STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 22, 2013

Paulinho alibeba Spurs ugenini, Man Utd ikilala 4-1

Sergio Aguero of Manchester City (16) celebrates as he scores their first goal during the Barclays Premier League match between Manchester City and Manchester United (Getty Images)
Kun Aguero akishangilia moja ya mabao yake ya leo yaliyoizamisha Manchester United
Wayne Rooney akiwa hoi

Paulinho
BAO la dakika za lala salama lililofungewa na Paulinho liliisaidia Tottenham Hotspur kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Cardiff City, huku Manchester United chini ya kocha wake David Moyes ikilala kwa mahasimu wao Manchester City kwa mabao 4-1.
Paulinho alifunga bao la Spur dakika ya tatu za nyongeza kabla ya mchezo huo kumalizika na kuipa timu yake pointi tatu muhimu zilizoifanya waende sambamba kileleni mwa msimamo na Arsenal iliyoshinda mapema mabao 3-1 dhidi ya Stoke City, japo inazidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa licha ya zote kufikisha jumla ya pointi 12.
Mabingwa watetezi Manchester United walijikuta wakipata kipigo cha aibu ikiwa na kocha wake David Moyes baada ya kunyukwa mabao 4-1 na Manchester City.
Mabao mawili ya Sergio 'Kun' Aguero, Yaya Toure na samir Nasir yalitosha kuipandisha City hadi nafasi ya tatu ikifikisha pointi 10 sawa na za Chelsea lakini ikiwa na uwianoi mzuri wa mabao ya kufunga na kufunga ikizipumulia Tottenham na Arsenal zilizopo kileleni.
Bao pekee la kufutia machozi ya Manchester United lilifungwa na nyota wake aliye katika kiwango cha juu kwa sasa Wayne Rooney.

Kipigo chaiporomosha Yanga, mabao 76 yafungwa mpaka sasa

Mabingwa watetezi
WAKATI mabingwa watetezi Yanga wakijikuta wakiporomoka kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi nafasi ya nane toka ile ya nne iliyokuwapo awali kabla ya pambano lao la leo dhidi ya Azam, jumla ya mabao 76 yameshatinga wavuni hadi sasa ligi ikiwa katika raundi ya tano.
Yanga imesaliwa na pointi zake sita na ikiwa nyuma ya wageni wa ligi hiyo Mbeya City yenye pointi saba, huku Azam na Coastal zikizipumulia maafande wa Ruvu ambazo zote zilichezea vichapo katika mechi zao leo.
Vinara Simba wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 11 na mabao yao 13 ya kufunga na kufungwa magoli manne, huku JKT Ruvu ikifuatia ikiwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ikiizidi Azam licha ya kulingana nao pointi 9 sawa na Ruvu Shooting na Coastal Union.
Azam yenyewe imefunga mabao nane na kuruhusu mabao matano, wakati JKT Ruvu imefunga mabao sita na kufungwa mawili na kuwa, ikifuatiwa na ndugu zao Ruvu Shooting waliofunga mabao sita na kufungwa matatu kisha Coastal iliyofunga magoli matano na kuruhusu nyavu zake zitikiswe mara mbili.
Kagera Sugar iliyoanza ligi kwa kusuasua ushindi wake wa jana dhidi ya Ashanti umeiweka katika nafasi ya sita ikiwa na pointi nane na kufuatiwa na Mbeya City wenye pointi saba kisha Yanga yenye pointi zake sita.
Oljoro JKT iliyokuwa nafasi ya pili toka mkiani imechupa hadi nafasi ya 11 mwa msimamo baada ya ushindi wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu ikifikisha pointi nne na kuirithisha nafasi hiyo Prisons-Mbeya huku Ashanti wakiendelea kuzibeba timu zote 13 za ligi hiyo ikiwa na poingti moja tu.
Mpaka sasa ligi ikijiandaa kuingia raundi ya sita siku ya Jumatano kwa pambano moja tu kati ya Rhino Rangers ya tabora itakayoialika Ashanti United mjini Tabora jumla ya mabao 76 yameshatinga wavuni, huku Tambwe Amissi wa Simnba akiongoza orodha ya wafungaji wenzake akiwa na mabao sita.
Tambwe anafuatiwa kwa mbali na washambuliaji nyota wa Yanga, Jerry Tegete na Didier Kavumbagu na Haruna Chanongo, mchezaji wenzake wa Simba wenye mabao matatu kila mmoja.
Angalia msimamo wa Ligi hiyo kwa sasa na orodha ya wafungaji pamoja na ratiba ya mechi zijazo.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014      
                                    P  W  D  L   F   A  GD  PTS
1.  Simba                      5   3   2   0  13  4    9   11
2.  JKT Ruvu                5   3   0   2   6   2    4    9
3.  Azam                       5   2   3   0   8   5    3    9
4.  Ruvu Shooting          5   3   0   2   6   3    3    9
5.  Coastal Union          5   2   3   0   5   2    3    9
6.  Kagera Sugar           5   2   2   1   6   3    3   8
7.  Mbeya City              5   1   4   0   5   4   1    7
8.  Yanga                       5   1   3   1  10  7   3   6
9.  Mtibwa Sugar           5   1   3   1   3  4   -1   6
10.Rhino Rangers           5   0   4   1   5  7   -2   4
11.Oljoro                       5   1   1   3   3   6  -3   4
12.Mgambo                   5   1   1   3   2  10 -8   4
13.Prisons                      5   0   3   2   2   8  -6   3
14.Ashanti                      5   0   1   4   2  11 -6   1

Wafungaji:

6- Tambwe Amisi (Simba)
3- Jerry Tegete , Didier kavumbagu (Yanga), Haruna Chanongo (Simba),
2- Jonas Mkude (Simba), Jerry Santo (Coastal Union),Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Paul Nonga (Mbeya City), Peter Michael (Prisons), Kipre Tchetche (Azam)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla, Haruna Moshi (Coastal Union), Henry Joseph, Betram Mombeki (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Hamis Kiiza (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris, Kipre Tchetche, John Bocco, Joseph Kimwaga (Azam), Mwagani Yeya, Steven Mazanda, Richard Peter (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Ayoub Kitala, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Juma Luzio, Masoud Ally, Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Salum Machaku, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Themi Felix, Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Godfrey Wambura, Clement Douglas (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary, Paul Malipesa (Oljoro JKT)

Mechi zijazo
Sept 25, 2013
Rhino Rangers vs Ashanti Utd

Sept 28, 2013

Yanga vs Ruvu Shooting
Rhino Rangers v Kagera Sugar
Mbeya City vs Coastal Union
Mgambo JKT vs Oljoro JKT

Sept 29, 2013

Ashanti Utd vs Mtibwa Sugar
JKT Ruvu vs Simba
Prisons vs Azam

Matokeo ya mechi zilizopita ni kama ifuatavyo:

Ratiba ya Ligi Kuu 2013-2014
DURU LA KWANZA
Agosti 24, 2013
Yanga vs Ashanti United (5-1)
Mtibwa Sugar vs Azam (1-1)
Oljoro JKT vs Coastal Union (0-2)
Mgambo JKT vs JKT Ruvu (0-2)
Rhino Rangers vs Simba (2-2)
Mbeya City vs Kagera Sugar (0-0)
Ruvu Shooting vs Prisons (3-0)

Agosti 28, 2013
Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar (1-0)
Rhino Rangers vs Azam (0-2)
JKT Ruvu  vs Prisons (3-0)
Mbeya City vs Ruvu Shooting (2-1)
Mgambo  vs Ashanti United (1-0)
Oljoro JKT vs Simba (0-1)
Yanga  vs Coastal Union (1-1)

Sept 14, 2013
Simba  vs Mtibwa (2-0)
Coastal Union  vs Prisons (0-0)
Ruvu Shooting va Mgambo JKT (1-0)
Oljoro JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Mbeya City  vs Yanga (1-1)
Kagera Sugar vs Azam (1-1)
Ashanti United  vs JKT Ruvu (0-1)

Sept 18, 2013
Prisons vs Yanga (1-1)
Simba vs Mgambo JKT (6-0)
Kagera Sugar vs JKT Oljoro (2-1)
Azam  vs Ashanti United (1-1)
Coastal Union  vs Rhino Rangers (1-1)
Mtibwa Sugar  vs Mbeya City (0-0)
Ruvu Shooting vs  JKT Ruvu (1-0)

Sept 21, 2013
Mgambo JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Prisons vs Mtibwa Sugar (1-1)
Simba vs Mbeya City (2-2)
Kagera Sugar vs Ashanti United (3-0)

Sept 22, 2013
JKT Ruvu vs Oljoro JKT (0-1)
Azam  vs Yanga (3-2)
Coastal Union v Ruvu Shooting (1-0)

Tevez akizidi kung'ara Italia, Inter yaua 7-0

Carlos Tevez
Tevez (10) akishangilia bao lake na wachezaji wenzake wa Juventus
 MSHAMBULIAJI nyota wa Argentina, Carlos Tevez ameendelea kung'ara kwenye Seria A baada ya leo kuisaidia Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hellas Verona, huku mabingwa wa zamani wa Ulaya, Inter Milan ikipata ushindi wa kishindo wa mabao 7-0 ugenini dhidi ya Sassuolo.
Tevez aliyetua kwa mabingwa hao watetezi wa Seria A akitokea Manchester City, aliifungia Juventus bao la kusawazisha dakika ya 40 baada ya  wageni wao kutangulia kwa bao lililofungwa na Cacciatore kabla ya Fernando Lliorente kufunga bao la pili na la ushindi sekundu chache kabla ya mapumziko.
Nayo Inter Milan ikiwa ugenini iliisulubu Sassuolo mabao 7-0, wafungaji wake wakiwa ni Palacio aliyefunga dakika ya 7, Taide dakika ya 23 na Pucino wa Sassuolo aliyejifunga dakika ya 33 na hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 3-0.
Mabao mengine yalifungwa na Alvarez, Diego Milito aliyefunga mawili na Cambiasso.
Katika mechi nyingine za ligi hiuyo Fiorentina ilipata ushindi ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta, Bologna kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Torino, As Roma kuizima lazio mabao 2-0 na Catania na Parma kushindwa kutambiana na muda mchache ujao itashuhudiwa pambano la kukata na mundu klati ya Ac Milan itakayoialika Napoli uwanja wa San Siro.















Yanga bado gonjwa, yanyukwa na Azam, JKT Ruvu 'nguvu ya soda', Boban anga'ra mkwakwani

'Muuaji' wa Yanga, Joseph Kimwaga akibebwa na wachezaji wenzake baada ya kuisidia Azam kushinda mabaop 3-2 leo Taifa.

