STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 22, 2013

Arsenal moto nchini yaibanjua Stoke 3-1 yarudi kileleni

Arsenal v Stoke City - Premier League
Bacary Sagna akishangilia bao lake jioni hii
VIJANA wa Arsene Wenger, Arsenal ya England imeendelea kutakata kwenye Ligi Kuu ya England baada ya jioni hii kuicharaza Stoke City kwa mabao 3-1 na kurejea kileleni mwa ligi hiyo ikiiengua Chelsea.
Arsena ikichezwa kwenye dimba la nyumbani la Emirates ilipata mabao yake  kupitia kwa Aaron Ramsey dakika ya 5 kabla ya Per Mertesacker kuongeza bao la pili dakika ya 36 kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mesut Ozil, ambaye aliiwezesha pia kupatrika bao la pili dakika ya 72 lililofungwa na Bacary Sagna.
Baop la kufutia machozi kwa wageni, Stoke lilitumbukizwa wavuni na Geoff Cameroon dakika 26.
Kwa ushindi huo Arsenal wamefikisha pointi 12 na kukalia usukani wa ligi hiyo ikiizidi Chelsea iliyoshinda jana mabao 2-0 dhidi ya Fulham ikisaliwa na pointi zake 10.
Katika mechi nyingine jioni ya leo, Swansea City ikiwa ugenini iliifumuaCrystal Palace kwa mabao 2-0. mechi nyingine ambazo zimetoka mapumziko sasa hivi mabingwa watetezi wapo hoi mpaka sasa wakiwa wamekandikwa mabao 4-0 na mahasimu wao Manchester City, huku Tottenham Hotspur wakiwa suluhu ya Cardiff City.

No comments:

Post a Comment