STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 29, 2014

Muumin & Double M Sound kujitambulisha Kigoma

Muumin
BAADA ya kukonga nyoyo za mashabiki wa mikoa ya Shinyanga na Kagera wakati wa sikukuu ya Pasaka, bendi iliyorejeshwa upya ya Double M Sound mwezi ujao inatarajiwa kwenda kujitambulisha kwa wakazi wa Kigoma.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Prince Mwinjuma Muumini aliiambia MICHARAZO kuwa, wanatarajia kwenda kuitambulisha bendi yao katika miji ya Kibondo na Kasulu iliyopo mkoani Kigoma.
Muumin alisema onyesho la kwanza mkoani humo watalifanya Mei 9 mjini Kibondo kabla ya siku inayofuata watahamia Kasulu kabla ya kurejea maskani kwao Kahama-Shinyanga kwa ajili ya kufanya mazoezi za uzinduzi rasmi.
"Tunashukuru tumerejea salama kutoka kwenye maonyesho yetu wakati wa sikukuu ya Pasaka kwa kutambulisha bendi eneo la Kakola, Ushirombo, Ruzewe, Ngara na Katoro. Kwa sasa tupo kambini mjini Kahama kujiandaa na ziara ya mkoani Kigoma mapema mwezi ujao," alisema Muumin.
Muumin aliongeza kuwa uongozi wao unajipanga kufanya uzinduzi na onyesho la kwanza kuitambulisha na kuizindua Double M Sound mjini Kahama mwishoni mwa mwezi ujao.
"Pamoja na watu kujua Double M Sound ipo Kahama, lakini hawajawahi kuiona hadharani kwa sababu tunapanga kuizindua rasmi mwishoni mwa Mei na kisha ndipo tuanze kuifanya maonyesho mjini hapa," alisema Muumin.
Double M Sound iliyowahi kutamba na nyimbo mbalimbali ilisambaratika mara baada ya uzinduzi wa albamu yao ya Titanic mwaka 2004 na Muumin ameamua kuifufua upya na kujichimbia Kahama kama maskani yake kwa sasa.

No comments:

Post a Comment