STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 22, 2013

Yanga bado gonjwa, yanyukwa na Azam, JKT Ruvu 'nguvu ya soda', Boban anga'ra mkwakwani

'Muuaji' wa Yanga, Joseph Kimwaga akibebwa na wachezaji wenzake baada ya kuisidia Azam kushinda mabaop 3-2 leo Taifa.

MABINGWA watetezi Yanga bado wana hali mbaya msimu huu baada ya jioni ya leo kunyukwa mabao 3-2 na Azam katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa, huku bao la ushindi la Wana Lambalamba' likitupiwa kimiani dakika za nyongeza na chipukizi, Joseph Kimwaga.
Yanga ambao walitoa visingizio vya ubovu wa uwanja wa Sokoine-Mbeya kutokana na sare mbili ilizopata toka kwa wenyeji wao Mbeya City na Prisons, walishtukizwa kwa bao la mapema ya sekunde ya 33 lililofungwa na John Bocco 'Adebayor' bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusawazisha bao dakika nne tu ya kipindi hicho kupitia Didier Kavumbagu kabla ya mtokea benchi Hamis Kiiza 'Diego' kuiongezea Yanga bao la pili dakika ya 65.
Hata hivyo mtokea benchi wa azam na mfungaji bopra wa msimu uliopita, Kipre Tchetche kuifungia Azam bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika mbili baadaye baada ya Niyonzima kuunawa mpira katika haraki za kuokoa.
Wakati mashabiki wakiamini pambano hilo litamalizika kwa sate hiyo ya mabao 2-2, dakika mbili za nyongeza ziliztosha kuisaidia Azam kupata bao la tatu lililofungwa na Jospeh Kimwaga aliyeingia uwanjani kutokea benchi na kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga ambao hawakuamini kama timu yao imelala.
Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 9 na kuchupa hadi nafasi ya tatu nyuma ya JKT Ruvu ambayo jioni ya leo imedhihirisha kuwa ilikuwa na 'nguvu ya soda' kutokana na kukubali kipigoi cha pili mfululizo leo na maafande wenzao wa Oljoro JKT ya Arusha.
Bao la washindi liliwekwa kimiani na Paul Malipesa dakika ya 79 katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi na kusitisha makali ya Ruvu waliokuwa kileleni kabla ya kuenguliwa na Simba.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Coastal Union ya Tanga ilitakata nyumbani mjini Tanga baada ya kuilaza Ruvu Shooting kwa bao 1-0, bao lililotupiwa kimiani na kiungo mshambuliaji,  Haruna Moshi 'Boban'.
Hata hivyo Coastal iliwabidi wasubiri hadi kwenye dakika ya 82 kujipatia bao hilo lililowapa pointi tatu muhimu zilizowafanya wafikishe jumla ya pointi 9 na kushika nafasi ya tano ikiwa na pointi 9 sawa na timu za JKT Ruvu, Azam, Ruvu Shooting Stars zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment