STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Mgambo yaifumua Coastal, Oljoro yapiga mtu

JKT Oljoro iliyoifumua Prisons Mbeya mjini Arusha
Mgambo inayoendelea kutesa timu kongwe kwa kuifunga Coastal 2-0 mjini Tanga
Rhino Rangers wameifanyia maajabu Mtibwa kwa kuilaza bao 1-0
 TIMU zilizopo katika hatari ya kushuka daraja, Oljoro JKT, Mgambo JKT na Rhino Rangers zimeibuka na ushindi katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ushindi wa timu hizo umezidi kufanya kinyang'anyiro cha timu za kutaka kushuka daraja kuzidi kunoga kwani hakuna aliyena uhakika mpaka sasa wa kushuka au kubakia katika ligi hiyo mpaka sasa ligi ikiwa kwenye raundi ya 24.
Mgambo ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ilipepetana na Coastal Union na kupata ushindi wa mabao 2-0.
Mabao ya washindi walitoka kuifumua Yanga wiki iliyopita yaliwekwa kimiani na Peter Malianzi, Boli Ajali
na 'Wazee wa Oman' wakishindwa kufurukuta kwa maafande hao ambao wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupona kuteremka Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wenyeji waliopo nafasi ya pili toka mkiani wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa Prisons-Mbeya. Shija Mkina ndiye aliyefunga bao la ushindi la Oljoro baada ya awali kutangulia kufunga kabla ya wageni kuchomoa.
Nayo timu ya Rhino Rangers inayoburuza mkia ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, bao hilo pekee la wenyeji likifungwa na Gideon Brown.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumatano kwa mechi ambazo zinaweza kuamua hatma ya ubingwa baona ya Yanga na Azam, wakati timu hizo zitakapokuwa viwanja viwili tofauti.
Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kupepetana na Kagera Sugar wakati Azam itawafuata Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Azam inaoongoza msimamo kwa pointi 53 na Yanga iliyoifumua JKT Ruvu jioni hii mabao 5-1 inafuatia ikiwa na pointi 49 na Mbeya inafuata na pointi 46 katika nafasi ya tatu, kisha Simba yenye pointi 37.

Rais JK, mkewe washiriki kumuangaMeja Jen. Msemwa


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa  aliyekuwa Kamishna wa Utafiti na maendeleo ya Jeshi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu Meja Jenerali Kevin Gerald Msemwa wakati wa hafla ya kuaga mwili wake iliyofanyika katika uwanja wa makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Upanga jijini Dar es salaam leo April 6, 2014. Meja Jenerali Msemwa alifariki April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam. 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kamishna wa Utafiti na maendeleo ya Jeshi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu Kevin Gerald Msemwa wakati wa hafla ya kuaga mwili wake iliyofanyika katika uwanja wa makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Upanga jijini Dar es salaam leo April 6, 2014. Meja Jenerali Msemwa alifariki April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam.

Malaga yachinja mtu 4 nyumbani

http://www.bettingtipository.com/wp-content/uploads/2013/04/granada_vs_malaga_121209a-480x330.jpg
MABAO mawili yaliyofungwa na Ignacio Camacho yaliisaidia Malaga kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 nyumbani dhidi ya Grenada katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Hispania.
Mfungaji huyo alifunga mabao yake katika dakika ya 14 na 37 na mengine mawili toka kwa Amrabat  kwa mkwaju wa penati na Juanmi yaliiwezesha Malaga kuzoa pointi tatu.
Amrabat alifungwa katika dakika ya 50 na lile la Juanmi lilifungwa kwenyue dakika ya 74 na kuwapa uongozi wenyeji wa mabao 4-0 kabla ya wageni kuchomoa bao moja dakika ya 78 lililofungwa na Yousef El Arabi.
Malaga imepanda hadi nafasi ya 11kwa kufikisha pointi 38 ikiipita Celta Vigo na wapinzani wao wameporomoka hadi nafasi ya 14 ikisaliwa na pointi zake 34.
Ligi hiyo baod inaongozwa na Atletico Madrid yenye pointiu 79 na kufuatiwa na Barcelona yenye pointi 78 kisha Real Madrid iliyokusanya pointi 76.

