STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 29, 2014

Manchester Utd yaua Old Trafford

Wayne Rooney heads home Manchester United's equaliser
Rooney akifunga bao la kwanza la Man Utd
Inside out: As Mata turns inside Bacuna the defender takes the Spanish midfielders legs out
'Fundi' Juan Mata akiwajibika uwanjani
KLABU ya Manchester United leo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford wameifumua bila huruma Aston Villa kwa kuikandika mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mashetani Wekundu waliotoka kuchezea kichapo cha aibu cha mabao 3-0 toka kwa Mahasimu wao, Manchester City, leo ilionekana wamekuja kivingine na hasa kocha wao David Moyes kuwachezesha kwa pamoja mafundi, Shinji Kagawa na Juan Mata.
Wageni walianza kuwashtua vijana wa Moyes kwa kufunga bao katika dakika ya 13 kupitia kwa Ashley  Westwood kabla Wayne Rooney kusawazisha dakika saba baadaye kwa pasi ya Mjapan Kagawa.
Rooney alirejea tena kimiani kwa kuifungia Man Utd bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Mata kuchezewa faulu na kufanya Mashetani hao kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 2-1
Kipindi cha pili Man walizidi kuonyesha wamedhamiria kuwatia adabu Villa walioiangusha Chelsea wiki iliyopita baada ya Juan Mata kufunga bao la tatu katika dakika ya 57.
Mtokea benchi Javier Hernández 'Chicharito' alihitimisha karamu ya mabao kwa kupachika bao la nne katika dakika ya nyongeza kabla ya mpira kwisha na kumpa Moyes afueni toka kwa mashabiki kwa ushindi huo mnono uliowafanya wafikishe jumla ya pointi 54.
Hata hivyo ushindi huo bado umeiacha Red Devils kwenye nafasi ya saba baada ya kucheza meci 32 na Aston Villa wamebaki nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi inayoendelea kwa sasa kwa mechi kadhaa.

No comments:

Post a Comment