizia kazi nzuri ya Lucas Podolski.
Sare hiyo imeikwamisha Manchester City kukaa kileleni baada ya Chelsea kufungwa bao 1-0 na Crystal Palace kwani imefikisha pointi 67 kwa michezo 30 na kubakia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool yenye pointi 68 na itakayoshuka dimbani kesho Anfield kuumana na Tottenham Hotspur.
Arsenal yenyewe wamesalia kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi 64 na baada ya kushuka dimbani mara 32.

Samatta aivusha TP Mazembe 8 Bora

Shujaa Mbwana Samatta
TIMU ya TP Mazembe ya DR Congo imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sewe ya Ivory Coast.
Bao hjilo pekee lililoivusha Mazembe lilitupiwa kimiani na Mbwana Samatta  katika dakika ya 66, huku wakikosa pia penati baada ya Jonas Sakuwaha kushindwa kumtungia kipa wa Sewe Sylvain Gbohouo.
Ushindi huo uliopatikana mjini Lubumbashi, umeifanya Mazembe kufuzu kwa faida ya bao la ugenini kwani matokeo ya jumla yamekuwa 2-2 baada ya wiki iliyopita vijana hao wa Kongo kufungwa mabao 2-1 bao lililofungwa na Mbwana Samatta ambaye ni Mchezaji Bora wa Mwaka wa TP Mazembe kwa mwaka jana.

Ni Mwadui na Stand kupanda Ligi Kuu msimu ujao


Kocha wa Mwadui Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' akikaribia kuipandisha daraja timu hiyo
TIMU ya Mwadui Shinyanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu baada ya kuinyuka Toto Africans nyumbani kwao Mwanza kwa bao 1-0.
Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa ushindi huo wa ugenini imefikisha jumla ya pointi 28 na imesaliwa na mechi moja, huku Toto Africans ikipoteza matumaini ya kurejea katika ligi hiyo.
Hii inatokana na Stand Utd pia ya Shinyanga iliyopo nafasi ya pili kuibutua JKT Kanembwa nyumbani kwao mjini Kigoma kwa mabao 3-2 na kufikisha jumla ya pointi 26 na kuendelea kuibana Mwadui ambao wamekuwa na upinzani mkubwa baina yao.
Toto iliyopo nafasi ya tatu imebakia na pointi 21 ambapo hata kama itashinda mechi yao ya mwisho haitaweza kuwafikisha popote na kuziacha timu pinzani za Shinyanga, Mwadui na Stand zikisubiri kujua hatma ya mmoja wao kupanda Ligi Kuu msimu wa 2014-2015 siku ya Aprili 5 mwaka huu.
Tayari timu mbili za Polisi Moro na Ndanda Fc zimeshafuzu ligi ya msimu ujao baada ya kuongoza kwenye makundi yao ya A na B.

Hivi ndivyo Shule ya Joyland ilivyowapa faraja yatima wa Chamazi

Wanafunzi wa Joyland Pre& Primary wakiwa wamejichangana na yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund huku walimu wao wakiwa wamesimama

Walimu wa Shule ya Joyland wakijitambulisha mbele ya hadhara mchana wa leo kabla ya kukabidhi msaada wao kwa yatima
Mkurugenzi wa Shule ya Joyland, Fred Otieno akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwa yatima wa kituo cha Yatima Trust Funds
Wanafunzi wa Joyland wakiwa wamekaa kando ya yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund
Baadhi ya yatima wanaolelewa na kituo cha Yatima Trust Funds wakiwa makmini kufuatilia matukio yaliyokuwa wakiendelea kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na Shule ya Joyland
Watoto wakiwa bize kufuatilia matukio kwenye hafla iliyofanyika leo Chamazi
Yatima wanaolelewa kituo cha Yatima Trust wakionyesha ujuzi wao wa kunengua
Wnachuana kucheza muziki uliokuwa unaporomoshwa
Kama Super Nyamwela! Dogo ana kipaji cha kucheza muziki nouma!
Bendi ya Shule ya Joyland ilikuwapo kuwatumbuiza yatima siku ya leo yaani ilikuwa faraja kubwa kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Joyland Pre& Primary, Fred Otieno akiomba kabla ya shughuli kuanza...yaani kama Pastor
Ameen! Walimu na watoto wakitikia sala ya mambi kabla ya shughuli kuanza leo Chamazi.
Ameeen! Watoto wakiitikia dua
Baadhi ya yatima wakiwa wamewabeba wanafunzi wa Joyland waliowatembelea kituoni kwao leo na kukabidhiwa msaada ya vitru mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Mil. 5
Utoto bana! wenzake wanaangalia mbele yeye anaangalia nyuma, lakini ni raha tupu!
Baadhi ya walimu wa Joyland wakiwa katika pozi kuangalia usalama wa watoto wao na yatima waliowatembelea
Yaani hawa madogo walifanya hata wenzao wasahau kucheza muziki kuwashuhudia vizuri wanavyochuana kunengua kwa raha zao
We angalia mpambano ulivyokuwa halafu toa maoni yako unadhani nani aliibuka mkali wa kudansi
Mkaanga Chips huyu balaa kama Titina Alcapone au Komba Belou Mafwala

Sehemu ya msaada uliotolewa na Shule ya Joyland kwa Yatima Trust Funds
Madam Anna alikuwa bize na mtoto aliyempakata...uchungu wa mwana jamani!
baadhi ya walimu wa Joyland waliowatembelea yatima wa Chamazi
Walimu wa Joyland wakiwa katika pozi

Messi airejesha Barcelona kileleni Hispania

http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/002/327/252/hi-res-159041765_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75BAO pekee la mkwaju wa penati lililofungwa na Lionel Messi katika dakika ya 77 limeisaidia Barcelona kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Espanyol na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligu Kuu ya Hispania ikiishusha Atletico Madrid.
Barcelona ambayo ilibanwa na wenyeji wao kabla ya kuja kuwazidi wapinzani wao waliompoteza kipa wao Casilla Cortés aliyelimwa kadi nyekundu.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufika jumla ya pointi 75, mbili zaidi ya Atletico Madrid ambayo ina 73 na inatarajiwa kushuka dimbani baadaye na iwapo itashinda inaweza kurejea kwenye kiti chake cha uongozi.
Vijana hao wa Diego Simeone itakuwa ugenini kupepetana na Athletic Club, moja ya mapambano matatu ya ligi hiyo kwa leo, jingine litazikutanisha timu za Celta Vigo dhidi ya Sevilla.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mingine kadhaa ukiwamo wa Real Madrid watakaokuwa nyumbani kwao Santiago Bernabeu kuikaribishaRayo Vallecano huku wakiuguza vipigi viwili mfululizo toka kwa Barcelona na Sevilla.

Chelsea yapigwa kimoja, Southampton ikiiua Newcastle Utd

John Terry own goal
Kitu! John Terry akijifunga bao langoni mwake wakati akichuana na Joel Ward huku kipa Petr Cech hakiwa hana la kufanya
Rickie Lambert scores
Rickie Lambet (7) akifunga moja ya mabao yake mawili Southampton ilipoinyuka Newcastle United kwa 4-0
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea imeendelea kunyanyaswa na timu ndogo baada ya leo kukubali kipigo cha bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Bao la kujifunga la beki na nahodha wake, Jerry Terry katika dakika ya 52, lilitosha kuinyong'onyesha Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho ambayo imesaliwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 32.
Pointi hizo zinaweza kufikiwa na Manchester City iwapo itashinda mchezo wake unaoanza hivi punde dhidi ya  Arsenal na kuwaondoa kileleni kwa tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
City hata hivyo kama itashinda itaongoza msimamo huo kwa saa chache tu iwapo Liverpool itapata ushindi katika mechi yao ya kesho nyumbani dhidi ya Tottenham.
Liverpool wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 68 na Ciy ni wa watatu wakiwa na pointi zao 66 na michezoi mitatu mkononi kwa sasa.
Katika mechi nyingine zilizomalizika hivi punde katika ligi hiyo Southmpton ikiwa nyumbani iliitafuna Newcastle United kwa mabao 4-0. mabao ya washindi yalifungwa na Jay Rodriguez, Rickie Lambert aliyefunga mawili na Adam Lallana, huku Stoke City ikitambia Hull City kwa bao 1-0 na Swansea City ikitamba nyumbani kwao kwa kuilaza Norwich City kwa mabao 3-0 na West Bromwich ilishindwa kulinda mabao yake na kulazimishwa sare ya 3-3 na wageni wao Cardiff City.