MABINGWA watetezi Yanga bado wana hali mbaya msimu huu baada ya jioni ya leo kunyukwa mabao 3-2 na Azam katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa, huku bao la ushindi la Wana Lambalamba' likitupiwa kimiani dakika za nyongeza na chipukizi, Joseph Kimwaga.
Yanga ambao walitoa visingizio vya ubovu wa uwanja wa Sokoine-Mbeya kutokana na sare mbili ilizopata toka kwa wenyeji wao Mbeya City na Prisons, walishtukizwa kwa bao la mapema ya sekunde ya 33 lililofungwa na John Bocco 'Adebayor' bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusawazisha bao dakika nne tu ya kipindi hicho kupitia Didier Kavumbagu kabla ya mtokea benchi Hamis Kiiza 'Diego' kuiongezea Yanga bao la pili dakika ya 65.
Hata hivyo mtokea benchi wa azam na mfungaji bopra wa msimu uliopita, Kipre Tchetche kuifungia Azam bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika mbili baadaye baada ya Niyonzima kuunawa mpira katika haraki za kuokoa.
Wakati mashabiki wakiamini pambano hilo litamalizika kwa sate hiyo ya mabao 2-2, dakika mbili za nyongeza ziliztosha kuisaidia Azam kupata bao la tatu lililofungwa na Jospeh Kimwaga aliyeingia uwanjani kutokea benchi na kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga ambao hawakuamini kama timu yao imelala.
Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 9 na kuchupa hadi nafasi ya tatu nyuma ya JKT Ruvu ambayo jioni ya leo imedhihirisha kuwa ilikuwa na 'nguvu ya soda' kutokana na kukubali kipigoi cha pili mfululizo leo na maafande wenzao wa Oljoro JKT ya Arusha.
Bao la washindi liliwekwa kimiani na Paul Malipesa dakika ya 79 katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi na kusitisha makali ya Ruvu waliokuwa kileleni kabla ya kuenguliwa na Simba.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Coastal Union ya Tanga ilitakata nyumbani mjini Tanga baada ya kuilaza Ruvu Shooting kwa bao 1-0, bao lililotupiwa kimiani na kiungo mshambuliaji,  Haruna Moshi 'Boban'.
Hata hivyo Coastal iliwabidi wasubiri hadi kwenye dakika ya 82 kujipatia bao hilo lililowapa pointi tatu muhimu zilizowafanya wafikishe jumla ya pointi 9 na kushika nafasi ya tano ikiwa na pointi 9 sawa na timu za JKT Ruvu, Azam, Ruvu Shooting Stars zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Arsenal moto nchini yaibanjua Stoke 3-1 yarudi kileleni

Arsenal v Stoke City - Premier League
Bacary Sagna akishangilia bao lake jioni hii
VIJANA wa Arsene Wenger, Arsenal ya England imeendelea kutakata kwenye Ligi Kuu ya England baada ya jioni hii kuicharaza Stoke City kwa mabao 3-1 na kurejea kileleni mwa ligi hiyo ikiiengua Chelsea.
Arsena ikichezwa kwenye dimba la nyumbani la Emirates ilipata mabao yake  kupitia kwa Aaron Ramsey dakika ya 5 kabla ya Per Mertesacker kuongeza bao la pili dakika ya 36 kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mesut Ozil, ambaye aliiwezesha pia kupatrika bao la pili dakika ya 72 lililofungwa na Bacary Sagna.
Baop la kufutia machozi kwa wageni, Stoke lilitumbukizwa wavuni na Geoff Cameroon dakika 26.
Kwa ushindi huo Arsenal wamefikisha pointi 12 na kukalia usukani wa ligi hiyo ikiizidi Chelsea iliyoshinda jana mabao 2-0 dhidi ya Fulham ikisaliwa na pointi zake 10.
Katika mechi nyingine jioni ya leo, Swansea City ikiwa ugenini iliifumuaCrystal Palace kwa mabao 2-0. mechi nyingine ambazo zimetoka mapumziko sasa hivi mabingwa watetezi wapo hoi mpaka sasa wakiwa wamekandikwa mabao 4-0 na mahasimu wao Manchester City, huku Tottenham Hotspur wakiwa suluhu ya Cardiff City.

Unyama! Watu watatu wa familia moja wauwawa kinyama

WATU watatu wa familia moja jijini Mwanza, akiwemo kichanga cha miezi saba, wameuawa kwa kunyongwa, kukatwa mapanga kichwani na kuchinjwa mithili ya kuku.

Mauaji hayo yamefanyika kati ya saa 9 na 10 usiku wa kuamkia jana, katika Kijiji cha Ihyila, Kata ya Buhongwa, jijini humo.

Waliofikwa na mauti hayo ni baba wa familia, Jones Elias Luhinga (44), mama wa familia, Lusia Elias Luhinga (35), na mtoto Eliud Elias Luhinga (mwaka mmoja).

Inadaiwa mauaji hayo yametekelezwa na mtu mmoja fundi wa kujenga nyumba (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyekaribishwa siku tisa zilizopita na Jones.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya majirani na ndugu wa familia hiyo ya marehemu, mtu huyo alifanya unyama huo usiku wa manane, na kwamba alfajiri alioga kisha kuwafungia ndani watoto wengine waliokuwa wamelala na kutokomea kusikojulikana.

