STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 12, 2013

Hussein Javu sasa njia panda

Hussein Javu akiwa katika pozi
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu amekiri kwamba amewahi kufuatwa na klabu za Simba na Yanga kwa nia ya kumsajili, lakini hadi sasa hajui kinachoendelea kuhusu majaliwa yake msimu ujao.
Javu alisema hata taarifa kwamba amesajiliwa Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu anazisikia tu hewani, ila ukweli suala hilo sio kweli kwa vile hajasaini mkataba wowote na mabingwa hao wa soka nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, mshambuliaji huyo aliyekuwa kinara wa mabao ndani ya Mtibwa Sugar na mmoja wa wachezaji wanaounda timu ya pili ya taifa 'Young Taifa Stars' alisema Simba na Yanga kwa nyakati tofauti walimfuata kwa nia ya kumshawishi kujiunga na timu zao, lakini  aliwaelekeza wamalizane na 'mabosi' wake.
"Unajua mimi bado nina mkataba na Mtibwa, pia klabu hii nimetoka nayo mbali hivyo sikuwa na maamuzi zaidi ya kuwataka Simba na Yanga wazungumze na uongozi wa klabu yangu na kwa msingi huo yaliyoendelea au yanayoendelea siyajui," alisema.
Kuhusu kwamba tayari keshasaini mkataba wa miaka mitatu Yanga, Javu alisema hilo halina ukweli kwa sababu hakuna fomu zozote alizosaini mpaka sasa na kushangaa habari hizo kusambazwa kwenye vyombo vya habari.
"Ningekuwa nimesaini ndugu yangu ningekuambia ukweli, hilo halijafanyika na wala sijajua kinachoendelea au kujua kama msimu ujao nitacheza Mtibwa, Yanga au Simba," alisema.
Aliongeza kuwa, yeye kama mchezaji anasubiri kusikia maelekezo ya viongozi wake kama wameafikiana na Yanga au Simba na wangetaka kumuuza hatakuwa na tatizo na kama wataamua kumbakisha Mtibwa Sugar kwa msimu mwingine pia kwake ni sawa tu kwani anafurahia maisha katika klabu hiyo ya Manungu.
"Nikibakishwa Mtibwa Sugar au kuuzwa Yanga au Simba poa mradi masilahi yawepo kwani soka ndiyo ajira yangu na siwezi kuchagua mahali pa kwenda," alisema.
Dai la kwamba yeye ni majeruhi wa kudumu wa goti, Javu alisema taarifa hizi zinalengo la kumharibia kwani hajawahi kuumia kwa siku za karibuni na kushangaa wanaompakazia uzushi huo.
Alisema anadhani wanaomzushia wanafanya hivyo kwa minajili ya kukomoana baina ya Simba na Yanga ambao wamekuwa na mvutano wa kumwania mara baada ya ligi kuu msimu uliopita kumalizika.

Mwanafunzi atekwa, azirai saa 14 Mbeya

 Kijana Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba mkazi wa Mama John kata ya Ilomba Jijini Mbeya ambaye alitekwa  akiwa akiwa anapelekwa uwani
 Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba  akiwa ameshikiliwa
 Majirani wakiwa wanasubiri kusikia kutoka kwa Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba
 Mama mzazi wa Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba Vumilia Komba akiwa anatoka kumtazama mtoto wake
 Vumilia Komba mama mzazi wa mtoto akiwa anataka kuulizwa maswali
 Mama mzazi wa kijana huyo Vumilia Komba  akihojiwa na waandishi wa Habari
 Ndugu jamaa na Marafiki pamoja na mzazi wa mtoto wakiwa wanatoa vitu vya mwanafunzi huyo
 Shati hili lilikuwa limechanwa ambalo ndilo lilitumika kuchanwa  na kumfunga mikono na kumziba mdomo


 Nguo pamoja na Viatu alivyokuwa amevivaa muhanga   wa tukioMjomba wa muhanga Kasian Mwezi Komba

Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba akifanya mazoezi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya

Emanuel Komba umri wa miaka (15)  kidato cha kwanza Shule ya sekondari Ilomba  akiwa amepata fahamu na kuelezea kisa kizimaWakiondoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya baada ya matibabu 

PICHA NA MBEYA YETU

Man City yapania kumnasa Ronaldo

http://i2.mirror.co.uk/incoming/article1867031.ece/ALTERNATES/s615/Cristiano-Ronaldo-1867031.jpg
Ronaldo
MANCHESTER, England
MANCHESTER City wameamua kuvunja benki kwa nia ya kumshawishi mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo atue katika uwanja wa Etihad katika kipindi hiki cha usajili.
Na wameiambia kambi ya Ronaldo kwamba wamejiandaa kuipiku ofa kutoka kwa Manchester United, jambo linalomaanisha kwamba wako tayari kumlipa mshahara wa zaidi ya paundi 300,000 (Sh. milioni 709) kwa wiki.
Man U wametumia miezi mitano iliyopita kujaribu kuandaa dili la kumrejesha Old Trafford nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, na Ronaldo mwenyewe ameshaonyesha kwamba bado timu hiyo iko moyoni mwake.
Man City wanatambua kuwa jambo hilo ni kiunzi kigumu kuruka, lakini mkurugenzi mtendaji wao Ferran Soriano na mkurugenzi wa soka Txiki Begiristain wote wamewaambia mawakala wa mchezaji huyo kwamba wako 'siriasi' sana na uhamisho huo.
Na wameweka wazi kwamba kama Real watakuwa tayari kumuachia Mreno huyo aondoke, watafanya kila liwezekanalo kuwapiku mahasimu wao Man U.
Mwenyekiti wa Man City, Sheik Mansur ameweka wazi kwa Soriano kwamba kama Ronaldo ataingia sokoni, City ni lazima wafanye chochote kinachowezekana kuhakikisha wanamsajili.
Ronaldo amebakisha miaka miwili katika mkataba wake Hispania, lakini licha ya kusema hadharani kwamba anakaribia kusaini mkataba mpya, Real bado hawajampa ofa yoyote ya mkataba mpya.
Jambo hilo linawaongezea matumaini Man U kwamba wanaweza kumnasa, ingawa mipango hiyo mipya ya Man City inaleta presha mpya Old Trafford.
PSG ndiyo klabu pekee ambaye kufikia sasa iliwasilisha ofa ya paundi milioni 55 ambayo Real waliikataa.
Klabu hiyo ya Ufaransa inajiandaa kumlipa pesa nyingi zaidi, lakini Ronaldo anafahamika kwamba anavutiwa zaidi kurejea Uingereza kama ataondoka Bernabeu.