STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 6, 2014

Mgambo yaifumua Coastal, Oljoro yapiga mtu

JKT Oljoro iliyoifumua Prisons Mbeya mjini Arusha
Mgambo inayoendelea kutesa timu kongwe kwa kuifunga Coastal 2-0 mjini Tanga
Rhino Rangers wameifanyia maajabu Mtibwa kwa kuilaza bao 1-0
 TIMU zilizopo katika hatari ya kushuka daraja, Oljoro JKT, Mgambo JKT na Rhino Rangers zimeibuka na ushindi katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ushindi wa timu hizo umezidi kufanya kinyang'anyiro cha timu za kutaka kushuka daraja kuzidi kunoga kwani hakuna aliyena uhakika mpaka sasa wa kushuka au kubakia katika ligi hiyo mpaka sasa ligi ikiwa kwenye raundi ya 24.
Mgambo ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ilipepetana na Coastal Union na kupata ushindi wa mabao 2-0.
Mabao ya washindi walitoka kuifumua Yanga wiki iliyopita yaliwekwa kimiani na Peter Malianzi, Boli Ajali
na 'Wazee wa Oman' wakishindwa kufurukuta kwa maafande hao ambao wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupona kuteremka Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wenyeji waliopo nafasi ya pili toka mkiani wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa Prisons-Mbeya. Shija Mkina ndiye aliyefunga bao la ushindi la Oljoro baada ya awali kutangulia kufunga kabla ya wageni kuchomoa.
Nayo timu ya Rhino Rangers inayoburuza mkia ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, bao hilo pekee la wenyeji likifungwa na Gideon Brown.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumatano kwa mechi ambazo zinaweza kuamua hatma ya ubingwa baona ya Yanga na Azam, wakati timu hizo zitakapokuwa viwanja viwili tofauti.
Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kupepetana na Kagera Sugar wakati Azam itawafuata Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Azam inaoongoza msimamo kwa pointi 53 na Yanga iliyoifumua JKT Ruvu jioni hii mabao 5-1 inafuatia ikiwa na pointi 49 na Mbeya inafuata na pointi 46 katika nafasi ya tatu, kisha Simba yenye pointi 37.

No comments:

Post a Comment