Carvalho akimpongeza Rodriguez |
James RodrÃguez alianza kuiandikia bao wenyeji katika dakika 18 akimalizia kazi ya Dimitar Berbatov, bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko licha ya kuwepo na kosa kosa za hapa na pale.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji na kuongeza uhai wa pambano hilo ambalo dakika ya 72 Monaco iliongeza bao la pili kupitia kwa Andrea Raggi na dakika nne baadaye Rodriguez aliongeza baop la tatu kwa mkwaju wa penati.
Wageni walicharuka na kujipatia bao la kujifutia machozi dakika mbili baada ya kufungwa bao la Monaco kupitia kwa Alejandro Bedoya akiunga mpira wa Audel.
Ushindi huo umeifanya Monaco kufikisha pointi 66 na kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao waliopo kileleni PSG kutoka 16 hadi kuwa 13 kwani vinara hao wanaongoza wakiwa na pointi 79.
Katika mechi nyingine za ligi Saint-Étienne ikiwa nyumbani kwao walilaziishwa sare ya bao 1-1 na Nice, huku Valenciennes wakikubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani kutoka kwa Olympique Lyon.
No comments:
Post a Comment