Mmoja wa ndugu wa marehemu Jones, aliyejitambulisha kwa jina la Benjamin Luhinga alinukuliwa akidai kuwa ndugu yake aliuawa kwa kuchinjwa kama kuku, kisha kukatwa panga katikati ya kichwa na upande mmoja wa juu ya sikio.

"Jones ni mjomba wangu, ameuawa kwa kuchinjwa hapa kwenye koromeo. Amekatwa na panga hapa kichwani na eneo hili la juu ya sikio. Lakini tumekuta mabegi yamefunguliwa, labda alikuwa akitafuta fedha.

"Binafsi nina shaka huenda mjomba wangu ameuawa kwa sababu za fitna au fedha aliyouza kiwanja huko Buswelu baada ya kulipwa na jiji na baadaye akaja kujenga huku Buhongwa," alisema.

Benjamin alisema fundi ujenzi anayetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo aliitwa na Jones na tangu awasili nyumbani hapo alikuwa akilala kwenye chumba cha watoto.

Alibainisha kuwa familia hiyo ina watoto tisa na haijulikani kwanini mtuhumiwa hakuwadhuru wengine nane waliokuwamo kwenye chumba alichokuwa akilala.

Inadaiwa kuwa mtoto aliyeuawa alikuwa amelala na wenzake na muuaji aliamua kumpeleka kwa mama yake ili akanyonye na ndipo alipokwenda kumnyonga.

Musa Sayi, mkazi wa Buhongwa alisema walipata taarifa za mauaji hayo jana alfajiri na walipofika walihisi kuna mtu amemaliza kuoga lakini hawakumuona.

“Mazingira tuliyoyakuta pale tulihisi kuna mtu anaoga, lakini hatukuona. Tulihisi ndiye muuaji labda amefanya mitambiko ya kichawi,” alisema.

Jeshi la Polisi kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza, Joseph Konyo (RCO), alisema Jones aliuawa kwa kukatwa panga kichwani na upande mmoja wa juu ya sikio, na si kuchinjwa kama kuku.

"Huyu baba mwenye nyumba yeye ameuawa kwa kukatwa panga katikati ya kichwa na likaingia sana na huku upande wa karibu na sikio. Hajachinjwa kama baadhi ya watu wanavyodai," alisema.

Konyo alisema walifika eneo la tukio hilo na kushuhudia miili ya marehemu hao.

Akizungumzia tukio la jana, RCO Konyo alisema yawezekana chanzo cha mauaji hayo yanatokana na fitna, visa na uhasama wa muda mrefu baina ya mwenye nyumba na baadhi ya watu na kuna uwezekano muuaji hakuwa peke yake.

Kamanda Konyo alisema polisi itawasaka wauaji hao ili iwafikishe kwenye vyombo vya sheria.

Tukio kama hilo limewahi kutokea Februari 16, 2010 huko Musoma mkoani Mara, baada ya watu 17 wa familia tatu za koo moja kuuawa kinyama na wengine watatu kujeruhiwa vibaya pamoja na ng’ombe kadhaa kuchinjwa huko Buhare.

Mauaji hayo ya Musoma yalielezwa kwamba yalikuwa ya kulipiza kisasi, baada ya kutokea wizi wa mifugo kisha watu kadhaa kuuawa miaka ya nyuma kabla ya mwaka huo 2010.

Mnamibia kuwania taji la IBF-Afrika Novemba

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AO9WimIAAAgLUj6xBwAAAB43WXc&midoffset=2_0_0_1_1294958&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331

DAR ES SALAAM, TANZANIA – Namibian Abraham 'Energy' Ndaendapo 10(3)-2(1)-0 will fight against a boxer to be named layer for the vacant "IBF Continental Africa Jr. Lightweight Title in November this year. Ndauendapo an elite boxer of hard punching club has elicited excitements in various quarters hence his nominal
 
The tournament will be promoted by one of the gurus of Namibian boxing fraternity Kinda Nangolo Managing Director of Kinda Boxing Promotions based in downtown Namibia  capital city of Windhoek. Kinda Nangolo himself a great former international boxier is a prominent businessman in Windhoek, the capital city of Namibia dealing with fish export among many business activities he is currently involved at.

