STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Yanga yaua Taifa, Mtibwa yapigwa kidude Tabora

Mrisho Ngassa, akishangilia moja ya mabao yake matatu na Simon Msuva na Didier Kavumbagu
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jioni ya leo imegawa dozi nene kwa maafande wa JKT Ruvu baada ya kuwanyuka mabao 5-1 katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo na kuwafanya wawakimbie Mbeya City waliopo nyuma yao.
Mabao matatu (hat-trick) ya Mrisho Ngassa na mengine ya Didier Kavumbagu na Hussen Javu yalitosha kuifanya Yanga kuwafukuzia Azam wenye pointi 53, wakati wenyewe wamefikisha pointi 49 baada ya timu zote kucheza mechi 23.
Ngassa alifunga mabao mawili katika dakika ya 9 na 15 katika kipindi cha kwanza na Kavumbagu aliongeza la tatu dakika chache kabla ya kwenda mapumziko Yanga wakiongoza mabao 3-0.
Kipindi cha pili Ngassa aliongeza bao la tatu kwake na la nne kwa Yanga katika dakika ya 48 kabla ya Javu aliyeingia uwanjani sekunde chache kabla ya mapumziko kumpokea Hamis Kiiza aliyeumia akifunga bao la tano kwa shuti kali dakika ya 53.
Idd Mbaga aliifungia JKT bao la kufutia machozi katika dakika ya 84 kwa mpira wa kichwa baada ya krosi matata ya Damas Makwaya kushindwa kuokolewa na mabeki wa Yanga na mfungaji kuuchupia akimduwaza kipa Deo Munishi 'Dida'.
Mara baada ya pambano hilo lililochezeshwa na Israel Mujuni Ngassa alikabidhiwa mpira wake tofauti na ilivyowahi kutokea kwa Amissi Tambwe wa Simba aliyewahi kufunga mabao manne na kushindwa kupewa mpira wake kwa hat-trick walipoizamisha Mgmabo JKT kwa mabaop 6-0.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Tabora, Rhino Rangers ilijitutumua na kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

No comments:

Post a Comment