STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Ubingwa mweupe kwa Juventus, yaifumua Sassuolo 3-1

Wachezaji wa tatu wa Juve (jezi za njano) wakiwania mpiura na beki wa Sassuolo walipoikandika timu hiyo mabao 3-1 ugenini
JUVENTUS imebakisha mechi moja tu kutangazwa tena kuwa mabingwa wa Italia baada ya usiku wa kuamkia leo kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Sassuolo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya nchini hiyo Seria A.
Mabingwa hao watetezi ambao Alhamis hii watakuwa nyumbani kwao kuwakaribisha Benfica ya Ureno kwenye mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi Ndoigo ya Ulaya (UEFA Europa League) ili kujaribu kupindua matokeo ya kipigo cha mabao 2-1, ilishtukiza kwa bao la mapema la dakika 9 la wenyeji liliwekwa kimiani na Simone Zaza.
Hata hivyo wakati wakitafakari jinsi ya kulirudisha bao hilo wenyeji hao waliwasaidia  kulisawazisha wenyewe baada ya Alessandro
Longhi kujifunga dakika ya 34.
Juventus maarufu kama kibibi kizee cha turin, iliongeza bao la pili katika dakika ya     58 kupitia Claudio Marchisio kabla ya Llorente kufunga bao la tatu katika dakika ya 76 na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 93, nane zaidi na ilizonazo wanaoshikilia nafasi ya pili Roma wenye pointi 85 na kila timu ikiwa imesaliwa na mechi tatu kabla ya kufunga msimu huu.

No comments:

Post a Comment