Bayern Munich bado haishikiki Bundesliga

http://thesoccerdesk.com/wp-content/uploads/2013/11/bayern-munich.jpg
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bayern Munich, imeendelea kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote katika ligi hiyo baada ya jioni hii kulazimishwa sare ya 3-3 ma Hoffenheim.
Bavarians waliotetea taji hilo mwanzoni mwa wiki hii kwa kuifunga Hertha Berlin mabao 3-1, ilishutuliwa na wageni wao baada ya  Anthony Modeste alipofunga katika dakika yua 23.
Hata hivyo wenyeji walicharuka na kusawazisha bao kupitia kwa Claudio Pizarro katika dakika ya 31 kabla ya Xherdan Shaqiri kuongeza la pili katika dakika ya 34.
Pizarro aliongeza bao jingine dakika ya 40 na dakika moja kabla ya mapumziko Salihovic aliifungia Hoffenheim bao la pili na kufanya timu yao iende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 3-2.
Kipindi cha pili wageni waliopo nafasi ya katikati waliendelea kuwasumbua wenyeji wao na kufanikiwa kusawazisha bao katika dakika ya 75 kupitia kwa Roberto Firmino.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Borussia Dotmund ikiwa ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Stuttgart, Bayer Leverkusern ililazimishwa sare ya 1-1 na Eintracht Braunschweig.
Nayo timu ya Wolfsburg wakiitandika Eintracht Frankfurt 2-1 na Mainz 05 ikapata ushindi mnono nyumbani kwa kuizabua Augsburg kwa mabao 3-0.

Ashanti Utd yawafumua maafande wa Oljoro JKT

Ashanti United ambao wameibuka na ushindi leo dhidi ya Oljoro JKT ya Arusha
 WATOTO wa Jiji, Ashanti United jioni ya leo imezinduka na kufufua matumaini yao ya kubaki katika Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuwacheza kwata maafande wa Oljoro JKT ya Arusha kwa kuwalaza mabao 2-1 katika pambano pekee la ligi hiyo lililochezwa leo.
Pambano hilo lilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi na washindi walienda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Hassani Kabunda, huku Oljoro wakipoteza penati katika dakika ya tano tu ya mchezo huo.
Kipindi ca pili wenyeji walipata bao la pili lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Hassani Kabunda kabla ya Oljoro kujipatia bao la kufutria machozi lililotokana pia kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Shaibu Nayopa.
Ushindi huo uliokuwa ukihitajiwa mno na Ashanti umeiwezesha timu hiyo inayonolewa na kocha mahiri, King Abdallah Kibadeni, kufikisha jumla ya pointi 21 kutokana na mechi 23 na kushika nafasi ya 11.
Oljoro ambayo inapigana kuepuka kushuka daraja kama ilivyo kwa wapinzani wao, imeendelea kusota kwenye nafasi ya 13 ikiwa na pointi 16, tatu zaidi ya wanaoburuza mkia Rhino Rangers ambayo kesho itakuwa wageni wa JKT Ruvu kwenye uwana wa Chamazi.
Mechi nyingine zitakazopigwa kesho ni kati ya vinara wa ligi hiyo, Azam itakayokwaruzana na Simba kwenye uwanja wa Taifa, Yanga watakuwa ugenini kuumana na Mgambo JKT, huku mabingwa wa zamani Mtibwa Sugar na Coastal Union watapepetana uwanja wa Manungu, Morogoro na Kagera Sugar itaialika Ruvu Shooting na jiji la Mbeya litashuhudia Mbeya City na Prisons-Mbeya zitaumana uwanja wa Sokoine.

