STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 29, 2014

Messi airejesha Barcelona kileleni Hispania

http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/002/327/252/hi-res-159041765_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75BAO pekee la mkwaju wa penati lililofungwa na Lionel Messi katika dakika ya 77 limeisaidia Barcelona kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Espanyol na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligu Kuu ya Hispania ikiishusha Atletico Madrid.
Barcelona ambayo ilibanwa na wenyeji wao kabla ya kuja kuwazidi wapinzani wao waliompoteza kipa wao Casilla Cortés aliyelimwa kadi nyekundu.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufika jumla ya pointi 75, mbili zaidi ya Atletico Madrid ambayo ina 73 na inatarajiwa kushuka dimbani baadaye na iwapo itashinda inaweza kurejea kwenye kiti chake cha uongozi.
Vijana hao wa Diego Simeone itakuwa ugenini kupepetana na Athletic Club, moja ya mapambano matatu ya ligi hiyo kwa leo, jingine litazikutanisha timu za Celta Vigo dhidi ya Sevilla.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mingine kadhaa ukiwamo wa Real Madrid watakaokuwa nyumbani kwao Santiago Bernabeu kuikaribishaRayo Vallecano huku wakiuguza vipigi viwili mfululizo toka kwa Barcelona na Sevilla.

No comments:

Post a Comment