 
 
Abraham Ndauendapo doing what he love most after hard training "listening to the music"
 
His company Kinda Boxing Promotions has highly contributed to the advancement of professional boxing in Namibia. Kinda Nangolo is proud to manage some of the most decorated IBF Continental champions in Gottlieb Ndokosho "The Bite" who is the current IBF AMEPG Featherweight Champion and the youthfulness King Albinus Felesianu, the current IBF Jr. Lightweight Youth Champion of the world.
 
Abraham "Energy" Ndaundendapo comes a long way to the professional boxing ranks and files, to the position that allows him to aim at the most prestigious IBF continental title in Jr. Lightweight. He had an awesomely amateur boxing career and pundits rank his future very high.
 
Watch this space as we build case for Abraham Ndauendapo of the Republic of Namibia as he lock on for the IBF Continental Africa Jr. Lightweight Title respectively!
 
Congratulations Abraham Ndauendapo and Kinda Nangolo. Africa is proud of YOU!

Nothing else like IBF/AFRICA as it advances the African interests to the Global professional boxing fraternity" 

They call it AFRICA….! We call it HOME. 


The United States Boxing Association (USBA) and International Boxing Federation (IBF) continental body to Africa, Middle East & Persian Gulf

Azam, Yanga leo ni vita kali Taifa

Kipre Tchetche na Nadir Haroub 'Cannavaro leo itakuwaje Taifa?
WACHEZAJI wa wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam FC ikiwa nyumbani.
Hata hivyo Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro amesema 'aah wapi...tunataka pointi tatu baada ya sare tatu mfululizo'.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Azam, wachezaji wa klabu hiyo iliyoshinda mechi moja na kupata sare mbili katika mechi zake nne za awali kama ilivyo kwa wapinzani wao, wamepania kushinda leo ili kutuliza mashabiki wao.
Ahadi ya wachezaji hao ilitolewa mbele ya Makocha Kally Ongalla na Ibrahim Shikanda, Mwenyekiti Said Muhammad, Katibu Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele kwenye kikao cha pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini mwenendo wa timu hiyo baada ya mechi nne za mwanzo za ligi.
 
Wachezaji hao wakiongozwa na John Bocco, Jabir Aziz na Salum Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika mechi zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri na bado ikashindwa kupata matokeo.
Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa kuanzia mechi ya leo ili kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.

Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa matokeo yaliyopita na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili kurudisha makali yaliyoifanya Azam kuwa timu ya kuogopwa.

Azam FC itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC ambapo katika mechi nne zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga. Lakini timu zote mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na idadi sawa ya pointi tatu 
Azam FC leo itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi yake itajazwa na David Mwantika.
Wakati Azam wakijipanga hivyo kocha Minziro wa Yanga amesema vijana wake wapo kamili kuhakikisha wanaitungua Azam ili kuwafukuzia watani zao Simba waliopo kileleni.
Yanga kama Azam wana pointi 6, tano nyuma na zile ilizonazo Simba wanaoongoza wa kiwa na pointi 11 baada ya jana kubanwa na Mbeya City.
"Hatukubali kuona tukiendelea kupoteza pointi, tumerejea kwenye uwanja wa Taifa, ambazo ni mzuri na kuwapa nafasi wachezaji kufanya wanavyofanya hivyo tunaamini ushindi ni lazima," alisema.
Alisema kikosi chao kitawakosa baadhi ya wachezaji akiwamo kiungo mkabaji, Salum Telela ambaye ni majeruhi, lakini akidai waliosalia wapo tayari kwa vita na kwamba Azam ikae chonjo.
Timu hizo zinakutana mwezi mmoja na ushei tangu zilipokutana kwene mechi ya Ngao ya Jamii na Azam kulala bao 1-0 lililofungwa na Telela. Pia hilo ni pambano la 11 la Ligi Kuu baina ya timu hizo tangu mwaka 2008 ambapo Yanga imeshinda mara 5 na kupoteza 3 na michezo miwili iliishia kwa sare.