Redd's Miss Tanzania washtuliwa na BASATA

http://1.bp.blogspot.com/-YgPsRHsV4MQ/TzyRlxUt_GI/AAAAAAAAISM/cx9pDCKriOI/s1600/IMG_9116.JPG
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeitaka Kamati ya Miss Tanzania kutohusisha burudani zinazokiuka maadili ya Mtanzania wakati wa mashindano yao ya urembo mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mashindano ya Miss Tanzania 2013 kilichofanyika kwenye ukumbi wa baraza hilo, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa BASATA, Vivian Shalua, alisema kuwa maadili ni muhimu kuzingatiwa katika mashindano hayo ili kuepukana na dhana potofu kuwa yanahusiana na uhuni.

“Maadili yazingatiwe katika mashindano ya mwaka huu, kuanzia kwa washiriki hadi burudani zitakazohusishwa, kama ‘vigodoro’, ‘kanga moja mbendembende’ na nasikia siku hizi kuna ‘tisheti ndembendembe’,” alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema kuwa BASATA ipo tayari kuyapigania mashindano ya Miss Tanzania kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo.
Mkurugenzi huyo pia aliitaka Lino kuwaelimisha mawakala wanaoandaa mashindano hayo juu ya umuhimu wa kuwa na vibali kutoka BASATA, ikiwa ni pamoja na kutowavumilia watovu wa nidhamu bila kujali ukongwe wao katika tasnia hiyo.
Kwa upande wake, Ofisa Sanaa Kitengo cha Matukio, Kurwijira Maregesi, aliitaka Lino kujipanga kujiweka tayari kufanya mashindano hata pale inapokosa mdhamini, huku mjumbe mwingine katika kikao hicho ambaye ni Ofisa Sanaa BASATA, Philemon Mwasanga, akisisitiza mawakala kuwekeana mikataba na warembo kabla ya mashindano kuanza.
“Lino isiwafumbie macho mawakala wasiojali mikataba na warembo, na warembo waisome na kuielewa ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea,” alisema.
Akijibu hoja kadhaa zilizoibuliwa katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga, alisema kuwa wamejipanga ili kuweza kufanya mashindano yao bila kutegemea wadhamini, huku akiitaka BASATA kuwasaidia katika hilo.
“Tatizo mashindano yetu gharama yake ni kubwa sana, nasi hatupendi kuona ubora wake ukishuka kutokana na kushindwa kumudu gharama, ndio maana tumekuwa tukihangaika kuomba udhamini kutoka katika makampuni mbalimbali makubwa hapa nchini,” alisema.
Juu ya mikataba baina ya warembo na mawakala, Lundenga alisema: “Mwaka huu tumesisitiza mawakala waingie mikataba na washiriki kabla ya mashindano na tutakuwa makini katika kufuatilia hilo na changamoto nyinginezo zilizoibuliwa katika kikao hiki.”
Mmoja wa warembo walioshiriki mashindano ya mwaka jana ambaye ni Miss Sinza 2013, Prisca Clement, alisema kuwa kuna umuhimu wa kuongezwa kwa zawadi katika ngazi za chini ili kumwezesha mshiriki kujivunia na kujitosa kwake katika mashindano hayo bila kujali kama ameshinda au la.
Mashindano ya Miss Tanzania 2014 yamezinduliwa mapema wiki hii ambapo fainali zake zinatarajiwa kuwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Orirginal.

Jahazi la timu ya Babi lazidi kuzama Malaysia

Kikosi cha UiTM anayoichezea Abdi Kassim (wa kwanza kulia mbele)
JAHAZI la timu ya UiTM anayoichezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' limezidi kuzama kwenye Ligi Kuu ya nchini Malaysia baada ya jana kufungwa kwa mara ya pili mfululizo.
UiTM iliyokuwa ugenini, ilikumbana na kipigo cha bao 1-0 toka kwa wenyeji wao Negeri Sembilan,  waliowafuata kwenye uwanja Tuanku Abdulrahaman, mjini Seremban ikiwa ni siku chache tangu idunguliwe nyumbani kwa mabao 4-1 na Felda United.
Kipigo hicho cha jana ni cha sita katika michezo 9 iliyocheza timu hiyo na kuifanya izidi kuporomoka kwenye msimamo wa ligi hiyo ikienda nafasi ya 11, nafasi moja toka mkiani.
UiTM iliyomsajili Babi kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMKM imesaliwa na pointi zake 7 kutokana na kushinda mechi mbili tu na kuambulia sare moja na kupoteza mechi zilizosalia.
Timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani Ijumaa ijayo kwa kuvaana na Kedah kwenye uwanja wao wa nyumbani.

