STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 10, 2013

Salvatory Mtebe aitamani Simba

Mtebe (kushoto) akimdhibiti Jerry Santo
BEKI mahiri wa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar, Salvatory Mtebe aliyebakisha mwaka mmoja kabla
ya mkataba wake na klabu yake ya sasa kuisha amesema anatamani kutua Msimbazi, kuichezea Simba.
Aidha beki huyo wa zamani wa Kagera Sugar na Athletico ya Burundi, amejipigia debe akidai anaweza kuwa suluhu ya ukuta wa Simba ambao tangu umpoteze Kelvin Yondani na Joseph Owino 'haujatulia'.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo beki huyo wa zamani wa Taifa Stars, alisema pamoja na kwamba amebakisha mwaka mmoja wa mkataba wake na Mtibwa, angependa kutua Msimbazi moja ya
klabu kubwa na zenye mafanikio makubwa kisoka.
Mtebe alisema anadhani kutua kwake Msimbazi kuitaweza kutengulia kitendawili cha tatizo la beki
wa kati iliyonayo klabu kwa kipindi kirefu sasa kwa kujiaminia uwezo alionao.
"Mimi bado nina mkataba wa mwaka mmoja Mtibwa, lakini kama nitapata klabu ya kuichezea sintakuwa na tatizo, kuna wakati Simba walikuwa wakinifuatilia lakini wakasitisha mipango pengine kwa kukwepa gharama za uhamisho, lakini nadhani mie nitawafaa sana pale kati, alisema.
Mtebe alisema kama Simba itashindwa kumnyakua bado milango i wazi kwa klabu nyingine yoyote
itakayokuwa inamhitaji mradi imalizane na uongozi wa klabu yake kwa ajili ya uhamisho wake na kuahidi kuifanyia makubwa kama anavyofanya akiwa na kikosi chake cha sasa akiwa na uwezo pia wa kupachika mabao kama alivyofanya kwa msimu wa ligi ilioisha hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment