STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Neymar akemea ubaguzi wa rangi Hispania

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar amesema atapambana na ubaguzi wa rangi baada ya mchezaji mwenzake Dani Alves kurushiwa ndizi wakati wa mechi yao waliyoshinda 3-2 ugenini dhidi ya Villarreal juzi.
"Sisi sote tuko sawa, sisi sote ni nyani, sema hapana kwa ubaguzi wa rangi," Neymar aliandika katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii, akiweka 'hashtag' #SisiSoteNiNyani.
"Ni aibu kwamba hadi mwaka 2014 bado kuna matendo kama haya. Ni wakati sasa wa watu kuinua sauti zao kukemea. Njia yangu ya kusapoti ni kufanya alichofanya Dani Alves.
"Kama nawe unasapoti kampeni hii, jipige picha ukila ndizi nakisha tutaitumia katika kupinga ubaguzi huu."

No comments:

Post a Comment