STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 29, 2014

Chelsea yapigwa kimoja, Southampton ikiiua Newcastle Utd

John Terry own goal
Kitu! John Terry akijifunga bao langoni mwake wakati akichuana na Joel Ward huku kipa Petr Cech hakiwa hana la kufanya
Rickie Lambert scores
Rickie Lambet (7) akifunga moja ya mabao yake mawili Southampton ilipoinyuka Newcastle United kwa 4-0
VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea imeendelea kunyanyaswa na timu ndogo baada ya leo kukubali kipigo cha bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Bao la kujifunga la beki na nahodha wake, Jerry Terry katika dakika ya 52, lilitosha kuinyong'onyesha Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho ambayo imesaliwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 32.
Pointi hizo zinaweza kufikiwa na Manchester City iwapo itashinda mchezo wake unaoanza hivi punde dhidi ya  Arsenal na kuwaondoa kileleni kwa tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
City hata hivyo kama itashinda itaongoza msimamo huo kwa saa chache tu iwapo Liverpool itapata ushindi katika mechi yao ya kesho nyumbani dhidi ya Tottenham.
Liverpool wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 68 na Ciy ni wa watatu wakiwa na pointi zao 66 na michezoi mitatu mkononi kwa sasa.
Katika mechi nyingine zilizomalizika hivi punde katika ligi hiyo Southmpton ikiwa nyumbani iliitafuna Newcastle United kwa mabao 4-0. mabao ya washindi yalifungwa na Jay Rodriguez, Rickie Lambert aliyefunga mawili na Adam Lallana, huku Stoke City ikitambia Hull City kwa bao 1-0 na Swansea City ikitamba nyumbani kwao kwa kuilaza Norwich City kwa mabao 3-0 na West Bromwich ilishindwa kulinda mabao yake na kulazimishwa sare ya 3-3 na wageni wao Cardiff City.

No comments:

Post a Comment