Waliokufa katika shambulizi la kigaidi Kenya wafikia 39

Hekeheka kila mtu akisalimisha roho yake
Mwanajeshi akitafuta mbinu za kuwasaidia mateka mikononi mwa watekaji
Baadhi ya majeruhi wakisaidiwa
IDADI watu waliopoteza uhai katika shambulio la kigaidi linalohusishwa na kundi la Al Shaabab imefikia 39 mpaka sasa.
Wapiganaji hao walishambulia jengo hilo saa saba za mchana Jumamosi

Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.
Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.
Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.
Taarifa nyingine zinasema kuwa mpaka sasa majeruhi wa tukio hilo wamefikia 162.

BBC

Ngumi Dar watapata uongozi mpya, BFT yauruka kimanga


Baadhi ya viongozi waliochaguliwa kuiongoza Chama cha Ngumi Mkoa wa Dar es salaam (DABA) wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa uchaguzi huo Zuwena Kipingu  (katikati) na Mwangalizi mkuu wa uchaguzi, Remmy Ngabo.


Mwenyekiti wa Mkutano wa Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Masumbwi Mkoa wa Dar es salaam Zuwena Kibena katikati akizungumza baada ya kumalizika uchaguzi huo na kupatikana viongozi wake
Baadhi ya wajumbe kutoka klabu ya Ashanti ya Ilala wakifatilia uchaguzi huo kutoka kushoto ni Emmanuel Mgaya, Hamisi Manyota na Juma Mwalimu  wakifuatilia uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa ngumi mkoa wa Dar es Salaam (DABA) uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Bondia Karama Nyilawaila akifuatilia uchaguzi huo, ambao hata hivyo umepingwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).

Mweka hazina wa klabu ya Ashanti ya Ilala, Emmanuel Mgaya akitumbukiza kura yake
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Timothi Kingu akijinadi wakati wa kuomba kula

Baadhi ya viongozi wakipiga kula za kuchagua viongozi watakaokiongoza chama cha mchezo wa ngumi Mkoa wa Dar es Salaam DABA
Wamboi Mangore akiomba nafasi ya Ukatibu Mkuu
Mmoja wa Wajumbe Jafar Ndame akiomba Kura za Ujumbe wa Kamati ya Uhusiano Habari na Masoko.
Juma Uwesu akiomba kuchaguliwa kwa wapiga kula  ujumbe wa maendeleo ya vijana
Arnord Ngumbi akiomba nafasi ya ujumbe wa vilabu,wilaya na taasisi za umma
Mazimbo Ali akijinadi mbele ya wajumbe wa mkutano kumpigia kura katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

Happiness Watimanywa ndiye Redd's Miss Tanzania 2013


MISS Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 usiku wa Septemba 21, Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City na kuwashinda warembo wenzake 29.
Na Father Kidevu Blog
HATIMAYE kitendawili cha nani atanyakua taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 kimeteguliwa usiku huu na mrembo Happiness Watimanywa kutoka Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati kufanikiwa kutawazwa Mshindi wa taji hilo na kuwashinda warembo wengine 29 waiokuwa wakiwania taji hilo.
Nyota ya Happiness ilionekana dhahiri kung’aa vyema katika fainali hizo mwaka huu tangu pale alipofanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia nusu fainali.
Wakati Happiness akinyakua Taji hilo pamoja na zawadi ya Gari na kitita cha shilingi Milioni 8 nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo Latifa Mohamed kutoka Kitongoji cha Kigamboni na Kanda ya Temeke na nafasi ya Tatu ikienda kwa Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo.
Pamoja nao warembo wengine walio ingia hatua hiyo ya tano bora ni Lucy Tomeka na Elizabeth Prety.
Hii ndio tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013. Je nani hapa ataondoka na taji, gari na kitita cha Milio ni 8? Warembo hao kutoka kushoto ni Happiness Watimanywa (Miss Photogenic), Elizabeth Pretty, Clara Bayo (Miss Sports Women), Lucy Tomeka na Latifa Mohamed.