STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 10, 2013

Breaking Newzzz: Muigizaji nyota Kash afariki duniaJaji Khamis 'Kashi' enzi za uhai wake

 
Kash enzi za uhai wake
MUIGIZAJI nyota wa zamani wa kundi la Shirikisho Msanii Afrika, Jaji Khamis 'Kashi' amefariki dunia akiwa kalazwa hospitali ya Muhimbili.
Habari iliyotufikia jioni hii  zinasema kuwa Kash alifariki mchana wa leo hospitalini hapo alipokuwa amelazwa .
 Baadhi ya wasanii wenzake wa zamani wa kundi hilo lililotamba na maigizo yake kwenye kituo cha ITV, wamethibitisha kufariki kwa muigizaji huyo ambaye pia alikuwa akicheza filamu.
Kashi alitamba na wasanii wenzake kupitia michezo kama Tamu Chungu, Dumaza, Hatia, Gumbizi na mengine.
Wasanii waliokuwa akiigiza nao kabla ya kundi hilo kuzimika ni pamoja na Bakar Makuka 'Beka', Richard Mshanga 'Bosi Masinde', Samson, Vailet, Grace Mapunda 'Mama Kawele' na wengine.
Mwili wa muigizaji huyo unatarajiwa kuzikwa kesho Jumanne na msiba upo Kinondoni-Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho ya marehemu Kashi mahali Pema Peponi Ameen.

Man City yamtolea macho Al ShaarawySp

Stephan Al Shaarawy
KLABU ya Manchester City inamtolea macho mshambuliaji kinda wa Italia anayeichezea AC Milan, Stephan El Shaarawy, japo mchezaji huyo kuitaka klabu hiyo kufanya kweli kama kweli inamtaka amesisitiza kuwa hafikirii kung'oka katika klabu yake ya sasa.
Habari zilizoripotiwa na gazeti la The Sun linasema kuwa kinda hilo linatakiwa Etihad kwa kitita cha paundi Mil. 30, lakini mwenyewe amenukuliwa akisema hafikirii kuondoka San Sirro.
"Sifikirii kuondoka Milan, iwapo City ni kweli inanihitaji mimi, ifanye hivyo, lakini nataka kubaki AC Milan, Mara zote najihisi kujiamini kwa sapoti ninayopewa na klabu, kocha Massimiliano Allegri na timu nzima," alisema.
"Pia nawashukuru wote kwa kunisaidia kuwepo kwenye timu ya taifa ya Italia," alisema mkali huyo wa mabao.

TCRA yaichimba mkwara Star Tv, kisa kujitoa Startimes
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa kituo cha Star Tv katikka king'muzi cha Star Times.

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini, TCRA imeagiza kituo cha runinga cha Star tv kurejesha channel yake mara katika  Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA

Lwakatare akwama tena kupata dhamana

Lwakatare (kulia) na mtuhumiwa mwenzake Ludovick wakiwa mahakamani leo.
 Baadhi ya wanachadema waliofika mahakamani leo.
Lwakatare akifunguliwa pingu.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare, kwa mara nyingine ameshindwa kuwekewa dhamana leo katika kesi inayomkabili ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuru jijini Dar es Salaam. 

Sababu za kuahirishwa kesi hiyo ni madai ya hakimu kuwa hakuweza kupata muda wa kupitia mafaili ya kesi hiyo maana alikuwa likizo. Lwakatare amerudishwa Segerea na kesi yake imetajwa kurudishwa mahakamani kesho asubuhi (Juni 11 mwaka huu).

