STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 7, 2014

Liverpool yarejea kileleni, Spurs, Sunderland kumenyana leo

Steven Gerrard (wa nne toka kushoto) akishangilia moja ya mabao yake ya penati  dhidi ya West Ham
MIKWAJU miwili ya penati ilitumbukizwa wavuni na Nahodha Steven Gerrard katika kila kipindi yalitosha kuirejesha Liverpool kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 ikiwa nyumbani kwa West Ham United.
Gerrard aliifungia Liver penati ya kwanza dakika moja kabla ya mapumziko , japo bao hilo lilirejeshwa kwenye muda wa nyongeza na Guy Roland Demel na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa ya bao 1-1.
Kipindi cha pili kama kilivyokuwa cha kwanza, West Ham walionekena kukaza buti na kuwabana wageni wao, lakini faulo iliyochezwa langoni mwao dakika ya 71 ilisababisha Liver kupewa penati ya pili ambayo pia ilitumbukizwa na Gerrard na mpaka mwisho vijogoo vya Liverpool walikuwa washindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo moja kwa moja uliwarejesha Liverpool kileleni mwa msimamo baada ya Jumamosi kuenguliwa na Chelsea kutokana na kufikisha pointi 74, mbili zaidi ya ilizonazo vijana wa Jose Mourinho na nne zaidi ya Manchester City waliopo nafasi ya tatu japo wenyewe wana michezo miwili mkononi kwani imecheza mechi 31 na wenzake wa juu michezo 33.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa pambano moja tu kati ya Tottenham Hotspur itakayoikaribisha Sunderland katika pambano litakalofanyika kwenye uwanja wa White Hart Lane.

No comments:

Post a Comment