PSG yazidi kupeta Ufaransa

Paris Saint Germain's Zlatan Ibrahimovic of Sweden, center, controls the ball past Nice's Mathieu Bodmer of France, left, during their French League One soccer match, in Nice stadium,southeastern France, Friday, March 28, 2014. (AP Photo/Lionel Cironneau)
Zlatan Ibrahimovic akichuana na wachezaji wa Nice wakati PSG ilipopata ushindi wa ugenini
BAO la kujifunga la Timothee Kolodziejczak wa Nice usiku wa jana liliisaidia mabingwa watetezi wa Ligue 1, PSG kuendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo na kujichimbia kileleni.
Wenyeji walijifunga bao hilo katika dakika ya 52 wakati Kolodziejczak akiwa katika harakati za kuokoa mpira na kuisaidia PSG ambayo Jumatano itavaana na Chelsea katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa  Ulaya kujikita kileleni.
Timu hiyo kwa ushindi wa jana imefikisha jumla ya pointi 76 kutokana na michezo 31 na kuwaacha wanaowafukuzia Monaco kwa pointi 13 hata Monaco itakayoshuka dimbani leo dhidi ya Evian TG.

Shule ya Joyland yasaidia yatima msaada wa thamani ya Sh. Mil.5

Mkuruigenzi wa Shule ya Joyland Pre & Primary, Fred Otieno (wa pili kulia) na mmoja wa walimu wa shule hilo wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa Baba Mlezi wa Kityo cha Kulelea Yatima cha Yatima Trust Fund, Haruna Mtandika (kushoto) huku wakisaidiwa na baadhi ya yatima wa kituo hicho.
Mmoja wa walimu wa Shule ya Joyland, Madam Anna akiwa amempakata mmoja wa yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Yatima Trust Fund, mara baada ya kukabidhi msaada wao kwa kituo hicho kilichopo Chamazi.
Mmoja wa yatima, Halima Seif akitoa shukrani zake na kuililia serikali na watu wengine kuwasaidia kuwaendeleza kielimu.
Viongozi wa Shule ya Joyland wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Fred Otieno (wa nne toka kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada walioutoa leo kwa kituo cha Yatima Trust Fund
Ngojeni tuwasaidie kupeleka ndani! Baadhi ya wasaidia wa kituo cha Yatima Trust Fund wakipelekea misada waliyopewa ndani ya stoo yao
Huu ni mwanzo tu, tutawaletea zaidi
Mkurugenzi wa Joyland Pre& Primary, Fred Otieno akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukabidhi msaada wao kwa yatima leo jijini Dar es Salaam.
Baba Mlezi na mmoja wa waasisi wa Yatima Trust Fund, Haruna Mtandika akitoa shukrani zake wakati akizungumza na wanahabari
 UONGOZI wa Shule ya Joyland Pre & Primary ukishirikiana na wazazi wa watoto wanaosoma shule iliyopo Tuangoma, Kigamboni umetoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 5 kwa kituo cha kulelea yatima cha Yatima Trust Fund.
Msaada huo ulikabidhiwa leo mchana na uongozi wa Shule hiyo kwa viongozi wa kituo hicho kilichopo Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika kwenye kituoni hapo.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Fred Otieno alisema uongozi wa shule yao ambayo haina muda mrefu tangu ianzishwe ukishirikiana na wazazi waliamua kujitolea msaada huo kama sehemu ya kuonyesha namna wanavyoguswa na yatima nchini.
Otieno alisema ingawa walichokitoa ni kidogo, lakini anaamini kitawasaidia yatima hao na kutoa wito kwa watu wengine kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia yatima sehemu yoyote walipo.
"Kama sehemu ya jamii tunaguswa na matatizo ya yatima na ndiyo maana tukaamua kuchangishana kuanzia walimu, uongozi wa shule, wazazi na hata wanafunzi ili kuja kuwafariji yatima hawa." alisema.
Otieno alisema yatima hawapaswi kuachwa, hawakupenda kuwapoteza wazazi, hivyo wafarijiwe kwa kusaidia kwa hali na mali na wao wameonyesha mfano ili wengine waige.
Naye Baba mlezi na muasisi wa kituo hicho, Haruna Mtandika aliyepokea msaada huo kwa niaba ya uongozi na yatima wanaolelewa kituoni hapo waliushukuru uongozi wa shule ya Joyland.
Mtandika alisema Yatima Trust Fund iliyoasisiwa mwaka 1996 na kusajiliwa rasmi mwaka 2001 wamefariji kwa kukumbukwa kwa msaada huo na kuwaomba watu waige mfano wa shule hiyo.
"Tunawashukuru sana Joyland kwa kuonyesha moyo wa huruma kwa yatima hawa, na Mungu awabariki zaidi kwani nimesikia shule yenu haina muda mrefu tangu muianzishe lakini umeonyesha mfano wa kuigwa," alisema
Pia alidokeza kwenye risala yao changamoto wanayokabiliana nayo ikiwamo uhaba wa samani kwa ajili ya malazi, chakula, ada na sare kwa watoto wanaowasomesha, ambapo Mkurugenzi wa Joyland, aliahidi kuwasomesha watoto wawili toka kituoni hapo.
Otieno, alisema watoto hao mmoja mmoja wa kike na mwingine wa kiume watasomeshwa kwa kugharamiwa na uongozi wa shuleni kuanzia chekechea hadi darasa la saba.
Naye mmoja wa watoto wanaolelewa kituoni hapo, Halima Seif (16) pamoja na kuushukuru uongozi wa Joyland, pia alitoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kuwasaidia kusomeshwa.
"Nilikuwa naomba watu watusaidie, kwa mfano mimi napenda shule, lakini sijaendelea na masomo ya sekondari kwa sababu sina wa kunilipia ada hiyo nawaomba watu wengine watuangalie sisi yatima," alisema Halima huku akimwaga chozi la uchungu.
Mara baada ya makabidhiano hayo, uongozi wa shule, walimu na waalikwa wengine walijumuika kula na kuburudika na muziki na yatima hao kama njia ya kuwafariji jambo lililonekana kufurahiwa na watoto hao.

Manchester Utd yaua Old Trafford

Wayne Rooney heads home Manchester United's equaliser
Rooney akifunga bao la kwanza la Man Utd
Inside out: As Mata turns inside Bacuna the defender takes the Spanish midfielders legs out
'Fundi' Juan Mata akiwajibika uwanjani
KLABU ya Manchester United leo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford wameifumua bila huruma Aston Villa kwa kuikandika mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mashetani Wekundu waliotoka kuchezea kichapo cha aibu cha mabao 3-0 toka kwa Mahasimu wao, Manchester City, leo ilionekana wamekuja kivingine na hasa kocha wao David Moyes kuwachezesha kwa pamoja mafundi, Shinji Kagawa na Juan Mata.
Wageni walianza kuwashtua vijana wa Moyes kwa kufunga bao katika dakika ya 13 kupitia kwa Ashley  Westwood kabla Wayne Rooney kusawazisha dakika saba baadaye kwa pasi ya Mjapan Kagawa.
Rooney alirejea tena kimiani kwa kuifungia Man Utd bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Mata kuchezewa faulu na kufanya Mashetani hao kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 2-1
Kipindi cha pili Man walizidi kuonyesha wamedhamiria kuwatia adabu Villa walioiangusha Chelsea wiki iliyopita baada ya Juan Mata kufunga bao la tatu katika dakika ya 57.
Mtokea benchi Javier Hernández 'Chicharito' alihitimisha karamu ya mabao kwa kupachika bao la nne katika dakika ya nyongeza kabla ya mpira kwisha na kumpa Moyes afueni toka kwa mashabiki kwa ushindi huo mnono uliowafanya wafikishe jumla ya pointi 54.
Hata hivyo ushindi huo bado umeiacha Red Devils kwenye nafasi ya saba baada ya kucheza meci 32 na Aston Villa wamebaki nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi inayoendelea kwa sasa kwa mechi kadhaa.