Bondia Mada Maugo 'King Maugo Junior' |
Mada Maugo (kulia) akiwajibika ulingoni katika pambano lake na mkongwe Rashid Matumla |
BONDIA mahiri wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo ‘King Junior’, jana alitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam jana.
Maugo miongoni mwa mabondia machachari anayepigana uzito wa kati, alikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mabere Marando.
Akikabidhi kadi hiyo kwa Maugo, Mabere ambaye ni mwanasheria maarufu nchini, alisema CHADEMA ni chama cha wananchi wenye uchungu na nchi yao, hivyo milango ipo wazi kwa kila mwenye nia njema na taifa lake.
Alisema Maugo akiwa kijana mwenye nguvu, amefanya hivyo baada ya tafakuri ya kina na kubaini kuwa CHADEMA ndicho chama kinachoweza kuleta mageuzi ya kweli kwa wananchi wote bila kujali jinsia, dini, kabila wala itikadi.
Na kuwataka watu wengine wakiwemo nyota wa michezo na burudani kutojificha kama wanakipenda na kukiamini chama hicho kwa kujiunga nacho badala ya kujificha kwa hofu ya kuelewekwa vibaya kwa watu wao wa karibu.
Uamuzi wa Maugo ni mwendelezo wa vijana wenye majina makubwa kwenye jamii kujiunga na chama hicho.
Hivi karibuni msanii Joseph Haule ‘Professa J’ alikabidhiwa kadi ya chama hicho mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment