Mchoro unaonyesha Red cell na tatizo la Sickle Cell |
Na Suleiman Msuya
TAASISI ya Motion Art Production (MAP) inatarajia
kufanya onyesho la michoro mbalimbali Juni 17 mwaka huu katika Jumba la Makumbusho
ya Taifa lengo likiwa ni kutoa elimu na
ufahamu dhidi ya ugonjwa wa maumbile mabaya ya damu (sickle cell).
Hayo yamebainishwa na Mwasisi wa taasisi hiyo
Honeymoon Aljabri wakati akizungumza na mwandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam.
Alisema watatumia maonyesho hayo kujadiliana na watu
mbalimbali ambao watatembelea kuona michoro yao ambayo itakuwa inahusu rasilimali
mbalimbali zilizopo hapa nchini kwa kutambua kuwa upo uwezekano wa kutokomeza
ugonjwa huo ambao unau watu wengi.
Aljabri alisema ugonjwa huo wa sickle cell
umesahaulika lakini takwimu zinaonyesha kuwa unamadhara makubwa kwa jamii hasa
katika nchi zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo.
“Sisi tunajihusisha na mambo ya sanaa lakini nimekaa
na kufikiri kuwa nina wajibu wa kutoa mchango wangu katika jamii kwa njia
nyingine hivyo nitatumia michoro mbalimbali ambayo ninachora kutoa elimu na
kujadiliana jinsi ya kutokomeza ugonjwa huu,” alisema.
Mwasisi huyo wa taasisi ya MAP alisema pamoja na
kutumia maonyesho hayo pia wanatarajia kufanyua matembezi ya kilometa tano
mwezi Septemba ambapo ni maadhimisho ya ugojwa huo.
Alisema katika matembezi hayo wanatarajia kuchangia
damu pamoja vitu mbalimbali ili kuweza kuwasaidia waathirika wa ugonjwa huo
hapa nchi.
Aljabri ametoa rai kwa Watanzania kuunga mkono
juhudi hizo kwani madhara ya ugonjwa huo ni makubwa hivyo ni wajibu kwa kila
mtu mwenye uwezo kuweza kusaidia ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea.
Aidha Mwasisi huyo wa MAP alisema pamoja na juhudi
zao hizo malengo yao ya kudumu ni kufungua kituo cha taarifa ambacho kitasaidia
watu wenye sickle cell kupata taarifa wapi wanaweza kupata huduma kwa urahisi.
Pia alisema kwa mwaka huu wataendesha kampeni hiyo
katika mkoa wa Dar es Salaam pekee
lakini matarajio yao ni kuhakikisha kuwa kwa miaka ijayo wanafanya kazi katika
maeneo yote ya nchi.
No comments:
Post a Comment