STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Haya ndiyo makundi ya AFCON 2015

Kocha Steven Keshi akiwa amebebwa baada ya kuipa Nigeria taji la AFCON 2013 nchini Afrika Kusini

WAKATI Tanzania itaanzia katika hatua ya awali ya michuano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015, mabingwa watetezi Nigeria watawakabili Afrika Kusini na Sudan katika kundi lao la kuwania kutinga katika fainali hizo zitakazofanyika Morocco.
Kikosi cha kocha Stephen Keshi kilitwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mwaka 2013 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Burkina Faso na watakutana na wenyeji wa mwaka huo, Afrika Kusini, katika kuwania kufuzu kwa fainali za 2015.
Timu hizo mbili zinaungana na Sudan katika Kundi A, wakati timu nafasi moja ya mwisho ya kufuzu kuingia katika kundi hilo kutokea katika hatua ya awali itagombewa na timu za Namibia, Congo, Libya au Rwanda.
Burkina Faso watakabiliana na Angola na Gabon katika Kundi C, na nafasi moja ya mwisho itagombewa na timu za Liberia, Lesotho, Kenya na Comoro.
Ivory Coast na Cameroon, ambao wataungana na Nigeria katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil, wamepangwa pamoja katika Kundi D la kuwania kufuzu pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ghana - taifa jingine litakaloenda kwenye Kombe la Dunia - litakabiliana na mahasimu wao wa Afrika Magharibi, Togo katika Kundi  E, wakati Algeria, wawakilishi wengine wa Afrika nchini Brazil, watakuwa na mechi dhidi ya Mali na Ethiopia katika Kundi B.
Mabingwa mara saba Misri watawavaa Tunisia na Senegal katikaKundi G.

Makundi yote ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2015 kwa ujumla:

Kundi A: Nigeria, Afrika Kusini, Sudan na moja kati ya Namibia, Congo, Libya na Rwanda

Kundi B: Mali, Algeria, Ethiopia na moja kati ya Sao Tome na Principe, Benin, Malawi na Chad

Kundi C: Burkina Faso, Angola, Gabon na moja kati ya Liberia, Lesotho, Kenya na Comoros

Kundi D: Ivory Coast, Cameroon, DR Congo na moja kati ya Swaziland, Sierra Leone, Gambia na Shelisheli

Kundi E: Ghana, Togo, Guinea na moja kati ya Madagascar, Uganda, Mauritania na Equatorial Guinea

Kundi F: Zambia, Cape Verde, Niger na moja kati ya Tanzania, Zimbabwe, Msumbiji na Sudan Kusini

Kundi G: Tunisia, Misri, Senegal na moja kati ya Burundi, Botswana, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Guinea Bissau.

No comments:

Post a Comment