STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Chelsea ilipaki mabasi mawili Anfield, kocha Liver alia

Makocha wanaofukuzana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England
MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amemtuhumu meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwa kupaki mabasi mawili na kuipa ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Anfield. 
Katika mchezo huo mabao ya Chelsea yalifungwa na Demba Ba aliyetumia vyema makosa ya nahodha Steven Gerrard kipindi cha kwanza na lingine la Willian katika majeruhi. 
Kocha Rodgers amesema wapinzani wao walipaki mabasi mawili langoni mwao akimaanisha walikuwa wakizuia kipindi chote cha mchezo huo hivyo kuwapa wakati mgumu kupenya ngome yao ingawa walijitahidi kujaribu. 
Rodgers amesema walijitahidi kushinda mchezo huo lakini walishindwa kupenya ngome ya wapinzani wao ambayo ilikuwa ikilindwa vizuri. 
Pamoja na ushindi huyo Mourinho bado ameendelea kudai kuwa hawana nafasi ya kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu na kudai kuwa mbio hizo wamewaachia Manchester City na Liverpool. 
Mreno huyo amesema kitu cha msingi alichokuwa akihitaji ni kupata alama tatu hizo muhimu ambazo zitawasaidia kujihakikishia nafasi tatu katika msimamo wa ligi hivyo kufuzu moja kwa moja bila kucheza mechi za mtoano katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Timu hiyo ya Mourinho kesho itakuwa na kibarua kizito mbele ya Atletico Madrid katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali.
Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka suluhu bila kufungana mjini Madrid na hivyo Chelsea inapatakiwa kuhakisha inapata ushindi au sare isiyokuwa na mabao iwapo inataka kufuzu hata kwa mikwaju ya penati.

No comments:

Post a Comment