Lazio, Fiorentina, Roma zashinda Italia

http://e1.365dm.com/14/01/768x432/Lazio-Celeb-v-Inter_3062528.jpg?20140106200749
Lazio
http://hasilprediksibola.com/wp-content/uploads/2013/12/Prediksi-Sassuolo-vs-Fiorentina.jpg
Fiorentina
 KLABU za Lazio, Fiorentina na Roma zimezidi kujiimarisha katika nafasi zao za Ligi Kuu ya Serie A baada ya kupata ushindi katika mechi za ligi hiyo zilizochezwa leo.
Lazio wakiwa nyumbani na ikicheza pungufu ya mchezaji wake Biglia kuonyesha kadi ya pili ya njano na kufuatiwa nyekundu dakika ya 57, waliifumua Sampdoria kwa mabao 2-0 , yaliyotupia kambani na Candreva katika dakika 42 na Lulic kwenye dakika ya 73.
Roma wakiwa ugenini waliifumua bila huruma Cagliari kwa mabao 3-1, huku Sassuolo ikipata ushindi pia ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta na Catania ikafa nyumbani kwao mbele ya Torino, wakati Fiorentina iliishinda 2-1 dhidi ya wageni wao Udinese.
Baadaye usiku Parma watapepetana na Napoli katika 'bonge' la mechi linalosubiriwa kwa hamu kabla ya Jumatatu kushuhudiwa mitanange mingine ya ligi hiyo kwa watetezi Juventuskuikaribisha Lirvono na AC Milan kuwafuata Genoa.

Yanga yaua Taifa, Mtibwa yapigwa kidude Tabora

Mrisho Ngassa, akishangilia moja ya mabao yake matatu na Simon Msuva na Didier Kavumbagu
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jioni ya leo imegawa dozi nene kwa maafande wa JKT Ruvu baada ya kuwanyuka mabao 5-1 katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo na kuwafanya wawakimbie Mbeya City waliopo nyuma yao.
Mabao matatu (hat-trick) ya Mrisho Ngassa na mengine ya Didier Kavumbagu na Hussen Javu yalitosha kuifanya Yanga kuwafukuzia Azam wenye pointi 53, wakati wenyewe wamefikisha pointi 49 baada ya timu zote kucheza mechi 23.
Ngassa alifunga mabao mawili katika dakika ya 9 na 15 katika kipindi cha kwanza na Kavumbagu aliongeza la tatu dakika chache kabla ya kwenda mapumziko Yanga wakiongoza mabao 3-0.
Kipindi cha pili Ngassa aliongeza bao la tatu kwake na la nne kwa Yanga katika dakika ya 48 kabla ya Javu aliyeingia uwanjani sekunde chache kabla ya mapumziko kumpokea Hamis Kiiza aliyeumia akifunga bao la tano kwa shuti kali dakika ya 53.
Idd Mbaga aliifungia JKT bao la kufutia machozi katika dakika ya 84 kwa mpira wa kichwa baada ya krosi matata ya Damas Makwaya kushindwa kuokolewa na mabeki wa Yanga na mfungaji kuuchupia akimduwaza kipa Deo Munishi 'Dida'.
Mara baada ya pambano hilo lililochezeshwa na Israel Mujuni Ngassa alikabidhiwa mpira wake tofauti na ilivyowahi kutokea kwa Amissi Tambwe wa Simba aliyewahi kufunga mabao manne na kushindwa kupewa mpira wake kwa hat-trick walipoizamisha Mgmabo JKT kwa mabaop 6-0.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Tabora, Rhino Rangers ilijitutumua na kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Timu ya watoto wa Tanzania yatinga fainali Brazil


TIMU ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Hadi mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho.
Kwa matokeo hayo, Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.
Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi  akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2

Arsenal yasulubiwa na Everton x3

Romelu Lukaku
Romelu Lukaku akishangilia bao walipokuwa wakiisulubu Arsenal muda mfupi uliopita
NDOTO za klabu ya Arsenal kuweza kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England, imezidi kufifia baada ya mapema leo kudunguliwa mabao 3-0 na Everton.
Mabao ya Steven Naismith katika dakika ya 14 na jingine la Romelu Lukaku katika dakika ya 34 yalitosha kuwpaa uongozi wenyeji wa mabao 2-0 hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kulikuwa na kosa kosa za hapa na pale mpaka pale Mikel Arteta alipojifunga bao katika dakika ya 62 katrika harakati za kuokoa bao langoni mwake.
Kwea ushindi huo Everton imejiimarisha kwenye nafasi ya tano ikifikisha pointi 63 moja zaidi ya Arsenal waliosalia kwenye nafasi ya nne wakati ligi ikielekea ukingoni.
Ligi hiyo itaendelea tena muda mfupi ujao kwa Liverpool kuwa wageni wa West Ham United kabla ya kesho Tottenham Hotspur kuialika Sunderland kwenye uwanja wao wa White Hart Lane.

Panga pangua makamanda wa Polisi hii hapa, Shilogile dah!