STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 18, 2015

Yanga, Azam vitani tena viwanja tofauti kesho

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/DSC02166.jpg
Yanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdDjGKemN2sVnPU1l723rHo-UtuVjBZ673i-L4ZgSmKzLiH8dPrkov8VclFd1qQYP1c48z_omeSmeZFlSwvlBweJ0Ous2ja2z3bmlzGANL_dA-GQmz780dcej0AwtKL-Z13vKA-TDyjsQ/s1600/HERM5672-1.JPG
Azam
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam pamoja na wapinzani wao wakuu katika mbio za kuwania ubingwa wa msimu wa 2014-2015, Yanga kesho wanatarajiwa kushuka viwanja tofauti kusaka nafasi ya kujiimarisha kileleni mwa msimu wa ligi hiyo.
Yanga waliopo Mbeya wanatarajiwa kuvaana na Prisons katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, wakati Azam watakabiliana na maafande wa Ruvu Shooting katika pambano linalotarajiwa kuwa kali litakalochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Timu hizo mbili zilizotoka kwenye majukumu yao ya kuiwakilisha taifa katika michezo ya kimataifa ya Ligio ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho zote zipo kileleni zikiwa na pointi 25, Azam akitangulia kwa kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na wapinzani wao.
Azam wanarejea kwenye ligi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 5-2 kwenye uwanja wa Chamazi dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati Yanga ikitoka kuwafyeka Mtibwa mabao 2-0.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alinukuliwa mapema jana kuwa kikosi chao kipo tayari jijini Mbeya kugawa dozi kwa maafande hao wa Magereza kabla ya kumalizia kazi kwa Mbeya City Jumapili na kuanza safari ya kuwafuata Wabotswana wa BDF XI kwa mechi ya marudiano ya kimataifa.
Azam wenyewe kupitia Meneja wao, Jemedari Said imetamba kuitoa nishai Ruvu Shooting kabla ya mechi yao ya mwisho ya ligi kuanza safari kuelekea Sudan kurudiana na El Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumapili walishinda mabao 2-0.
Licha ya Yanga na Azam kutamba kujiandaa kugawa dozi kwa wapinzani, timu za Ruvu Shooting na Prisons inayoburuza mkia nazo zimetamba hawatakubali kufa kikondoo katika mechi hizo za kesho kwani hata wao wanazihitaji pointi tatu toka kwa vigogo hao.
Msemaji wa Ruvu Masau Bwire na Kocha wa Prisonsa, David Mwamaja walisema kwa nyakti tofauti kuwa wanahitaji ushindi kuliko kitu kingine katika mechi hizo za kesho kwa lengo la kujiweka katika nafasi nzuri ndani ya ligi hiyo iliyoanza  kushika kasi kwa mechi za duru la pili.

Bingwa wa FDL kujulikana J2 Taifa

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/DSC_4165.jpg
Mwadui Shinyanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX4CPi_gLzDiNDFJxODqQK-bun_Lz_-fqogmOSBafonpNyQztxKsciMrA9kx7T2CAkfa14juJT5WVK1BxZPxkqTuD40uPWHMTtpatpKUHMvQpdWau2Aw3yYJfbYrgwYFAnwHWaIEFpT7c/s1600/sports.JPG
Aficans Sports 'Wana Kimanumanu
KLABU za African Sports  ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa fainali  kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema kwa mujibu wa Kanuni, ni lazima apatikane mshindi mmoja ambaye ni bingwa.
“Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans,”alisema.
Alisema  timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka  Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.
Katika hatua nyingine, Rais wa TFF  Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma),  Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
 Katika salamu zake  Malinzi alisema klabu hizo zinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.
 Kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL 2015/2016,” alisema.

KWA UCHAFU HUU ELIMU TANZANIA ITAPANDA KWELI?!



Haifahamiki ni wanafunzi wa shule gani ya Sekondari, lakini hii ni taswira ya kitu gani kinachoendelea katika shule zenu nyingi na sababu ya kupatikana kwa division ziro lukuki

Rais wa FIFA alaani ubaguzi wa mashabiki wa Chelsea

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02939/sepp-blatter_2939007b.jpg
Rais wa FIFA, Sepp Blatter aliyekerwa na kitendo chga kibaguzi kilichofanywa na amshabiki wa Chelsea dhidi ya mtu mweusi mjini Paris.
PARIS, Ufaransa
RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Soka Sepp Blatter amewalaumu mashabiki wa klabu ya Chelsea, kwa kitendo chao cha kumzuia mtu mweusi kuingia ndani ya treni huku wakiimba nyimbo za kibaguzi jijini hapa.
Blatter amelaaini kitendo hicho kilichofanywa na baadhi ya mashabiki hao wa Chelsea cha ubaguzi wa rangi dhidi ya mtu huyo mweusi na kumzuia kuingia katika treni jana Jumanne.
Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wameonekana katika mkanda wa video wakizuia mlango wa treni kabla hawajamsukuma mtu huyo huku wakiimba nyimbo za kibaguzi: 
"Sisi wabaguzi, sisi wabaguzi na hicho ndicho tunachokitaka."
Tukio hilo lilitokea baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya uliofanyika jijini hapa na Chelsea kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Paris Saint-Germain kwenye uwanja wa Parc des Princes, huku klabu hiyo ikijibu haraka kuwa kitendo hicho sio cha kiungwana.
Ni wiki moja tu baada ya kocha wa zamani wa AC Milan Milan Arrigo Sacchi kutoa kauli kuwa "kuna weusi wengi" katika ligi ya vijana ya Italia, ambapo Blatter akijibu matukio yote hayo katika mtanda wake wa kijamii wa Twitter.
Matukio ya kibaguzi katika michezo yamekuwa kama ugonjwa sugu, huku adhabu dhidi ya wahusika yakielezwa kuruhusu kuendelea kuyahamasisha.

Jeshi Nigeria ladai kuua Boko Haram 300

http://d.ibtimes.co.uk/en/full/1418176/nigeria-boko-haram-2000-feared-killed-after-baga-attacked-second-time-days.png
baadhi ya wapiganaji wa Boko haram wakiwa 'kamili' na zana zao
ABUJA, Nigeria
ZAIDI ya wanamgambo 300 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika zoezi la kijeshi huko Kaskazini-Mashariki ya Nigeria, limesema jeshi la Nigeria.
Baadhi ya askari wamekamatwa na silaha kadhaa zimeharibiwa, alisema msemaji wa jeshi hilo, Chris Olukolade.
Pia katika tukio hilo askari wawili walipoteza maisha yao na wengine 10 walijeruhiwa wakati wa zoezi hilo la siku mbili huko katika jimbo la Borno, aliongeza.
Hatahivyo, vifo hivyo havijathibitishwa.
Jeshi la Nigeria lilituhumiwa katika siku zilizopita kuwa limekuwa likitoa taarifa za uongo kuhusu kujeruhiwa kwa maadui.
Boko Haram wamevamia raia huku wakiwaua maelfu wa askari tangu kundi hilo lianzishe vurugu kwa ajili ya kuanzisha taifa lao la kiislamu mwaka 2008.
Nigeria, Chad, Cameroon na Niger hivi karibuni vimeunda jeshi la muungano na kudai kuwa limekuwa likifanya vizuri dhidi ya Boko Haramu.
Tisho la kundi hilo linaelezwa ndiyo sababu ya kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu wa nchini huo uliokuwa ufanyike Jumamosi iliyopita na kupelekwa mbele hadi majuma sita yaani Machi 28.

Rooney aomba radhi kwa kujirusha

http://a2.fssta.com/content/dam/fsdigital/fscom/Soccer/images/2015/02/18/021815-Soccer-Manchester-United-Rooney-PI-CD.vadapt.620.high.0.jpgGOLIKIPA wa klabu ya Preston, Thorsten Stuckmann amesema Wayme Rooney alimuomba radhi kwa jinsi alivyodanganya na kupata penati katika mchezo wao dhidi ya Manchester United waliofungwa mabao 3-1. Rooney alianguka katika eneo la hatari baada ya kile kilichoonekana kama kuguswa na Stuckmann. Stuckmann alikaririwa na gazeti la The Sun akidai kuwa Rooney alimfuata na kumuomba radhi kwani ilikuwa nafasi yake ya kupata penati na alilazimika kuitumia.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alifunga penati hiyo na kuihakikishia nafasi United ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal.
Kitendo hicho cha Rooney kilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wachambuzi wa soka lakini aliungwa mkono na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roy Hodgson na mchezaji mwenzake wa zamani Phil Neville ambao walidai alijirusha ili kumkwepa golikipa.
Stuckmann mwenye umri wa miaka 33 amesema suala hilo liko wazi kuwa ile haikuwa penati lakini walipewa kwa sababu wenyewe ni United na kama ingekuwa mchezaji wao ndiye angefanya vile hadhani kama angepewa mkwaju huo.

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

Mourinho akiri sare ilikuwa kama zali kwa PSG

http://images.dailystar-uk.co.uk/dynamic/58/photos/879000/161879.jpg
Kipa aliyeibeba Chelsea jana ugenini dhidi ya PSG
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekiri kikosi cha kilikuwa na bahati kupata sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya timu 16 bora dhidi ya Paris Saint-Germain. 
Katika mchezo huo Branislav Ivanovic ndiye aliyeifungia Chelsea bao la kuongoza kabla ya Edinson Cavani hajasawazisha. 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Mourinho amesema ukiona jinsi golikipa wake Thibaut Courtois alivyokuwa akiokoa michomo mingi ya wapinzani hakuna shaka kuwa ilikuwa bahati kwao kuibuka na ushindi. 
Mourinho amesema sasa karata iko upande wao kwani mchezo huo utaamuliwa katika Uwanja wa Stamford Bridge baada ya wiki mbili zijazo.

Rais Kikwete apangua Ma-DC, Mwakalebela, Kisu waula!

https://pamelamollel.files.wordpress.com/2013/02/frederick-mwakalebela.jpg
Mwakalebela

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/12/kiss.jpg
Shaaban Kissu (kulia)

Na Rahim Junior, Dodoma 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete ameendelea kufanya panga pangua katika serikali yake baada ya kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Ma-DC wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya awali.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, leo mchana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni; Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilaya ya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Mtangazaji wa TBC, Shaaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Waliotenguliwa uteuzi wao lakini watapangiwa majukumu mengine ni'; Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa; ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).