STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Del Piero atundika daluga zake

MCHEZAJI mkongwe Alessandro Del Piero ameamua kutundika daruga kuitumikia klabu ya Sydney FC lakini anaweza kurejea kwa shughuli nyingine. 
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa kocha katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Australia baada ya Frank Farina kutimuliwa. 
Del Piero, 39 na klabu hiyo wanataka kuendelea na mahusiano lakini haijabainika wazi ni uhusiano wa namna gani. 
Akiwa amefunga jumla ya mabao 24 yakimfanya kuwa mfungaji bora wa klabu katika misimu yote miwili aliyoitumikia, mkali huyo aliandika ujumbe kushukuru na kuaga kupitia mtandao wake. 
Del Piero amesema katika ujumbe huo ule wakati umewadia safari yake akiwa na Sydney FC inakaribia ukingoni ingawa inasikitisha lakini amekuwa na muda mzuri katika kipindi chote alichoitumikia.

No comments:

Post a Comment