MAP kutumia michoro kutoa elimu dhidi ya Sickle Cell

Mchoro unaonyesha Red cell na tatizo la Sickle Cell
Na Suleiman Msuya
TAASISI ya Motion Art Production (MAP) inatarajia kufanya onyesho la michoro mbalimbali Juni 17 mwaka huu katika Jumba la Makumbusho ya Taifa lengo likiwa ni  kutoa elimu na ufahamu dhidi ya ugonjwa wa maumbile mabaya ya damu (sickle cell).
Hayo yamebainishwa na Mwasisi wa taasisi hiyo Honeymoon Aljabri wakati akizungumza na mwandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema watatumia maonyesho hayo kujadiliana na watu mbalimbali ambao watatembelea kuona michoro yao ambayo itakuwa inahusu rasilimali mbalimbali zilizopo hapa nchini kwa kutambua kuwa upo uwezekano wa kutokomeza ugonjwa huo ambao unau watu wengi.
Aljabri alisema ugonjwa huo wa sickle cell umesahaulika lakini takwimu zinaonyesha kuwa unamadhara makubwa kwa jamii hasa katika nchi zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo.
“Sisi tunajihusisha na mambo ya sanaa lakini nimekaa na kufikiri kuwa nina wajibu wa kutoa mchango wangu katika jamii kwa njia nyingine hivyo nitatumia michoro mbalimbali ambayo ninachora kutoa elimu na kujadiliana jinsi ya kutokomeza ugonjwa huu,” alisema.
Mwasisi huyo wa taasisi ya MAP alisema pamoja na kutumia maonyesho hayo pia wanatarajia kufanyua matembezi ya kilometa tano mwezi Septemba ambapo ni maadhimisho ya ugojwa huo.
Alisema katika matembezi hayo wanatarajia kuchangia damu pamoja vitu mbalimbali ili kuweza kuwasaidia waathirika wa ugonjwa huo hapa nchi.
Aljabri ametoa rai kwa Watanzania kuunga mkono juhudi hizo kwani madhara ya ugonjwa huo ni makubwa hivyo ni wajibu kwa kila mtu mwenye uwezo kuweza kusaidia ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea.
Aidha Mwasisi huyo wa MAP alisema pamoja na juhudi zao hizo malengo yao ya kudumu ni kufungua kituo cha taarifa ambacho kitasaidia watu wenye sickle cell kupata taarifa wapi wanaweza kupata huduma kwa urahisi.
Pia alisema kwa mwaka huu wataendesha kampeni hiyo katika mkoa wa Dar es Salaam  pekee lakini matarajio yao ni kuhakikisha kuwa kwa miaka ijayo wanafanya kazi katika maeneo yote ya nchi.

Salvatory Mtebe aitamani Simba

Mtebe (kushoto) akimdhibiti Jerry Santo
BEKI mahiri wa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar, Salvatory Mtebe aliyebakisha mwaka mmoja kabla
ya mkataba wake na klabu yake ya sasa kuisha amesema anatamani kutua Msimbazi, kuichezea Simba.
Aidha beki huyo wa zamani wa Kagera Sugar na Athletico ya Burundi, amejipigia debe akidai anaweza kuwa suluhu ya ukuta wa Simba ambao tangu umpoteze Kelvin Yondani na Joseph Owino 'haujatulia'.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo beki huyo wa zamani wa Taifa Stars, alisema pamoja na kwamba amebakisha mwaka mmoja wa mkataba wake na Mtibwa, angependa kutua Msimbazi moja ya
klabu kubwa na zenye mafanikio makubwa kisoka.
Mtebe alisema anadhani kutua kwake Msimbazi kuitaweza kutengulia kitendawili cha tatizo la beki
wa kati iliyonayo klabu kwa kipindi kirefu sasa kwa kujiaminia uwezo alionao.
"Mimi bado nina mkataba wa mwaka mmoja Mtibwa, lakini kama nitapata klabu ya kuichezea sintakuwa na tatizo, kuna wakati Simba walikuwa wakinifuatilia lakini wakasitisha mipango pengine kwa kukwepa gharama za uhamisho, lakini nadhani mie nitawafaa sana pale kati, alisema.
Mtebe alisema kama Simba itashindwa kumnyakua bado milango i wazi kwa klabu nyingine yoyote
itakayokuwa inamhitaji mradi imalizane na uongozi wa klabu yake kwa ajili ya uhamisho wake na kuahidi kuifanyia makubwa kama anavyofanya akiwa na kikosi chake cha sasa akiwa na uwezo pia wa kupachika mabao kama alivyofanya kwa msimu wa ligi ilioisha hivi karibuni.

Hali ya kiafya ya Mzee Mandela sivyo nzuri tumuombeeni

Nelson Mandela, Winnie, Jacob ZumaRais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela akisaidiwa kutembea na Rais wa Jacob Zuma kushoto na mke wake wa zamani, Winnie Mandela kulia katika picha ya hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini.
RAIS mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa huku akiwa amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela amb
aye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.

Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.Nelson MandelaMzee Mandela akifurahia jambo na watoto nyumbani kwake hivi karibuni.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.

Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.

Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.

Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.

Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.

Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela. 
 
BBC

KIBANDA USO KWA USO NA DK BILAL JIJINI DAR ES SALAAM


2 7b5b3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhariri wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, AbsalomKibanda, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 10, 2013 kwa mazungumzo. Kibanda alimtembelea Mhe. Makamu ili kumwelezea hali yake kiafya inavyoendelea baada ya matibabu. Picha na OMR

KIMWANA GLORY STEPHEN NDIYE REDD'S MISS ARUSHA 2013

 Mrembo alieshikilia taji la Redd's Miss Arusha Glory Stephen  akipungia watu walongina kuanglia kinyanganyiro hicho mara baada ya kutangazwa mshindi na fasi ya pili ikiwa imeshikiliwa na Nance Mushi
 Muaandaaji wa Redd's Miss kanda ya kaskazini Faustin Mwandago akiwa anawapongez warembo walioshinda kinyanganyiro cha Arusha na kuwaambia wote waliongia tano bora anawapa nafasi ya kushiriki kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini


 mgeni Rasmi wa sherehe za kumsaka mlibwende wa Arusha (Redd's Miss Arusha)John  Mongela  katikati afisa utamaduni wa jiji la Arusha akifuatia wa kwanza  kulia ni muaandaaji wa Redd's Miss kanda ya kaskazini Mwandago
Warembo waliongia katika hatua ya tano bora Redd's miss Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutanganzwa wa shindi
Chanzo:Libeneke la Kaskazini

Mada Maugo ajitosa CHADEMA ahimiza wengine kutojificha

Bondia Mada Maugo 'King Maugo Junior'
Mada Maugo (kulia) akiwajibika ulingoni katika pambano lake na mkongwe Rashid Matumla

BONDIA mahiri wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo ‘King Junior’, jana alitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam jana.

Maugo miongoni mwa mabondia machachari anayepigana uzito wa kati, alikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mabere Marando.

Akikabidhi kadi hiyo kwa Maugo, Mabere ambaye ni mwanasheria maarufu nchini, alisema CHADEMA ni chama cha wananchi wenye uchungu na nchi yao, hivyo milango ipo wazi kwa kila mwenye nia njema na taifa lake.

Alisema Maugo akiwa kijana mwenye nguvu, amefanya hivyo baada ya tafakuri ya kina na kubaini kuwa CHADEMA ndicho chama kinachoweza kuleta mageuzi ya kweli kwa wananchi wote bila kujali jinsia, dini, kabila wala itikadi.

Na kuwataka watu wengine wakiwemo nyota wa michezo na burudani kutojificha kama wanakipenda na kukiamini chama hicho kwa kujiunga nacho badala ya kujificha kwa hofu ya kuelewekwa vibaya kwa watu wao wa karibu.

Uamuzi wa Maugo ni mwendelezo wa vijana wenye majina makubwa kwenye jamii kujiunga na chama hicho.

Hivi karibuni msanii Joseph Haule ‘Professa J’ alikabidhiwa kadi ya chama hicho mjini Dodoma.

Swagger One aangusha tatu kwa mpigo

Swagger katika pozi
Filamu ya Jeshi la Mfu itakayoanza kutolewa kabla ya nyingine

Kava la filamu ya Salamu Toka Kuzimu
Muonekano wa filamu ya Katikati ya Jiji

MSANII wa zamani wa muziki wa kizazi kipya aliyejitosa kwenye uongozaji wa filamu, Hussein Ramadhan 'Swagger One' amerekodi filamu mpya tatu kwa mpigo za 'Jeshi la Mfu', 'Sauti Toka Kuzimu' na 'Katikati la Jiji'.

Akizungumza na MICHARAZO, Swagger aliyetamba na makundi ya Double W na Crime Busters, alisema filamu ya kwanza kutoka kati ya hizo ni 'Jeshi la Mfu' itakayofuatiwa na 'Sauti Toka Kuzimu' na kisha 'Katikati ya Jiji' inayozungumzia maisha halisi ya biashara ya miili inayofanywa na baadhi ya wanajamii nchini.

Alisema filamu zote hizo zimewashirikisha wasanii mchanganyiko wakiwamo wenye majina na chipukizi kwa lengo la kutoa ladha tofauti na pia ni kati ya filamu anazotarajia zitaleta mapinduzi katika tasnia hiyo kutokana na simulizi zake.

"Ni filamu za aina yake, sijisifu kwa vile nimeziandaa, ila ukweli ndivyo ulivyo siyo filamu za sebuleni na kulilia mapenzi, ni kazi za kusisimua ambazo tumezoea kuziona kwa watayarishaji na waongozaji wa kimataifa duniani," alisema.

Mtayarishaji huyo aliongeza kuwa amekuja na filamu za kusisimua ili kuondoa dhana kwamba soko la filamu limetekwa na masimulizi ya mapenzi tu.

"Nimekuja tofauti ili kuwapa fursa wasiofagilia filamu za kimapenzi wapate ladha nyingine ya kusisimua hasa hii ya 'Sauti Toka Kuzimu' au 'Jeshi la Mfu' ni kama filamu zile zinazozalishwa Hollywood kwa simulizi na mandhari zake, watu wasubiri kuziona," alisema Swagger.

Kabla ya kujitosa kwenye utayarishaji wa filamu, Swagger alianza kuigiza akishirikiana na mama yake aliyekuwa nyota wa michezo wa kuigiza sambamba na akina Mzee Majuto, Mzee Small, marehemu Mwanachia n Qudrat Olomoda maarufu kama 'Chombeza'.

Wakazi Moro waichoka CCM warejesha kadi
Baada ya kutoa hotuba nzito na zenye kugusa matatizo ya wananchi, wananchi hao walirudisha kadi zao na kwa kuwa kadi hizo lissu hakuja nazo akazichoma moto.

Credit:Mpekuzi Huru

MAGDALENA OLOTU AWA REDD'S MISS KIGAMBONI 2013


IMG_0566Mshindi wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed( wa pili kushoto) na Mshindi wa tatu Irene Rajab ( wa pili kulia) pamoja na mshindi wa nne na wa tano.
IMG_0570
IMG_0588Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.
IMG_0596Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.
IMG_0601Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.
IMG_0605Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.
IMG_0612Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile( na FullshangweBlogu)

Mengi awaonya wanaowania Urais 2015MWENYEKITI wa makampuni ya IPP Reginald Mengi ametoa ya moyoni kwa wote wenye mpango wa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka miwili ijayo.

Mengi ameyatoa maombi yake ya m
oyoni na kuyaweka hadharani kupitia akaunti yake ya twitter June 7, na hiki ndicho alichokiandika.

“Nawaombea Mungu wanaotaka Urais wasipokee mshiko wa mfanyabiashara fisadi mkubwa ambaye pia ni kinara wa madawa ya kulevya.”

Swali ni mfanyabiashara gani, hilo linaweza kuwa ni jiwe gizani kama yupo kweli aliyetajwa litakuwa limemfikia.

Chanzo: Upekuzi Huru

Washindi wa tuzo za Kili Music Awards 2013 hawa hapaAdd caption

WIMBO BORA WA RNB; RAMA DEE ft MAPACHA-KUWA NA SUBIRA

KIKUNDI BORA CHA TAARABU-JAHAZI MODERN TAARAB

MTUNZI BORA WA TAARABU-THABIT ABDUL

WIMBO BORA WA TAARABU;KHADIJA KOPA-MJINI CHUO KIKUU

MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA KWA TAARABU-ENRICO


MSANII BORA WA KIKE -TAARBU; ISHA MASHAUZI

MSANII BORA WA KIUME -TAARABU; MZEE YUSUPH

WIMBO WENYE VIONJO VYA ASILI-MRISHO MPOTO ft DITTO-CHOCHEENI KUNI

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI BONGO FLAVA-BEN POL

MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA-MUZIKI WA KIZAZI KIPYA; MAN WALTER

MSANII BORA WA KIUME BONGO FLAVA-DIAMOND
MSANII BORA WA KIKE BONGO FLAVA-RECHO

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI HIP HOP-KALA JEREMIAH

WIMBO BORA WA BONGO POP;OMMY DIMPOZ-ME AND YOU

MSANII BORA ANAYECHIPUKIA-ALLY NIPISHE

MSANII BORA WA KIUME-DIAMOND

KIKUNDI BORA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA-JAMBO SQUAD

MTAYARISHAJI CHIPUKIZI WA MWAKA-MENSEN SELECTA

WIMBO BORA WA BENDI;MASHUJAA-RISASI KIDOLE

MTUNZI BORA WA MASHAHIRI -BENDI; CHARLS BABA

MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA-BENDI ;AMOROSSO

MSANII BORA WA KIKE-BENDI ;LUIZA MBUTU

MSANII BORA WA KIUME-BENDI ;CHARLS BABA

BENDI BORA YA MWAKA-MASHUJAA BAND

WIMBO BORA WA ZOUK; AMINI -NI WEWE

WIMBO BORA WA REGGAE;WARRIORS FROM THE EAST-KILIMANJARO

WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL; DABO-PREDATOR

MSANII BORA WA HIP HOP-KALA JEREMIAH

WIMBO BORA WA HIP HOP; NAY WA MITEGO-NASEMA NAO

WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI;JOSE CHAMELEONE-VALUVALU

WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA;OMMY DIMPOZ ft VANESSA-ME AND YOU

WIMBO BORA WA MWAKA; KALA JEREMIAH-DEAR GOD

VIDEO BORA YA MWAKA;OMMY DIMPOZ-BAADAE

HALL OF FAME-KILIMANJARO BAND WANA NJENJE

HALL OF FAME-SALUM ABDALLAH YAZIDU

MSANII BORA WA KIKE-LADY JAY DEE